Mwenyezi Mungu atusamehe Wana Kamati ya Ushindi ya Simba Sports Club kwani tulichokifanya wiki nzima hadi leo tumeibuka na Ushindi huu wa aina yake ni KUFURU kubwa mno Kwake. Tunamshukuru Mtaalam wetu yule Mama mwenye ziwa moja wa Zanzibar, Ndugu zetu wa Kiufundi watu wa Mkwajuni Zanzibar, Majirani wazuri wa Uwanja wa Taifa na Askari mmoja mwaminifu kabisa wa Uwanja wa Taifa kwa ushirikiano wenu mzuri. Tunashukuru kuwa tulichokifukia tumeshakiondoa na kukirudisha kunakostahili na wenye nacho wakakichukue na waendelee na taratibu zao zingine.
Mwisho kabisa tuwashukuru wana Yanga hasa hasa Bwana Salum Mkemi ambaye majuzi tu aliwazuga wana Yanga FC kwa kuitisha Press Conference na kutamba kuwa Yanga leo itaifunga Simba Sports Club goli 10 huku akiitukana Simba kwa Shombo zote kwani kwa kusema ukweli kama Wana Yanga FC watataka kujua ni nani kawaharibia leo kila kitu basi ni Mwanachama wao huyu ( Salum Mkemi ) ambaye wao wanadhani ni mwenzao lakini sisi Wana Simba Sports Club ndiyo Mtu ambaye tumekuwa tukimtumia 100% kuiua Yanga FC kuanzia zile Goli 5 hadi hii ya leo.
Najiandaa kwenda Kanisani Kesho kutubu kwa Maulana kwa shughuli Pevu tuliyoifanya leo na ambayo haielezeki na inatisha kuisikia pia. Poleni sana Wana Yanga FC na kwa hizi points 2 ambazo tutawaacheni nazo mkitukamata nazo katambikeni mizimu yenu ila kwa sasa nijuavyo ni kwamba Simba Sports Club tayari ni Bingwa kwa 85% kwani endapo tutashinda Mechi zetu 5 tu mfululizo kuanzia hiyo ya tarehe 4, March 2017 dhidi ya Mbeya City uwanja wa Taifa basi Ubingwa unakwenda rasmi Msimbazi kwao Simba Sports Club.