kiatu kipya
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 3,269
- 1,977
Shubaamit!!!! Wale chura hawana hamu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Upo??hahaha dah jamani acheni hizo....mnyama leo lazima atoroke town na kurudi porini maana tutamchinja
Vipi mshapoteana au bado??Pamoja figisu figisu zenu mliomfanyia mwenyekiti wetu kupitia kwa wanachama wenu siro na makonda leo wamatopeni tutawatandika 3 kwa beseni ili mwende mkapoteane kabisaa
kama nataka kuamini kilichoandikwa ni kweli vile , but napata shaka hizo red kadi 2 mbona hazikuonekana?
Ijumaa tunakuitaji centralHujaiona hiyo 1 iliyotolewa Mkuu? Unajua tulivyohangaika kuihangaikia Kiutamaduni ( Kindumba ) hiyo nyingine isitolewe? Kile Kipepsi cha Abdi Banda alichompiga Haji Mwinyi Ngwali na kile Kitendo cha Beki wetu Novatus Lufunga kucheza ile Faulo iliyowapa Penati Yanga FC unadhani Kisheria pale Referee hakupashwa kutoa straight red card Kwao? Uchawi tulioutumia Simba Sports Club jana Mkuu ni wa Kafara kubwa na mbaya sana ambao hata nikiuelezea humu Watu mnaweza mkaogopa hata siku zingine kuja Uwanjani. Wakati Yanga FC wanaingia Uwanjani na kupitia Geti lisilo la Kawaida unajua Wachezaji wote waliposhuka kuna Mtu gani wa Simba tena Mwanamke ila tulimvalisha Jezi ya Yanga FC aliokota nini pale? Na alivyokiokota alikiweka wapi kisha kuna Askari mmoja wa Uwanjani walio chini ya TFF alikuja na kukichukua kisha akakiwahisha kwa Mtaalam wa Simba SC ambapo aliweza kukifanyia Kazi japo kilishindana kwa Mchezaji mmoja tu Simon Msuva ambaye jana kwa taarifa yako tu ndiyo alibeba dawa zote za Kindumba za Yanga FC. Tulihangaika mno kummaliza Simon Msuva hadi tukasubiri mapumziko yafike ambapo wakati anatoka kuja Vyumbani kuna Mtu mmoja wa Simba alikuwepo pale chini jirani na wale Waandishi wa Habari wa Azam Tv tulimpaka kitu mikononi kisha tukamlazimisha apeane mikono na Msuva na Kazi yetu ikawa imeshaisha na kama ulifuatilia mpira Simon Msuva wa Kipindi cha Kwanza hakuwa wa Kipindi cha Pili. Tuliwaua Wachezaji wote wa Yanga FC nguvu na hasa miguu yao na wakawa wazito huku Kazi kubwa akiwa alishaimaliza Golikipa Wetu Daniel Agyei ambaye jana ndiyo tulimbebesha Mzigo ( Ndumba ) na kama utakumbuka wakati anaingia Uwanjani akiwa na Kipa mwenzake Manyika Peter JR alikuja usawa wa Uwanja akawa anatambaa na mstari wa katikati ya Uwanja huku anatoa Mbegu fulani ( chakula cha Ndege Bundi ) katika Chupi yake kisha anazitupa na aliweza kufanya hivyo mara 3 na akamaliza na kuendelea zake na Mazoezi.
Mkuu nina mengi ila naomba tu niishie hapa na tunashukuru tu kuwa jana Simba Sports Club tumeshinda lakini nikuambie tu ambacho hukijui ni kwamba kwa aina ile ya Kafara tulilolifanya jana pale Uwanjani kama Simba Sports Club tusingeshinda basi kuna Kiongozi wa juu mmoja wa Simba angefariki pale pale au ajali moja kubwa mno ingetokea maeneo yale yale ya Uwanja kwani tulichokifanya jana ni KUFURU si tu kwa Mwenyezi Mungu bali nadhani hata kwa Mkuu wa Mashetani mwenyewe LUCIFER.