Jana Azam TV na promoter walio dhamin mapambano sikuona kama walitaka kukuza Mchezo wa ngum na kuuendeleza Bali kuuharibu kabisa
Mapambano ya Jana Hasa lile la Mwisho la Mfaume Mfaume kila mtu kuanzia walio kua ndan ya ukumbi nje ya ukumbi mpaka Azam wenyewe walishangaa how Mfaume Mfaume Ameshinda kwa jinsi alivyo pigwa?
Tanzania Roho mbaya tu ndio inatusumbua Baadh ya wadhamin wanataka kulazimisha kila mtu awe Bingwa ili tu waweze kupata mapambano Sawa ni vizur basi tafuten mabingwa wa kweli Sasa kwa uozo kama ule anatoka mbele eti namtaka Mwakinyo Mwakinyo si atamuua?
Pambano ya Jana kidogo unaweza Sema alie stail kuitwa Bingwa ni Dulla Mbabe japo Ana tatizo la kuachia Sana ngum, za sura zimfikie sababu hil ni mbaya mana kama Bondia Ana pumz akikaza mpaka raund ya mwisho basi Dulla mbabe atakua kapigwa kwa point na Ndio mana Twaha kiduku Alimshinda.
Ila naamin Twaha kiduku Akirudia na Dula mbabe Ameisha na kama kwel Anaona yeye ni Bingwa na Anastail kupigana na Mwakinyo basi na Yeye akubali Kurudia pambano kwanza na Dulla mbabe aone kama atatoboa
Mapambano ya Jana Yameshusha hadh na Heshima ya Ngum za Sasa Ambazo Mwakinyo kapambana mpaka kufanya mchezo wa ngum uwe na uwezo wa kuingiza watu Zaid ya maelf kwa usiku mmoja embu mpeni mwakinyo Heshima yake msitake kila mtu awe bingwa ubingwa acha autafute mwenyewe msiwabebe
Pia wachambuz wa Jana na wao walikua mashabiki wa mabondia wa tanzania sijui kama ndio sheria ilivyo ama laa Lakin Jana ilikua kituko na ilionyesha dhahir kua Baadhi ya Mabondia wengi hawampend Mwakinyo kwa kuangalia mwakinyo akiwa anapambana wanavyo chambua mchezo na mabondia wengine wakiwa wanapambana Mara nyingi akiwa mwakinyo Hua wanaponda Aina ya upiganaj wake ila wakiwa Hawa Mabondia uchwara Sasa utasikia Leo anaua mpinzani hafikish raund ya Tatu Mara mpige mbavu ya kulia tumbon ehe ehe shame on you Tanzania
Sasa kama Jana Yale Makelele yote ya mchambuz juu ya mpinzani kushambuliwa na mchambuz jua anakipaza saut plas mashabiki mpinzani unafikir atakua huru kurusha ngum au ndio kumtoa mchezon kisaikolojia?
Azam TV na promoter wengine kama kwel mnataka watu waendelee kuangalia Ngum tanzania Bado mwakinyo ananafas ya kufanya ivyo ila mkitaka mlazimishe Hawa Mabondia VITAMBI wenu mlio wapa ubingwa kwa kupigana wao kwa wao zitarud zama za kina cheka promota tbc na eatv kiingilio Buku na bado watu Mia hawafiki
Azam na promoter mnatakiwa mjisafishe juu ya aibu ya Jana either kwa kuwafukuza wale majaj au kuwasimamisha
Pia mpeni mwakinyo pambano aje haraka kulinda Iman na heshima ya ngum ilio kua tayar ipo kabla haijapotea najua anataka hela nyingi ila mkumbuke yeye ndie star wa mchezo