Kwa yaliotokea Jana usiku wa mabingwa haraka Mwakinyo aandaliwe pambano

Kwa yaliotokea Jana usiku wa mabingwa haraka Mwakinyo aandaliwe pambano

Allafrica.

Allafrica
Mkuu nimesoma hiyo article yote sijaona sehemu wamesema kuwa mwakinyo ni bondia namba 1 africa kwenye uzito wake, labda unisadie wewe kama umeona, lakini pia hiyo website haipo special kwa ajili ya boxing ispokuwa inatoa habari zote mchanganyiko, na wanaelezea namna ambavyo boxing inaweza kuwa fursa Tanzania kwa kutumia mfano wa mwakinyo, mwongozo please
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mwakinyo anastahili heshima aliyoitafuta mwenyewe nje ya nchi. Kaenda nje bila watu kujua zaidi ya watu wachache walio karibu naye, watu tumeshtuka baada ya kuanza kupata taarifa mitandaoni kuwa kuna mtanzania kapiga mtu huko Uingereza kabeba mkanda. Ndio tukaanza kumfuatilia mtandaoni na kujua jamaa kuwa hata vifaa vya mazoezi vya kisasa hakuwa navyo zaidi ya matairi yaani ilikuwa "from zero to hero" Sasa hawa wakina Kiduku na wengineo waache kukurupuka badala ya kupoteza muda sijui wanaomba mapambano na Mwakinyo na wao si waende wakawatandike wazungu huko warudi na mikanda dunia itawatambua kama inavyomtambua sasa Mwakinyo badala ya kung'ang'ania kila siku ooh namtaka Mwakinyo namtaka Mwakinyo. Kuna wazungu kibao wapo huko wanataka mabondia wa kuwapiga ili waongeze rekodi zao na kupanda ngazi. Sasa hao ndio wazuri badala ya hao wazungu kuweka rekodi wakina Twaha Kiduku wao ndio waende wakapindue meza kama Mwakinyo watengeneze rekodi zao kama Mwakinyo iwapo kweli wana uwezo huo. Vinginevyo kelele zao zitabaki blah blah na kupotezeana muda tu wakati jasiri muonyesha njia Mwakinyo kashawaonyesha njia ya kupita ili waweze kufanikiwa.

Kwenye kupromoti ngumi kati ya Azam na Mwakinyo kiukweli wote Mwakinyo na Azam wanastahili pongezi sana na ndio wamefanya wengi wetu tuanze kupenda tena ngumi mchezo uliokuwa umekufa kabisa. Kwa sababu kabla ya Mwakinyo kushinda nje ya nchi hata hao Azam walikuwa hawana ujasiri wa kudhamini ngumi na zaidi wangepoteza fedha zao. Kwani kila mdau wa michezo anajua ujanja ujanja ulio kuwa unaendelea kwenye mchezo wa ndondi kiasi ulikuwa unaonekana mchezo wa kitapeli tapeli na upangaji wa matokeo. Jiulizeni ilikuwaje kila bondia aliyekuwa anaenda nje alikuwa anapigwa tena raundi za mwanzo kabisa na hata wakirudi walikuwa hawasikitiki na kila siku walikuwa wanapishana uwanja wa ndege kwenda nje kupigwa..
 
Twaha akirudiana na Dulla atafanya nini eti [emoji1529][emoji1529][emoji1529]?
 
Yani mwakinyo apigane na watu wa ndondo mwakinyo levo zingine
 
Uyo bondia wa ndondo baada ya wiki atamtafuta chiz mwenzake wapigane utasikia nilitafunwa na Mbuzi Mara sho sho watu kulazimisha mwakinyo apambane na Hao watu wao wa morogoro ni kutaka wapate Jina kwa mgongo wa mtu
 
Jana Azam TV na promoter walio dhamin mapambano sikuona kama walitaka kukuza Mchezo wa ngum na kuuendeleza Bali kuuharibu kabisa

Mapambano ya Jana Hasa lile la Mwisho la Mfaume Mfaume kila mtu kuanzia walio kua ndan ya ukumbi nje ya ukumbi mpaka Azam wenyewe walishangaa how Mfaume Mfaume Ameshinda kwa jinsi alivyo pigwa?

Tanzania Roho mbaya tu ndio inatusumbua Baadh ya wadhamin wanataka kulazimisha kila mtu awe Bingwa ili tu waweze kupata mapambano Sawa ni vizur basi tafuten mabingwa wa kweli Sasa kwa uozo kama ule anatoka mbele eti namtaka Mwakinyo Mwakinyo si atamuua?

Pambano ya Jana kidogo unaweza Sema alie stail kuitwa Bingwa ni Dulla Mbabe japo Ana tatizo la kuachia Sana ngum, za sura zimfikie sababu hil ni mbaya mana kama Bondia Ana pumz akikaza mpaka raund ya mwisho basi Dulla mbabe atakua kapigwa kwa point na Ndio mana Twaha kiduku Alimshinda.

Ila naamin Twaha kiduku Akirudia na Dula mbabe Ameisha na kama kwel Anaona yeye ni Bingwa na Anastail kupigana na Mwakinyo basi na Yeye akubali Kurudia pambano kwanza na Dulla mbabe aone kama atatoboa

Mapambano ya Jana Yameshusha hadh na Heshima ya Ngum za Sasa Ambazo Mwakinyo kapambana mpaka kufanya mchezo wa ngum uwe na uwezo wa kuingiza watu Zaid ya maelf kwa usiku mmoja embu mpeni mwakinyo Heshima yake msitake kila mtu awe bingwa ubingwa acha autafute mwenyewe msiwabebe

Pia wachambuz wa Jana na wao walikua mashabiki wa mabondia wa tanzania sijui kama ndio sheria ilivyo ama laa Lakin Jana ilikua kituko na ilionyesha dhahir kua Baadhi ya Mabondia wengi hawampend Mwakinyo kwa kuangalia mwakinyo akiwa anapambana wanavyo chambua mchezo na mabondia wengine wakiwa wanapambana Mara nyingi akiwa mwakinyo Hua wanaponda Aina ya upiganaj wake ila wakiwa Hawa Mabondia uchwara Sasa utasikia Leo anaua mpinzani hafikish raund ya Tatu Mara mpige mbavu ya kulia tumbon ehe ehe shame on you Tanzania

Sasa kama Jana Yale Makelele yote ya mchambuz juu ya mpinzani kushambuliwa na mchambuz jua anakipaza saut plas mashabiki mpinzani unafikir atakua huru kurusha ngum au ndio kumtoa mchezon kisaikolojia?

Azam TV na promoter wengine kama kwel mnataka watu waendelee kuangalia Ngum tanzania Bado mwakinyo ananafas ya kufanya ivyo ila mkitaka mlazimishe Hawa Mabondia VITAMBI wenu mlio wapa ubingwa kwa kupigana wao kwa wao zitarud zama za kina cheka promota tbc na eatv kiingilio Buku na bado watu Mia hawafiki

Azam na promoter mnatakiwa mjisafishe juu ya aibu ya Jana either kwa kuwafukuza wale majaj au kuwasimamisha

Pia mpeni mwakinyo pambano aje haraka kulinda Iman na heshima ya ngum ilio kua tayar ipo kabla haijapotea najua anataka hela nyingi ila mkumbuke yeye ndie star wa mchezo
UnaZi
 
Back
Top Bottom