Mke wake alianza kubadilika tabia akanifuata na kuniomba ushauri,nikamuuliza kulikoni? akasema ni mara ya pili sasa mkewe anambwagia mtoto na kwenda misele isiyo na kichwa wala miguu,akimwambia aondoke na mtoto mwanamke anakuwa kiburi,anakaidi na kuondoka akimwacha mtoto analia,tena ndo first born huyo mtoto,jamaa akaamua kufuatilia ili ajue kulikoni,amefanya u spy kwa miezi 6.
Jana tena mwanamke akaondoka kama kawaida yake na kumuacha mtoto akilia,jamaa akanipigia cm kuwa niende haraka kumpa kampani ya kumfuatilia wife wake,ilikuwa saa 3 usiku,kwa kawaida mke wa jamaa huaga kuwa anakwenda kwenye hisa(michezo wachezayo wanawake wengi mjini) tulipofika kwenye ile nyumba ambayo ndo mara nyingi hupenda kwenda ktk hisa,tukakuta hayupo,jasusi wa jamaa aliyemuweka kwa kazi ya kum spy.
Mkewe,akatuelekeza aliko shem,jamaa akashindwa ku drive,ikabidi nishike sterling,looh kufika tukavamia nyumba ya mgoni na kumkuta shem yupo uchi kama alivyozaliwa,jamaa kazirai,nimekesha hosp,shem kakimbia sijui aliko,SITAKI KUOA.