Ben mwanachadema alitekwa 2016 na kupotea hadi leo hii hawa kina TumainiEl wakafurahia.Asante sana.
Mimi ninawaambia watu hapa JF wapimeni watu kwa kauli zao na msizisahau.
Huyu jamaa TumainiEL ni moja ya watu walioonyesha kwa uwazi kabisa wanaombea mabaya yamfike Ben.
Umesema vyema, waliomtuma pengine hawapo tena. Hafahamu miaka michache tu imepita alishiriki kwenye uovu uliomtokea Ben. Iwe alifanya hivi kwa ushabiki tu au kwakufahamu.
Sifa kuu ya watu wanamna hii ni kubadilika badilika kama kinyonga.
Mwaka 2017 Nape katolewa bastola hadharani pengine leo hii angekuwa kauwawa kama yule mtu asingezuiliwa ajabu polisi wakamkana yule sio askari na wala sio kutoka chombo chochote cha usalama?
Lakini teknolojia ikawaumbua yule alikuwa ni miongoni mwa walinzi wa Makonda.
Mwaka 2018 Mo Dewji mbunge wa zamani na mwanaccm akatekwa na kurudishwa akiwa hoi.
Watekaji watashangilia upande kwakuwa sio wao ila ikiwafika ndio wanajua leo hakuna aliye salama.