Kwa yanayoendelea nchini je, Watanzania tupo salama?

Ben mwanachadema alitekwa 2016 na kupotea hadi leo hii hawa kina TumainiEl wakafurahia.

Mwaka 2017 Nape katolewa bastola hadharani pengine leo hii angekuwa kauwawa kama yule mtu asingezuiliwa ajabu polisi wakamkana yule sio askari na wala sio kutoka chombo chochote cha usalama?

Lakini teknolojia ikawaumbua yule alikuwa ni miongoni mwa walinzi wa Makonda.

Mwaka 2018 Mo Dewji mbunge wa zamani na mwanaccm akatekwa na kurudishwa akiwa hoi.

Watekaji watashangilia upande kwakuwa sio wao ila ikiwafika ndio wanajua leo hakuna aliye salama.
 
Tunaweza kusema hatuko salama lakini kuna makundi hayako salama zaidi

1. Wakosoaji wa serikali
2. Wanaofichua uovu wa serikali
3. Wafanyabiashara wasiokuwa chawa
Haya ndiyo makundi ambayo yapo kwenye hatari zaidi
Lakini sisi wananchi wa vijijini hatujafikiwa bado na mkono wa magaidi na watekaji.
 
2017 : Ulisomea wapi kuwa waziri anaenguliwa nafasi yake halafu anaitisha PRESS CONFERENCE pasi na kuwaambia wakubwa zake na kumpa ruhusa....

Ujinga huo....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
2017 : Ulisomea wapi kuwa waziri anaenguliwa nafasi yake halafu anaitisha PRESS CONFERENCE pasi na kuwaambia wakubwa zake na kumpa ruhusa....
Kwahiyo wewe unaunga mkono matishio ya silaha hadharani kwa wenye ruksa kutumia silaha kutoka vyombo vya usalama?
Ujinga huo....
Ujinga wa nani Nape au Kisanduku aliyechomoa bastola hadharani kama mwehu?

Kwani mafunzoni huko hawakufundishwa somo la emotion intelligence?

Kila mtu akianza kuchomoa silaha hovyo hovyo mtaishi kwa amani?

Ndio maana nilitoa pendekezo kuwepo na periodic mental health screening and psychotherapy kwa askari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…