Naomba kujua hili kisheria because nimeachishwa kazi sasa nahitaji kudai fidia zangu kupitia mahakama. Nilipoenda kwenye chama cha wafanyakazi ili kuanza process za kufungua mashtaka nilihitaji kudai muda wangu wa ziada sababu tangu nianze kazi huwa nafanya masaa 48 kwa week badala ya 45.
Sasa katibu wa chama ananipa tarifa kwamba overtime huwa inaisha ndani ya siku 60. Kisheria nahitaji kujua hilo? Pia kupatiwa usafiri, mimi binafsi nilikuwa natumia usafiri kwa gharama zangu ila sikuwahi kuhoji, je nina haki ya kudai fidia ya gharama zangu za usiku? Naomba kufahamu hilo!
Shukrani mkuu