Hakuna aliye mkamilifu duniani zari alimwacha mumewe akakimbilia kwa Dai akidhani huko ndio kuna nafuu lazima tuelewe kila binadamu ana mapungufu ingawa yanatofautiana jifunze kutorudia kosa.
Kila mtenda hutendwa hili liko wazi ona Ivan alivyotendwa na kuumia alipoachwa na Zari leo zamu ya Zari kuumia tena ameumizwa zaidi maana amezalishwa na bado amebwagwa.
Hii haimpi Dai unafuu wowote lazima naye atatendwa na atadhalilishwa na kupelekwa mahakamani na guilty haitaisha moyoni mwake.
Matumizi ya mtandao, hili limekuwa janga sasa mtandaoni sio mahali pa kuanika mapungufu ya ndoa/mahusiano yako na sio mahali pa kuwaringishia watu kiben10 chako.
Usitupie picha zako mapenzi watu waone unapendwa na unapigwa denda vizuri fikiria zile picha za Dai na Zari za kushikana shikana leo zina thamani gani kwao yale matambo kwa snap-chat leo yanageuka kukuzomea.
Wadau toeni mafunzo hapa ili mambo yasiharibike kwa wengine bali wajifunze.
Acha uwongo wewe!.
Zari alidate na watu wengine baada ya kuachanana Ivan. Hakutoka kwa Ivan ili akimbilie kwe Dai. Huu ni uwongo nambari moja.
Uwongo mwingine ni kusema Zari kaachwa wakati Zari ndiye amemuacha Dai. Acheni kujifariji. Juzi Dai akiwa Kigali alisema ana mpenzi mmoja Zari, na kwamba anampenda sana.
Kupendwa na kupenda hadharani ni satisfaction ya wakati huko kulingana na emotional requirements na si akiba kwa kesho. You need to show love to your love one. Stop finding excuses for not being romantic!. Eti nikiwa romantic kesho nikiachana nitasemwa!. Wapiii?????? How do you know tomorrow, utakuwa na hizo hisia kali ulizonazo leo za mapenzi?
Bado Zari is a Hero kwa sababu ameweka bayana hawezi ku compromise dignity yake, kwa kuishi na mwanamme kahaba asiyechagua ili mradi sketi tu.
Somo nikwamba wanaume wa kiswahili tunatia aibu. Tuache kujidhalilisha, tuwapende wandani wetu badala ya kuruka ruka bila mapngo na kuishia kuzaa watoto kama kuku wa kienyeji. Kutembea na wanawake kibao bila mpango si ushujaa wala ulijari bali ni ukahaba unaodhalilisha familia na vizazi vijavyo!.
Diamondi ambe Mungu ampe maisha marefu. Kinyume ch a hapo damu anazochanganya hizo, mke atakayeoa awe tayari kulea watoto wa kambo kutoka mama watatu ama zaidi na damu tofauti, na viasili tofauti na haiba tofauti. Mfano Zari, hata neno, yeye tayari anawatoto wake na anaweza kuwatunza bila shida. Kuna mabeta, naye anazaa watoto akitegemwa mke wa dai atawalea. Kuna huyu wa juzi, naye anategemea azae mke wa dai alee, kuna weme naye anategemea azaa, mke wa dai alee, bado kuna wa rwanda naye anategemea azeo mke wa dai alee. kuna wa big bro naye anategemea azao mke wa dai alee!. Huyo mke mwenye kulea timu ya mpira kutoka kwa wanawake wa nje, hayupo kasoro Zari tu!.
Zari alimpenda dai kwa mapenzi yakweli. Hivyo vikahaba vingine vinahitaji fedha na fame tu!. Hakuna kitu, hakuna hekima, hakuna uaminifu, hakkuna uvumilivu.
Dai kachezea shilingi chooni ambayo ataijutia!. Hakuna mwanamke kama Zari kati ya hao wote anaotangatanga nao!. Na mwisho wa Dai bila kurekebisha tabia, utaishia kwenye level ya uswahili uswahili tu!.
Kwa kwlei inasikitisha sana, Dai kukosa akili kiasi cha kupoteza lulu kwa ajili ya mimalayA. Inasikitisha mjuu wangu. Lakini Mungu ni Mkubwa. Tumwachie Yeye.