Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Kitabu cha Torati kinachosomwa na dini kuu 3 duniani yaani Uislamu, Ukristo na Uyahudi kina hadithi ya kusisimua sana kuhusu nabii mmoja wa kale aliyeitwa Mussa.
Hadithi ya maisha ya Mussa inafundisha kuhusu jambo moja kuu nalo ni HAKI. Hii ni kwa sababu, Mungu alitaka kuwatoa waisrael utumwani nchini Misri walipokuwa wanaishi bila kupata HAKI zao za msingi na kutendewa HAKI.
Hadithi ya Nabii Mussa ndiyo msingi wa dini kuu tatu za duniani (Uislamu, Ukristo na Uyahudi) kuamini katika HAKI (Social Justice) kama msingi mkuu wa maisha ya binadamu na moja ya takwa la Mungu kwa binadamu. Hadithi hii inasimika hoja kuu kuwa Mungu anapenda HAKI na hapendi watu kuonewa na kunyanyaswa.
Kwa miaka mingi nchini Tanzania, amani umekuwa wimbo unaohubiriwa kila siku na Wanasiasa. Wanasiasa wanaojineemesha kwa ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka walijikita kuhubiri amani huku wakiitumia vibaya kuwafanya Wananchi kuwa wajinga kiasi kwamba hawawezi kudai haki zao.
Baada ya Wananchi kuchoshwa na uongo wa Wanasiasa na kuamua kuchukua maamuzi, mwaka 2025 utakumbukwa kuwa mwaka ambao HAKI ilisimikwa rasmi kama hitaji kuu la Watanzania katika maisha yao.
Mwaka 2025 utakumbukwa kama mwaka ambao kwa mara ya kwanza nchini Tanzania alipatikana mtetezi wa kweli wa HAKI Bwana Tundu Lissu ambaye watawala walishindwa kumuhonga hadi kufikia kumfunga jela kwa nguvu bila hukumu ya Mahakama.
Mwaka 2025 utakumbukwa daima kuwa mwaka ambao Watanzania waliamka rasmi na kukataa chaguzi za kiini macho hadi kufikia kuingia barabarani na kukataa uchaguzi ulionajisiwa na Watawala ili kujisimika madarakani.
Mwaka 2025 utakumbukwa pia kama mwaka ambao vyombo vya ulinzi na usalama hasa Polisi, JWTZ na TISS vilikubali kutumiwa na kikundi kidogo cha wanasiasa kuhujumu matakwa ya Wananchi wanaodai HAKI hadi kufikia kuwasaliti Wananchi, kuwaua na kuwafikia kwenye makabuli ya halaiki bila kuwapa heshima ndugu zao kuwaaga wapendwa wao.
Mwisho mwaka 2025 umetufundisha kuwa HAKI lazima ipiganiwe na bila kupiganiwa haiwezi kupatikana kamwe.
Tunahitaji msaada wa Mungu katika hili na hatupaswi kukata tamaa.
Tanzania bila utekaji, kesi za kupambikiwa, mauaji ya wananchi wanaodai haki inawezekana kabisa.
Tusiache kuipigania Tanzania yenye HAKI.