Peter Madukwa
JF-Expert Member
- Sep 20, 2012
- 3,147
- 2,513
Kwaheri Rais Magufuli, ndiyo lugha pekee iliyobaki tunayoweza kuitumia kwa sasa kwa kuwa hakuna namna ambayo tunaweza kuifanya kurudisha uhai wa mpendwa wetu, tumwombee apumzike kwa amani roho yake ilazwe mahali pema peponi, Amen.
Mimi binafsi pamoja na mapungufu ya kibinadamu bado ninaamini kuwa RAIS Magufuli alikuwa kiongozi shupavu ambaye alikuwa na ujasiri wa kipekee wa kufanya maamuzi.
sifa kuu ya kiongozi inaanza ña uwezo wake wa kufanya maamuzi kwa kuwa ktk kufanya maamuzi si wote wanaoweza kupendezwa kwa hiyo inahitaji moyo na busara ya kipekee na kujitoa mhanga ktk kufanya maamuzi kwa maslahi ya taasisi au taifa.
Rais Magufuli alibarikiwa uwezo huu, hakutaka nchi ishikwe mkononi na watu binafsi wanaojiita Matajiri au wafanyabiashara au kikundi fulani cha wanasiasa.
hakutaka watu fulani wajione bora kuliko wengine maana kuna watu ktk kipindi kirefu walidhani wao wameiweka serikali mfukoni, lakini Magufuli hakutaka jambo hilo litokee ktk utawala wake, huu ni ujasiri uliowashinda wengi.
Rais Magufuli alikuwa na ujasiri wa kutumbua viongozi wazembe bila kujali wao ni nani ktk chama hata nje ya chama, kwa mfano alimtumbua hata Rafiki yake wa karibu Mh Charles Kitwanga kwa kosa la kuingia bungeni akiwa amelewa. Uamuzi huu ulikuwa wa kipekee ambao ulifanya watu waone kweli Rais Magufuli hana utani ktk utawala wake
Ujasiri wa Magufuli ulikuwa sawa na ule wa Rais wa kwanza Hayati JK NYERERE ambaye hakutaka serikali yake iwekwe mfukoni
Kimsingi, Rais Magufuli alikuwa na nia ya dhati kabisa ya kuibadilisha Tanzania na ndiyo maana alianzisha miradi mikubwa kwa manufaa ya baadaye (kiongozi wa maslahi binafsi hawezi kuanzisha miradi mikubwa ya kitaifa) kwa hiyo Rais Magufuli hakuangalia maslahi yake binafsi wala kujilimbikizia mali, TUNAAMINI KUWA MAMA SAMIA SULUHU ATAENDELEZA MAZURI YOTE ALIYOYAACHA MAGUFULI NA KUKAMILISHA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO INAYOENDELEA NCHI KWA MASLAHI YA TAIFA.
Naomba nitumie fursa hii pia kumtakia kila la heri mama Samia Suluhu ktk majukumu yake mapya ya kuwa Rais wa kwanza mwanamke ktk historia ya Tanzania.
mimi binafsi ninaamini mama Samia Suluhu ni kiongozi ambaye atatuvusha kuelekea ktk nchi ya ahadi, kuwaunganisha watanzania, kudumisha demokrasi na umoja wa watanzania na kuimarisha uhusiano wa kimataifa.
tunaamini kuwa Rais Mama Samia Suluhu Hassani atawahudumia watanzania bila kujali itikadi zao za kisiasa, ukabila wala udini na kujenga taifa la kistaarabu, utu na usawa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano na sheria za nchi.
Buriani Rais John Magufuli na kila la heri Mama Samia Suluhu Hassani ktk kipindi hiki kigumu cha kuondokewa ghafla na kiongozi wetu wa nchi
Mungu ibariki Tanzania iendelee kuwa nchi ya amani, umoja, haki na upendo