Kwaheri TTCL, kila lenye mwanzo halikosi mwisho

Alikuwa anafanya nini huko ughaibuni?
JPM alimleta yule jamaa kutoka ughaibuni asimamie TTCL akawa apigana kwelikweli.

Baada ya JPM kufariki yule jamaa akaondolewa hapo na nadhani amepewa nafasi ya kisiasa ya ukatibu tarafa au kitu kingine.
 
Kwa hiyo hakuwa anajua masuala yoyote ya biashara ya mitandao ya simu??
 
JPM alimleta yule jamaa kutoka ughaibuni asimamie TTCL akawa apigana kwelikweli.

Baada ya JPM kufariki yule jamaa akaondolewa hapo na nadhani amepewa nafasi ya kisiasa ya ukatibu tarafa au kitu kingine.
Shirika lilikuwa na ufanisi gani wakati wa Jiwe kama sio kulazimisha wafanyakazi wa Serikali na Mashirika yake kutumia kinguvu line za TTCL?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli

Tangu kuanza kutoa gawio kwa Serikali mwaka 2016, Shirika hili la TTCL hapa mmetangaza faida ya Bilioni 8

Naomba niwaambie tu ukweli, TTCL mnapigwa vita kweli kweli, vingine ni vita vya chini ka chini, hata leo kulikuwa na mbinu za kunifanya nisije hapa kuzungumza na nyinyi, kuzindua mfumo nenu na kupokea gawio, lakini nikasema hapana


Waziri amesema Mfuko wa Mawasiliano upo chini ya wizara yake, pesa zinachangwa na Watanzania na TTCL ni ya Watanzania, kwa nini inakodi minara ya mashirika mengine na kulipia Sh mil. 700 hadi mil. 800. Kwa nini usitumie pesa hizo kujenga minara ukawapa TTCL moja kwa moja?


Taasisi zilizojiunga kutumia TTCL, ofisi yangu ya Rais haikutajwa, chama changu CCM hakikutajwa, inaonekana hawa wanaopinga hata kwenye ofisi yangu wamo. Kama wananisikia ninataka ndani ya mwezi mmoja tuanze kutumia simu za TTCL na wizara nyingine

Mwaka 2016 Serikali iliamua kununua 39% ya hisa zilizokuwa zikimilikiwa na Bharti Airtel kwa Bil.14 ili kuirudisha TTCL Serikalini, hii inaonyesha Serikali haikufanya makosa kwani kabla ya kuirejesha Serikalini hatukuwahi kupata gawio lolote

Ombi kubwa kwa Watanzania, ni lazima tujali vitu vyetu, nitoe ombi kwa Viongozi wa dini, licha ya kazi kubwa ya kuliombea Taifa na kutuombea kuzishika amri za Mungu basi mtuombee pia kuthamini vitu vya kwetu
 
Mkongo wa Taifa wenyewe umesha washinda.....
Miaka sijui Saba bila matokeo ya kuonekana, naona wanapotezea tu serikali mapato kwa kuto kuunganishia wahitaji ili Serikali ikusanye kodi. Dar peke yake hawajaweza kuunganishia watu wanaohitaji hata nusu, lini wataweza kufika mikoani?
 
Naona ilikuwa kazima ife
 
Inasikitisha kwakweli hili ni kweli walikuwa na unau flani sasa unashindwa kuelewa hujuma hizi zote wakuu wanashindwa kung'amua au Udo kila mtu na urefu wa kamba yake inchi inafunguliwa?
Licha ya kusikitisha tu baki yafedhehesha, yatia aibu na dhihaka.

Wale walokuwa wakitusifia pale tulipofika uchumi wa kati wakiwemo WB sidhani kama wana cha kusema.
 
Hawa jamaa waliwahi kutoa gawio kwa serikali miaka ya nyuma ?

JokaKuu zitto junior
 
Jamaa mwenyewe ndio yule Waziri Kindamba!? Kuna taasisi yoyote ambayo aliwahi kuwa CEO akaiongoza vizuri kabla ya kukabidhiwa TTCL!? Au alikuwa anaongoza kwa maelekezo ya JPM!?
Nakumbuka jpm alisema taasisi zote za serikali zitumie ttcl nazani iliisaidia kuiongezea nguvu ala nape alipoitenguwa Ili bas nikajiwa itakufa tu
 
Maadam Ccm bado ndio watawala haya mambo yataendelea tu.
 
Hawa jamaa waliwahi kutoa gawio kwa serikali miaka ya nyuma ?

JokaKuu zitto junior
JPM aliweka targets kwa kila CEO au kiongozi kwamba nakupa vifaa fanyia kazi na nataka uonyeshe uhamiri wako.

Wengi watasema alikuwa akilazimisha au nini lakini kwa mfano Kindamba alikwenda SUA na akatiliana nao saini mkataba wapate wafanyakazi watumie simu za TTCL kuna ubaya gani hizo ni different terms & conditions ambazo kilakampuni huweka.

Na kuna wakati alisema walikuwa wakilenga kati ta 7 hadi 10 bilioni kwa mwezi.

Sasa Serikali imenunua hisa zote kutoka Bharti Airtel na imekupa weye uendeshe shirika, halikadhalika ATCL wamepewa ndege mpya wazitumie kuendesha kampuni ipate faida kwa kupanua masoko na kadhalika.

Je, wataka nini tena mtu mweusi umepewa kila kitu wahanyahanya tu hujitambui warukaruka kama kinega mti huu mti ule?
 
Tatizo ni Ccm
 
yule jamaa aliuza hisa akazipeleka SA awamu ile, then karudi kivingine kawanunua wale wawili kawaunganisha.. Yule wa monduli zile hisa zake pale Voda sijui zimekaaje naye.
Hawa wavetcong inafahamika nani mdosi pale.. Wale wadosi wa kino~ Moroco inafahamika kuanzia mpokea kodi wa ule mjengo na Big banana ni nani..

TTCL ilikwapuliwa na wale jamaa wa Kino Moroco then yule jamaa wa Chato akairudisha pamoja na zile hisa pale Moroco Kino, sasa wale jamaa waKino Morroco wanataka lidude lao hapo ndio TTCL inapofia kwa muuza supu pale kino.

Kuna Uzi humu unauliza, Hii nchi ni mali ya nani?
 
SIM card tuzitupe kabisa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…