Kwaheri TTCL, kila lenye mwanzo halikosi mwisho

Mimi nilisema Starlink haiwezi kupewa ruhusa Tz watu wakawa wanabisha, same reason hawafufui mfumo wa reli ambao ungesafirisha mizigo kwa gharama nafuu sababu mabosi ndo wamiliki wa malori.
Tatizo ni mifumo.

Tanzania hakuna mifumo imara, wako tu wahuni wanajiamulia wanavyotaka kwa maslahi yao siyo kwa ajili ya taifa.

Kutengeneza mifumo iwe inadhibiti na kuwaadhibu hao hata kama ni mafia wa namna gani waadhibiwe vikali kama kule China, Cuba walifanya mageuzi na walifanikiwa, hata Tanzania inawezekana.

Kama hatutaweka mifumo imara nchi itaendelea kuwa Banana republic siku zote kwa miaka na mikaka.
Mfumo unatoa dira ya taifa, Tanzania hivi ina dira ya taifa? Au aliepita alifufua ttcl leo huyu anasema hiyo hiyo ttcl ambaye yeye alikuwa msaidizi wa aliyetoa maauzi kuifufua ttcl leo anatoa maamuzi ya kuiua.
 
Kila la heri kwenye kifo chake? Au?

Mimi naitakia Buriani. Kwa heri ya kuonana TTCL Mobile. Tulikupenda ila Menejimenti yako imekupenda zaidi
πŸ˜… kiukweli buriani kabisa, kuna siku tumekatikiwa internet asubuhi, tumewasiliana nao wamekuja kurespond saa tisa jioni. Hatuna internet hatujafanya kazi toka asubuhi, kisa sijui kulikuwa na cable cut mahali kwenye miundombinu yao, ila ndio hivyo walikuja kurekebisha jioni kabisa.

Watu wa serikali acheni uzembe bwana!
 
Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani, tutafidiwa chochote au ndio vile tena?

Tunaitakia kila la heri.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ndo maana watu kama sisi ambao twafanya tathmini katika maeneo mbalimbali kwa mimi naweza kabisa kumuelezea mama Samia wapi ashindwa katika uongozi wake.

Ndo maana nikasema tangu huko nyuma kwamba yawezekana kabisa mama ana nia njema moyoni mwake lakini huenda nafsi yamsuta au mahadisi wamganda.

Yupo mwandishi aitwa Beerel ambae ameandika kuhusu masuala ya uongozi yeye asema , uongozi ni kusaidia, kuelekeza na kusimamia mabadiliko kama ambavyo msaidizi wake alikuwa akifanya (hapa naomba tuachane na mengine tuzungumzie mazuri yake) kuhakikisha taasisi za serikali na mashirika yote yanapokea mabadiliko.

Kazi kubwa ya uongozi ni kutambua hali halisi iliyo mbele yako iwe hali ngumu ya uchumi, rushwa, ubadhilifu na wizi wa mali ya umma na kadhiai zingine.

Beerel asema kama hakuna mabadiliko basi hatuhitaji viongozi kwahiyo wajibu mkubwa wa kiongozi ni kuelezea tatizo (JPM alieleza matatizo ya nchi hii) kwa kushirikiana na wengine na yeye mama Samia akiwemo.

Hivyo tokea hapo, hali halisi yatazamwa kutokea kila kona, habari mbaya zote zakabiliwa, na mwelekeo mpya waelekezwa katika hali hiyo halisi ambayo huendelea kutokea na kukua.

Jambo jingine kubwa ambalo kiongozi au uongozi wapaswa kufanya ni kuwakomboa watu (to liberate people) kutoka katika fikra za kufikirika na kuwaweka tayari kuwataka wafuate unoyataka.

Sasa mtihani ulipo ni penye kuhakikisha hawa wanoongozwa waenda nawe na wakubalia kuhusu hali halisi na watakuwa nawe sambamba kukabiliana nayo. na kuelezea hali halisi ukawaambia unowaongoza ni ngumu kwani viongozi haohao huanza kupuuza hali halisi na kuacha kabsa kushugulika nayo.

Hali halisi ya nchi hii ni kama inojionyesha na kila mtu afahamu, hivyo mheshimiwa raisi ana kazi kubwa huko mbele hata kama akichaguliwa tena kuendelea na uraisi hiyo 2025.
 
Okay mwaka 2020 TTCL iliwahi kutoa gawio la Bil 2.1 PITIA tukisogea miaka miwili mbele tunaambiwa inajinedesha kihasara sasa hapa nadhani wangeweka tu wazi what happened mpk TTCL atoke kutoa 2.1 mpk kuonekana hasara within just 2 years
 
Licha ya kusikitisha tu baki yafedhehesha, yatia aibu na dhihaka.

Wale walokuwa wakitusifia pale tulipofika uchumi wa kati wakiwemo WB sidhani kama wana cha kusema.
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 

umezungumzia Air India kuwa na CEO kutoka New Zealand, nimeona juzi Saudia Arabia na shirika lao jipya something Riyadh Air wana CEO kutoka Australia kama sikosei..

Sasa utajiuliza kwanini kama sisi kila siku tunashindwa tusiajili CEO' s na operations managers kwenye haya mashirika kutoka ughaibuni, mfano ATCL, TPA, TTCL nk kwanini tusiajili competent people kutoka nje? sisi tukabaki watazamji tu..

Maana pamoja na issues za wizi lakini pia tunachangamoto ya Incompency na skilled labor force ambapo tunaweza kuoutsorurce na kutrain baadhi ya levels.
 
Ndio saa 100 hawwzi kufikiria vitu vigumu unamsingizia tu huyu bibi yupo tiaria kukata mkono ili kuondoa kinnyesi kulilo kufuta kinyesi kwa maji
 
Hawa CEO ni vichwa khasa na kabla hajakubali offer ya kuja TTCL wanasheria wake watataka wapitie vitabu vya TTCL kuangalia ufanisi na uendeshaji wake.

Kwa mfano huyo wa Air India kabla hajapewa hiyo kazi Air India mwaka jana walimpa offer jamaa mmoja mturuki aitwa Ilker Ayci ambae alikuwa CEO wa Turkish Arlines na akakataa kwani kukiluwa na issues za kuuzwaji wa Air India kwenda Tata na serikali ilikuwa ikitia pua lake humo huvyo jamaa akatoa nje.

Ila kama serikali yaamua kuwa makini wapo watu waitwa "headhunters" hawa ni wataalam wa kutafuta vichwa vyenye utaalam wa aina mbalimbali ila lazima serikali iwe tayari kulipa fedha nyingi na hawa kutaka kulipwa dola.

Lakini serikali imefanya mambo haya kunaile management iuloongoza TANESCO na sote twafahamu yalotokea hivyo mambo haya serikali ina watu wayafahamu uzuri tu.
 

Nazani Nia yenu Sasa imetimia,mpo umumu mliyokuwa na mipango ya kuipoteza ttcl, Ii nchi ilitakiwa watu kunyongwa afhalani. Mashilika binafsi Yana shine ya serikali yanakufa daa Tanzania miaka kumi mguu mbele mingene kumi mguu nyuma kama mlevi mpaka tufike tumechoka
 
Pasipo MAONO, taifa huangamia.
Hapo ndio kawaza mpaka mwisho yani πŸ˜πŸ˜πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜πŸ˜πŸ€”.
Shirika hilo hilo wakipewa Wachina au wageni wengine linaweza fufuka kunani Africa, kunani Tanzania?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…