Kwaheri Windows 10, The end is 14 October 2025, haya ndio mambo muhimu unayopaswa kuyajua na hatua za kuchukua

Kwaheri Windows 10, The end is 14 October 2025, haya ndio mambo muhimu unayopaswa kuyajua na hatua za kuchukua

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
A. Hakutakuwa na updates za Usalama (Security updates) – Virusi vipya na mbinu mpya za mashambulizi zitaweza kupenya kwenye mfumo wa Windows 10, ingawa antivirus kama windows defender itaendelea kupokea updates, Windows 10 kama mfumo endeshi haitaendelea kupokea updates rasmi zinazoweka viraka kwenye matundu. Hivyo wadukuzi wakigundua kuna shimo flani katika mfumo wanaweza kupenya.


B. Hakutakuwa na marekebisho ya matatizo mapya (bugs)

  • Windows bugs - Hiya ni matatizo ya mfumo wa window, mfano Pc kujizima, kuganda, au kupunguza kasi, hutoweza kutegemea masahisho, marekebisho au huduma kutoka microsoft kutatua tatizo hilo.
  • Hardware bugs - Ikiwa utapata matatizo ya vifaa kama printers unapotumia windows 10, Microsoft haitatoa msaada wa kiufundi kutatua matatizo hayo
  • Software Bugs - Ikiwa utapata matatizo katika software hasa mpya kama vile kugoma kufunguka, kuganda, kujifunga, n.k. Labda utahitaji kutafuta msaada usio rasmi kutoka kwa wadau wa wa majukwaa ya mtandaoni.

C. Hakutakuwa na features mpya kwa windows 10, wataopata feaures mpya ni wenye windows 11 na kuendelea, mfano mipangilio mipya, muonekano mpya, tak bar ya kisasa, n.k.

D. Makampuni ya software na Hardware taratibu yataanza kuisusa windows 10, watahamia rasmi kutoa nakala za software kwenye windows 11 na windows mpya zijazo

Hatua za kuchukua

Nunua pc ya kisasa iliyofikia vigezo vya windows 11 iwe na Intel Core 8th gen au mpya, 4 GB Ram, Uefi, TPM 2.0+

Ikiwa unahitaji kuendelea kutumia Windows 10, tumia Windows 10 Enterprise LTSC 2021. Itapokea updates za usalama hadi 2027, lakini haitapata updates za features mpya na ina vitu vichache ukilinganisha na matoleo mengine ya kawaida.
 
PC yangu ni Gen ya 6 core i5. RAM 8 na SSD. Itafaa kweli kuweka hiyo 11? Maana hapa ina 10 tayari.
 
PC yangu ni Gen ya 6 core i5. RAM 8 na SSD. Itafaa kweli kuweka hiyo 11? Maana hapa ina 10 tayari.
Unaweza kuweka kimagumashi na wengi wamefanya hivyo lakini ni nje ya vigezo vya kampuni, changamoto zozote zinaweza kujitokeza sababu ni window ya kufoji
 
Back
Top Bottom