Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 433
Imamu wa Msikiti wa Mtambani wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Sheikh Shaban Pembe amehoji sababu ya nguvu kubwa ambayo vyombo vya habari vya kimataifa na baadhi ya majirani wa Tanzania, hususan Kenya, wameiweka katika kuripoti matukio ya vurugu yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akitoa hotuba msikitini, Sheikh Pembe amesema katika siku za hivi karibuni vyombo vikubwa kama CNN vimerusha ripoti kuhusu matukio ya uchaguzi huo, huku BBC na vyombo kadhaa vya habari nchini Kenya vikiendelea kuripoti kwa kina kile kilichotokea, akihoji kama ni huruma ya dhati kwa Tanzania, au kama kuna “ajenda iliyojificha nyuma ya mwamvuli wa haki.”
Sheikh Pembe amesema ni muhimu Watanzania kujiuliza ni kwa nini matukio hayo yamepata umakini mkubwa wa kimataifa kuliko ilivyozoeleka.
Katika kutoa hoja yake, Sheikh Pembe pia ameeleza mtazamo wake kuhusu uhusiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya, akisema ushindani uliopo baina ya nchi hizo mbili unaweza kuwa moja ya sababu za maslahi yanayochochea namna baadhi ya vyombo vya habari au wadau wanavyochambua matukio ya uchaguzi wa Tanzania.
Amedai kuwa miaka ya nyuma bidhaa nyingi za Kenya zilikuwa zikitegemea soko la Tanzania, lakini sasa uzalishaji wa ndani umeongezeka na bidhaa nyingi zinazoingia sokoni zina nembo ya ‘Made in Tanzania’.