Kwahiyo tumewahamishia Shule nyingine Walimu waliokuwa wakichekelea kupigwa Mwanafunzi ili wakacheke zaidi huko?

Kwahiyo tumewahamishia Shule nyingine Walimu waliokuwa wakichekelea kupigwa Mwanafunzi ili wakacheke zaidi huko?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Je, hawa Walimu waliokuwa Wakichekelea Mwalimu Mkuu alipokuwa akimuadhibu Kikatili Mwanafunzi angekufa bado wangeendelea Kucheka?

Kwanini mmewahamisha Shule nyingine na siyo Kuwafukuza kabisa Kazi? Wao Wana tofauti gani na Mwalimu Mkuu aliyekuwa akimchampa huyo Mwanafunzi?

Hovyo kabisa.
 
Wakuu wanakuwaga wanoko sana wale walimu wasingeweza kumzuia. Hata hivyo walimu waliokuwa wanacheka wamefanya kosa kuepusha shari ni bora wangejiondokea ofisin,vp aliyerekod video naye bado yupo kazin?
 
mpwayungu village


Binafsi ninawashauri walimu wote nchini waachane na suala la kuchapa wala kufuatilia kwa kina watoto wa watu.

Mwalimu jikite kufundisha tu, mtoto wa mtu akizingua achana naye, hakikisha masuala yote ya kinidhamu unamwachia mzazi wake atajuana naye huko kwao, hata wakifeli wote wewe hautanyimwa mshahara.

Pia walimu tafuteni kazi nyingine binafsi za kuwawazisha zaidi ili ukose muda wa kutosha wa kumuwaza mtoto wa mwingine, ili ujiepushe na matatizo.

Mchuma janga hula na wakwao.
 
mpwayungu village


Binafsi ninawashauri walimu wote nchini waachane na suala la kuchapa wala kufuatilia kwa kina watoto wa watu...
Kuchapa kupo na kwa maisha yetu ya kiafrika kuna umuhimu wake. Lakini walimu wanapaswa kutofautisha stress za maisha yao na kazi zao.

Unakuta mwalimu ana hasira za kugombana na mkewe halafu anazipeleka kazini. Athari yake ndio ile kupiga mtoto wa mtu kama unapiga mwizi.

Kuna upigaji wa mtoto ambao atahisi kabisa kuwa kaadhibiwa bila kuleta athari yeyote.

Kubwa na muhimu kabisa kuna haja ya watu kuacha kuchukulia ualimu kama chaka la ajira. Ualimu ni kama unesi ama udaktari, ni wito. Kabla ya kupenda kufundisha inapaswa uwe na upendo na watoto.

Sasa jitu linajijua kabisa halipendi watoto halafu anaenda kusomea ualimu kwa vile anataka ajira ya haraka. Hapo unatarajia nini zaidi ya unyama.

Mwisho wa yote namsifu mno mzazi wa yule kijana. Ingetokea kwa mwanangu nina yakini pasi na shaka huyo mwalimu angekuwa anafaya shopping ya wheel chair na magongo saa hizi.
 
Sasa hili likitokea hapa ni wazi upo katika taaluma sio.
Ikiwa una deal na watoto wenye background tofauti unapaswa uwe na uwezo mkubwa wa kutochukulia vitu kiubinafsi. Hapo ndipo niliposema mwalimu anapaswa ajue kutofautisha hisia zake binafsi na taaluma yake.

All in all una point ya maana zaidi, kuepuka yote ni bora mambo ya kuchapana yaachwe kabisa tu.
Huwa najiuliza mwalimu usipochapa anapungukiwa nini?, hapo ndipo ninapowashauri walimu waache kuchapa hakika wataishi vema.

Ninajua kuacha kabisa kuchapa kwa shule zetu hizi kuna athari lakini ni bora kuliko wewe mwalimu kujikuta uko mikonini mwa vyombo vya dola huku ukivuta pumzi ya moto au ukiwindwa na wazazi wa watoto mithili ya pakashume mitaani.

KILA MMOJA ASHINDE MECHI ZAKE
 
Huwa najiuliza mwalimu usipochapa anapungukiwa nini?, hapo ndipo ninapowashauri walimu waache kuchapa hakika wataishi vema...
Mbali ya uhitaji wa kuchapa sababu ya uhalisia wa malezi yetu, wengi wa walimu wana maisha ya dhiki mno. Kama tujuavyo penye dhiki huwa hakuna amani ya nafsi wala maisha kupelekea kujijengea hisia ya kuwa wewe ni duni/dhaifu (inferiority complex).

Ili kujipa thamani kidogo, kimbilio pekee ni kukabiliana na wale walio dhaifu zaidi yako kupelekea kutumia kiboko hata pasipohitaji kiboko.

Kwa walimu wengi kuchapa wanafunzi ni kama therapy kwao, kujipa validation kuwa hata wao wana uwezo wa kufanya jambo lenye impact (katika hili uoga na kilio cha mwanafunzi kinamuaminisha kuwa hata yeye anaogopeka, baada ya kutukanwa na muuza duka anaemdai na kudharauliwa na mkewe nyumbani).

Mpaka mtu mzima aweze kututumua misuli kupiga mtoto ambae hawezi kujibu mashambulio elewa kuna walakini wa kisaikolojia kwa huyo mpigaji.

Mbali ya kusitisha kupiga, kuna haja walimu wakaangaliwa upya kimaslahi, kwa sasa taaluma inayodharauliwa kuliko zote hapa nchini ni ualimu.
 
Katika kupitia pitia nyuzi mbalimbali kuhusu sakata hili sijaona aliyetoa sababu za kitaalam za kwanini ni hatari kumchapa mtoto kwwnye nyayo ni hatari kuliko mkononi na matakoni. Na kwanini imfanye mwalimu afukuzwe kazi kwa jambo hilo. Si kama naunga mkono jambo lile hapana. Nahitaji sababu za kitaalam tu. Povu ruksa.
 
Katika kupitia pitia nyuzi mbalimbali kuhusu sakata hili sijaona aliyetoa sababu za kitaalam za kwanini ni hatari kumchapa mtoto kwwnye nyayo ni hatari kuliko mkononi na matakoni. Na kwanini imfanye mwalimu afukuzwe kazi kwa jambo hilo. Si kama naunga mkono jambo lile hapana. Nahitaji sababu za kitaalam tu. Povu ruksa.
Nazungumzia upigaji wa kwenye nyayo, hebu jaribu kufanya utafiti wako mwenyewe tafuta kijana mwenye nguvu akupige halafu ulete mrejesho hapa.
 
Watanzia acheni unafki.. mbon hamuwasem Askari wavyo chapa watuhumiwa vituon wakiwa wanapeleleza kesi... ?
Yule kachapia fimbo pale askari anatumia nondo tena kukukandamiza ukubali kosa na ikitokea umeshinda kesi unaenda jiuguza nyumban kwenu...
 
  • Thanks
Reactions: K11
Ilitosha mwalimu kushushwa tu cheo kumfukuza wanamwonea. Nia ya mwalimu ilikuwa kumrekebisha mwanafunzi na sio kumuumiza. Hata mm hizo fimbo nlichapwa sana tu. Mbona mabinti wanachapwa mikonononi ambako ni lain kuliko mguini bado hamjasema kitu.
Watu tumepigwa hadi luler za vichwa tena zile za kuchorea ubaoni. Mm sioni kosa la mwalimu hapo hata waliokua wanacheka hawana kosa mwenye kosa ni aliyerekodi video
 
  • Thanks
Reactions: K11
mpwayungu village hili suala linakuhusu inabidi tusikie maoni yako juu ya hili kwa sababu wewe unaexperience juu ya walimu hivyo hata kwenye adhabu wanazostahili kupewa walimu huenda unafahamu zaidi😂😂😂
 
  • Thanks
Reactions: K11
Kwa kucheka kwao wametenda kosa gani?
Chukua mfano huu...

Mwanao anapigwa na mwenzake ngumi za uso na vichwa alafu mkeo anacheka na kushangilia!.

Haya toa jibu kitakachofuata...
 
Walimu hawajui matumizi sahihi ya Smart Phones ( Simu Janja) wao wenyewe wanaharibiana , kila kitu ni kurekodi tu .
Simu Janja pia ni adui mkubwa sana pale inapotumika kinyume na matumizi.
Pia Walimu acheni makasiriko ya namna hiyo kwani zama zimebadilika sasa Matumizi ya nguvu hayana tena nafasi yake.
Sio Kwa kuchapa kule
Video inaonesha mwalimu kabeba Mafimbo makubwa means ni Mwalimu wa kuchapa chapa watoto.
Imekula kwako.
 
Ilitosha mwalimu kushushwa tu cheo kumfukuza wanamwonea. Nia ya mwalimu ilikuwa kumrekebisha mwanafunzi na sio kumuumiza. Hata mm hizo fimbo nlichapwa sana tu. Mbona mabinti wanachapwa mikonononi ambako ni lain kuliko mguini bado hamjasema kitu.
Watu tumepigwa hadi luler za vichwa tena zile za kuchorea ubaoni. Mm sioni kosa la mwalimu hapo hata waliokua wanacheka hawana kosa mwenye kosa ni aliyerekodi video
Kwa hiyo kwa sababu wewe ulipigwa basi ihalalishwe?
 
Kwa kucheka kwao wametenda kosa gani?
Kufanya ‘action’ isivyo sahihi ni kosa. Pia kufanya ‘Inaction’ isivyo sahihi ni kosa. Hao walimu wamefanya ‘In-action’ kwa kuto mkamata mwalimu mkuu na kumreport polisi wakati anafanya ule ukatili.
 
Back
Top Bottom