Huyu mtoa mada yupo sober kweli,
Watu wakutie ulemavu, hapohapo wakudhulumu Ushindi wa kura ulizopata kwa haki, unawezaje kuwa na lugha laini kwa watu wa aina hiyo unapotaka kuwashitakia kwa wananchi?
Ni rahisi kusema hivo kwasab siajabu hata selo hujawahi kufikishwa..tena kuwekwa sero kwasab ya kutetea watu baki..sio familia yako.
Lissu anawashitaki CCM kwa Makundi mbalimbali juu ya namna chaguzi zinavyoporwa, anaeleza taratibu step by step, tena kwa lugha rahisi kabisa..
Hivi unaujua uchungu na maumivu ya dhuluma wewe..
Lissu akiwa binadamu kama wewe, mwathirika wa moja kwa moja ni lazima aeleze haya madhira kwa hisia.
Kama mna sababu zenu za kutompenda Lissu muwe wazi tu.
Ok Sasa hao CCM ambao kwako ndio mafundi wa kushawishi watu, hebu waweke Fair election, halafu wao Waongee kwa upole Lissu ahutubie kwa ukali majukwaani tuone nani mshindi.