Kwako Mbunge Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) kauli hii inaweza kukosesha Ubunge

Kwako Mbunge Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) kauli hii inaweza kukosesha Ubunge

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
5,771
Reaction score
14,732
Aliyekuwa msanii wa hiphop, Mwana Fa kwenye mahojiano amesema kwamba kama sio mazishi yeye hawezi kumchangia yeyote harusi yake.

"Mimi huwa sichangi harusi ya mtu, kama ni mazishi nitachanga kwa sababu hilo halikupangwa, kifo kinakujaga tu".

Mwamba ameongea ukweli hapa!

WATU MPAKA WAFE NDIO UCHANGIE. HAYA NA WEWE USIJE KUOMBA KURA ZA WATU NAYO NI MCHANGO WA KUKUFANYA UWEPO BUNGENI UKIWA HAI.

447729225_444621958313581_3902491795804630742_n.jpg
 
NAYO NI MCHANGO WA KUKUFANYA UWEPO BUNGENI
Yuko bungeni ili akuwakilishe. Ubunge ni kazi, na bunge siyo fungate.

Na alichozungumza ni uhalisia. Fanya harusi ya kadiri ya uwezo wako, baada ya kujipanga kwa muda wako. Achana na mambo ya kutegemea michango ya watu kufanya mambo yako ya starehe.

Mnawatwisha watu mizigo!
 
Yuko bungeni ili akuwakilishe. Ubunge ni kazi, na bunge siyo fungate.

Na alichozungumza ni uhalisia. Fanya harusi ya kadiri ya uwezo wako, baada ya kujipanga kwa muda wako. Achana na mambo ya kutegemea michango ya watu kufanya mambo yako ya starehe.

Mnawatwisha watu mizigo!
UNAFAHAMU MAANA KIOO CHA JAMII UKISHAKUWA UNATAZAMWA NA WENGI KAULI BILA KUFIKIRIA INAWEZA KUKULETEA MBELENI TATIZO
 
Harusi si lazima kuchangia mjue ilo ni hiari ya mtu, simple mpe anaekupa ndo msemo wa mjini, just imagine una group la chuo ,msingi, seco alafu kila group watu 20 wanaoa na kuolewa, ujinga wa mchango wa harusi unawekewa kima, msiba hauna kima
 
Aliyekuwa msanii wa hiphop, Mwana Fa kwenye mahojiano amesema kwamba kama sio mazishi yeye hawezi kumchangia yeyote harusi yake...
Anasema hivyo kwa vile anajuwa hawezi ķurudi tena kuwa mbunge wa Muheza.

Huyu anachoweza ni miziki ya kufokafoka tu lakini kupanga mawazo yenye tija hawezi kabisa.

Matakataka aliyotuachia Mwendazake haya. Akaacha watu wazuri wenye uwezo akina Adadi Rajab
 
"Kadi za harusi kuchanga changa, Kanyaga!
Wakati mwenyewe nina majanga, Kanyaga!
Sina godoro sina kitanda
Ati nikuchangie kodi kwenda kupanga (yii)" Diamond Platnumz
 
Ameeleza vyema sana kwamba harusi siyo jambo la glafla bali ni la kupanga ,sasa kama umelipanga basi jiandae wewe mwenyewe.

Kauli aliyoitoa ni ya kigreat thinker haina connection na wapiga kula ,amesema issue za ugonjwa ,misiba atakchangia fasta.
 
Back
Top Bottom