Kwako Rais Samia, fupa la ukwepaji Kodi Kwa wafanyabiashara wape wanunuaji wamalizane nalo lakini Serikali iwahamasishe kwa gawio katika manunuzi

Watanzania watahamasika kulipa kodi sio kwa elimu tu bali pia waone pesa yao ya kodi haichezewi na wanaotajwa kufuja wanafungwa na kutaifishwa mali zao, haiwezekani Mkuu wa Ngorongoro hifadhi anakaa hotel ya milioni 3 kwa siku mpaka zinafika 200 milioni anaishia kuondolewa tu, mara mifumo ya kodi inachepushwa halmashauri
 
Tumelipa kodi sana tu na bado tunalipa zile ambazo hatuwezi zikwepa lakini matumizi yake hayaeleweki. sasa unataka tudai haki lini. soma comment za watu wengi kwanini hawaoni shida kukwepa kodi. Lawama ni kwamba zinaishia kuwanufaisha wachache. hata serikali ifanye vipi, raia wanaona kodi wanayolipa inawanufaisha wachache hivyo siwezi kuwa na uchungu mfanyabiashara akiibia serikali hata kidogo.
 
Kabla ya huo muswaada wa Salma mama Maria Nyerere alikuwa anaishije? Hela ya chumvi alikuwa anaipata wapi??
 
Umesikiliza na upande wa pili au Yale maneno ya yule Diwani ndio ushahidi pekee ulionao? Kama unahukumu Kwa maneno ya upande mmoja, je huoni unakiuka principle of natural justice?
 
Kwa hasira ambayo nchi hii inapata, Rais aanze na miji mikubwa aanze na Dar, Mwanza, Arusha, Dodoma, Tanga, Mbeya, Tanga, Morogoro, Moshi n.k. TRA iaajiri au isambaze watu wa usalama wao. Hao watu wawepo kufuatilia wanunuzi wavae nguo za hadhi ya chini sana. Wafuatilie wanunuzi, wote mnunuzi na muuzaji ni ndani, mwenye biashara afilisiwe uone ndan8 ya miezi 3. Rais asicheke na hawa watu.
 
K
Kukwepa Kodi ni uhalifu kama uhalifu mwingine uwe umefanywa na mmoja au na wengi, hivyo acha kushiriki uhalifu ukiamini wengi wanafanya nitakuwa salama. Ndio ninyi mnashirimi kwenye maandamano ya wengi, unadakwa peke yako ukipelekwa mahakamani unajitetea tulikuwa wengi sikuwa pekee yangu mbona wengine hawajakamatwa?

Mfanyabiashara anayekwepa Kodi ni mhalifu na wewe unayemsaidia mfanyabiashara kukwepa Kodi ni mshirika wa uhalifu
 
Mfumo mzuri ni ule unaoshirikisha idadi ndogo ya watu. Ukijaza usalama na watu wengine kimsingi unakaribisha ukwepaji Kodi zaidi maana mfanyabiashara atazungumza na hao watu lakini idadi ya watu ikipungua maana yake mfanyabiashara atakosa wa kuzungumza naye atazungumza na mfumo.

Kuna kipindi nilishauri Serikali itumie mfumo wa INVENTORY MANAGEMENT SYSTEM iliyofungamanishwa na Mfumo wa EFD na huo mfumo wa EFD uwekwe Bei elekezi Kwa Kila bidhaa na tukitumia hii mbinu ya kuwapa gawio wanunuaji ,hapo suala la kukwepa Kodi litakuwa historia.
 
Ndio ni uhalifu kuukabidili inabidi mkate mzizi la sivyo haijalishi itafanyika nini bado watu wataendelea kukwepa kodi kwa sababu kodi yao wanaona inatumbuliwa. Simple as that. Sasa kama mtapambana na watu abdala ya chanzo mkisistiza uzalendo wakati kodi mnaila ikishakusanywa, kamwe hamuwezi kufanikiwa.
 
Wao wenyewe wakubwa wanabiashara na wanakwepa kodi hili hawawezi kulipitisha litawaathiri sana na wao pia, usiamini wanasiasa
 
Niliwahi kuwaza juu ya jambo hili, ahsante sana Kwa bandiko lako.

CC: mwigulu88
 
Katika wafanyabiashara wanao ongoza kukwepa Kodi ni kariakoo,wafanyabiashara wa kariakoo ndio wanaosambaza bidhaa nchi nzima na nchi za jirani.Walipaji Kodi wazuri ni wauzaji wa bidhaa za rejareja wauzaji wa bidhaa za jumla wanafunga mizigo ya jumla kwenda mikoani lakini hawatoi risiti na wakitoa kama anavyosema mtoa mada inatolewa risiti ya magumashi ya kuonyesha njiani endapo atakaguliwa.Watanzania tuwe wazalendo taifa bila Kodi suala la maendeleo ni ndoto kwetu hiyo migomo isiwe kama kichaka cha kukwepa kulipa Kodi watumishi wanalipa Kodi kwenye mishahara Yao lakini husikii migomo sababu wanajua ni kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao
 
Ni vigumu watu kuhamasika kulipa kodi wanapoona zinaenda kulipa wenza wa viongozi, kuongeza mavietee, kulipana posh za safari na vikao vya wabunge, pensheni kubwa za wabunge na mambo mengine kama hayo.
Mimi ni mwalimu huku kijijini Kazuramimba, naomba hiyo posho ya 60% Kwa wenza wa viongozi, ituhusu na sie watumishi wa kawaida ambao kamba zetu za malisho ni fupi. Lakini Cha kushangaza Sheria hii imewekwa Kwa viongozi wa juu ambao kamba zao za Kula ni ndefu pasipo kifani. Na hata wakifa familia na wenza wanabaki wakiogelea kwenye bahari ya utajiri wa Kula Kwa kamba ndefu.
CC: Lucas Mwashambwa , Meneja Wa Makampuni , johnthebaptist , Crimea
 
Nakala Kwa: TRA Tanzania
 
Dkt.Mwigulu tafadhali pokea ushauri huu kwa maslahi mapana ya taifa letu. Naweza kusaidia kufanikisha jambo hili nikihitajika kufanya hivyo
 
Suala la kulipa Kodi ni lazima ndio maana zinawekwa taratibu za ukusanyaji na mara nyingine matumizi ya nguvu yanahitajika. Kigezo gani unatumia kusema hivyo?
Ukitaka watu walipe Kodi basi usifuje Kodi zao Kwa anasa...Lakini pia Kodi iwe realistic na sio kama hivi sasa umekaa siku3 hujauza ,duka linamtaji wa 20M alafu unapigiwa simu eti kuna assesment yenye madai ya 200M..Unamuuliza afisa TRA hivi hata kwa kuangalia bidhaa zilizo dukani unaona ni sahihi kunidai hiyo 200M ? Anakujibu comply na Sheria za Kodi..Kibambikiana kusiko lazima inageuka kuwa hujuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…