NAFIKIRE
JF-Expert Member
- Sep 5, 2014
- 660
- 456
Kwanza nianze kukupongeza Mheshimiwa waziri kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya kwenye wizara unayoiongoza..Hongera sana
Mheshimiwa waziri niende moja kwa moja kwenye dukuduku langu lilonisukuma kupandisha hili wazo langu hapa kwenye jukwaa letu pendwa la JF.
Mheshimiwa waziri ninajua fika moja ya jukumu mama la wizara yako ni kuwatafutia vijana ajira na mazingira bora ya kazi.
Mheshimiwa waziri nimefikiria niakona moja ya njia ya kuongeza fursa za kazi ndani ya serikali ni kupunguza umri wa kustaafu kwa hiyari utoke kwenye miaka 55 mpaka miaka 45..Mimi ninaamini wewe ukishirikiana na viongozi wengine ndani ya serikali na viongozi wakuu mnaweza mkalichata jambo hili mkaona faida zake na hasara zake kama zipo na hatimaye mkapeleka mswada bungeni kwa majadiliano zaidi.
Faida ya kunguza umri wa kustaafu kwa "HIYARI" kwa mtazamo wangu mimi ni nyingi sana.Moja ya haraka ya kupunguza umri wa kustaafu kwa hiari ni ongezeko la nafasi za ajira ndani ya serikali kwa kiwango kikubwa na vijana wengi wanaotamani kuajiriwa na serikali watapata ajira serikalini.
Faida ya pili ninayoiona kwa haraka watu watakaostaafu kwa hiari wataingiza fedha zao mtaani kwa kuanzisha biashara mbalimbali ambazo zitatoa ajira kwa vijana na watu wengine na hivyo kufanya mzunguko wa fedha kwenye jamii kuwa mkubwa.
Pia kuingia kwa vijana wengi ndani ya serikali kwa kiwango kikubwa wenye uzoefu mbalimbali kutaongeza ufanisi wa kazi kwa kiasi kikubwa.
Nawasilisha