Kwako Tundu Lissu kuhusu suala la Lugha

Yaani nimegundua kuna tatizo kubwa la ufahamu kwa wanambogamboga wote. Haiwezekani mtu kaongea kwa lugha nyepesi,tena kiswahili kitupu,halafu wao wameelewa vinginevyo.
Kuna kipindi cha awamu hii nilidhani ni propaganda,nikaja gundua kumbe si propaganda,ila ni ukilaza wa wanambogamboga ndio tatizo.
 
Ndio maana Rungwe kaja na Sera ya Ubwabwa....Lishe!
Ukiona mtu Ni mzito kuelewa kagua makuzi yake hususan Lishe....!
Lishe duni inasababisha udumavu!
 
Wewe unaamini wakoloni walikuwa wanajadiliana na waafrika au walikuwa wanafanya yao tu bila kuzungumza na wenyeji kama ufanyavyo na kuku wako?
Kwa kihoja chako tu hiki inaonekana huijui historia kwahiyo siwezi poteza nguvu zangu kumuelewesha mtu ambae hajui na anajifanya anajua.
 
Kwa kihoja chako tu hiki inaonekana huijui historia kwahiyo siwezi poteza nguvu zangu kumuelewesha mtu ambae hajui na anajifanya anajua.
Swali kingongo hilo lina kila kitu utakacho embu jibu basi.
 
Wabongo wengi hawajui English huko maofisini hata memo ya kiingilishi hawawezi andika, tena wenye masters hawajui, kweli hawajui English.
 
Maneno mingii wakati watoto wako unawasomesha FM academia..!!

Mimi mwanangu namfundisha kichina..Kingeleza...kifaransa na kiswahili ni lugha yake ya 4.

Msidanganye watu, mnaua uchumi wenyewe afu mnataka watoto wetu wajifunze lugha ambayo itawatesa kwemye soko la ajira la kimataifa siyo!!
 
Wachina Hawajui kiingereza na wanawasiliana na mataifa yote duniani ikiwemo Tanzania
Kwani Lisu amesema anapenda kingereza au amesema tuamue lugha ya kufundishia? Alikuwa wazi kuwa hiki kingeresa watu wanakariri tu hawaelewi
 
Lisu mwenyewe hana kiingereza kizuri maneno mengi tu hana lolote.
 
Hoja za ccm kulazimisha kiswahili zinakera sana....hao wote baraza LA mawaziri na viongozi wetu waanamizi walisoma vizuri shule za mkoloni kingereza na hiki kitu kimewapa ufanisi mkubwa ktk kazi zao embu wafikirie
Mwl Jk nyerere
Mkapa
Kikwete
Asha rose migiro
Mama Tibaijuka
Membe
Kabudi,Lisu na wengine....
Sasa Pima welendi na ufanisi wao ktk majukumu mbalimbali ya kitaifa na ki mataifa....
Nawashangaaga sana nyie watu dizaini yako kwa hiyo unataka taifa lote na watoto wetu wawe na English ya level ya Cosmas Cheka?
 
English language is an important to reaching on top Tz I agree with lisu ✌✅
 
Wakija Tz wanajifunza Kiswahili wakienda Uingereza wanajifunza kiingereza, nk
Hata watanzania wakienda uingereza wanajifunza kiingereza, na wakienda China wanajifunza kichina. Au hujui Hilo unadhani watanzania wakienda China wanawafundisha wachina kiswahili?
 
Chadema wao ndo wakaitwa nyumbu, Lissu akisema lolote Basi wanadakia na kuanza kumsifia.
Wakoloni walikuja hawajui lugha yoyote ila walitutawala , walisaini mikataba nakuendesha serikali. Waliwezaje wakati hawakujua lugha zetu?
 

..Nadhani hukumuelewa vizuri Tundu Lissu.

..Nenda kamsikilize tena hoja zake.

..mimi nilimsikiliza mpaka aliposema tunapaswa kuamua kufundisha Kiingereza, au Kiswahili.

..lakini akaweka angalizo kuwa; Je, tunao uwezo wa kuwekeza ktk kufundisha kwa Kiingereza toka msingi, na haswa tukizingatia wingi wa shule zetu?

..kwa hiyo mpaka hapo utaona kwamba Tundu Lissu mtizamo wake ni kwamba tunapaswa kufundisha kwa Kiswahili.
 
Sio wote wanakuja.Mfano china ni Wauzaji wakubwa wa bidhaa nje ya nchi ikiwemo Tanzania na hawajawahi toka nje ya China na hawajui kiingereza
Wachina wakati tunapata uhuru si tulikuwa nao dunia ya 3? Sasa wapo wapi? Kwa hoja yako wao wameendelea kwasababu wanatumia lugha yao na sisi tupo hapa tulipo kwasababu ya Kiingereza?
 

Nimefurahi kuna mtu mwingine anajivunia lugha ya Kiswahili lakini kwakweli lugha yetu inadidimia.

Kitu kinachonichefua zaidi ni kuwasikiliza "waandishi wa habari" na "wasanii" wakiharibu lugha yetu. Kwa mfano utamsikia "mwandishi wa habari" akitumia Kiswahili kibovu kama WEWE KAMA WEWE au kutotamka maneno kwa ufasaha kama KALIBU badala ya KARIBU, HABALI badala ya HABARI n.k.

Kingine ni kuwasikiliza majuha wengine wakipenda kuchanganya maneno ya Kiswahili na Kiingereza. Unasikia mtu badala ya kusema MAMBO SAFI/POA anasema MAMBO FRESH.

Wizara ya utamaduni na baraza la Kiswahili pia wavivu na hakuna wanachokifanya.
 
Ni muhimu watu wakajua lugha ya kiingereza inatuwezesha kujifunza na kuwasiliana na mataifa mengine.
Punguza ushamba na ujinga wewe...lugha yako yenyewe inaweza kua mali duniani,hukui kua wachina,wakorea na wengineo wengi tu hawasamini kingereza na maisha yanakwenda? Mkoloni ni mshenzi sana kawafanya watu muwe na akili finyu
 
Waulize wachina kwanini walibadili mtindo wa lugha yao walipoingia kwenye uchumi wa biashara. Lissu alisema tuamue lugha moja tu ya kufundishia na hakutaja lugha gani, sijui unamzungumzia Lissu yupi. Katika haki ya kawaida kwa sasa unatakiwa uzijue lugha nyingine wezavyo endapo unataka kufanya biashara za kimataifa kwani hata hao waingereza wanajifunza kiswahili na kimatengo. Watanzania tunapenda sana kudanganyana huku wenetu mnazngumza lugha mnazotukataza kuzijua ili tubaki kuwa vibarua wenu!
 
Punguza ushamba na ujinga wewe...lugha yako yenyewe inaweza kua mali duniani,hukui kua wachina,wakorea na wengineo wengi tu hawasamini kingereza na maisha yanakwenda? Mkoloni ni mshenzi sana kawafanya watu muwe na akili finyu
Jiwe anaaibisha kwa kisukugreza chake kwa kweli lazima tufanye kitu watoto wetu wasije kuwa marais wa hovyo.
 
M
Hata watanzania wakienda uingereza wanajifunza kiingereza, na wakienda China wanajifunza kichina. Au hujui Hilo unadhani watanzania wakienda China wanawafundisha wachina kiswahili?
Mzee nawewe unatetea kilugha kibovu cha mkuu nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…