Kwako Waziri Mkuu: Suala la kuuza vyakula nje

Serikali kutangaza kununua chakula Kutoka wakulima wakati huo huo WANUNUZI Kutoka nje wakiambiwa wapate kwanza Export licence Kutoka mamlaka husika huoni kuwa ni zuio Hilo?

Usiwe unachelewa kuelewa.
 
Una akili sana bro.
Unatumia bia gani?
 
Hii nchi viongozi wetu hawana msimamo kbs... Rais na Bashe wakae wayamalize.. Ili kilimo kikue lazima bei iwe nzuri evidence yeyote ambayo imeletwa ikathibitisha kuwa baada ya chakula kuuzwa nje nchi iliingia kwenye bar la njaa au vitani... Evidences zilizopo ni kwamba chakula kikiuzwa nje kwa bei nzuri ndivyo ambavyo wakulima huhamasika kuzalisha zaidi na zaidi..
Bata Waheed..
 
Uwekwe utaratibu mzuri utakaonufaisha pande zote 2.. mtayarishaji na mlaji..
 
Serikali haifuati mambo yenu ya biblia. Usirudie tena kuandika huu ujinga wako wa kutufananisha na hao watu wa enzi za ujima.
 
Kuruhusu mahindi na mchele kuuzwa nje ya nchi hakutaongeza uzalishaji wa mazao hayo kwa sababu mbili kubwa:
1. Bado wakulima wetu wanategemea jembe la mkono
2. Kilimo chetu bado kinategemea mvua- ambayo kutokana na athari za tabia nchi/climate change-hazitabiriki (kunyesha na kiasi)
 
Serikali haifuati mambo yenu ya biblia. Usirudie tena kuandika huu ujinga wako wa kutufananisha na hao watu wa enzi za ujima.
Hahahahahaha ila inawatambua viongozi wa dini zote na inahitaji maombi yao .. maombi ya wajinga hahahaha
 
Ukiruhusu mkulima auzao kienyeji njaa itakuwa kali nchi hii maana mkulima anauza hadi mbegu kisa pesa
 
Ukiruhusu mkulima auzao kienyeji njaa itakuwa kali nchi hii maana mkulima anauza hadi mbegu kisa pesa
Upo sawa kbs kiongozi. Ndiyo maana tunashauri serikali iwe mnunuzi mkuu wa mazao ya chakula . Ili wakati wa njaa ituuzie kwa bei nafuu
 
Upo sawa kbs kiongozi. Ndiyo maana tunashauri serikali iwe mnunuzi mkuu wa mazao ya chakula . Ili wakati wa njaa ituuzie kwa bei nafuu
Hapo sawa mkuu serikali inunue .maana watu wanaandika bila kufikiri hii nchi njaa ajawahi tokea mpaka watu wakafa njaa ikitokea hilo ndo watajua umuhimu wa chakula.Unaweza ukawa na pesa chakula cha kununua hakipo.hapo ndo mtajua umuhimu wa kutouza chakula ovyo kisa pesa.Ipo siku yaja watu watafutulu maji
 
Lima heka moja tu ya mahindi Kisha tuonane mwaka kesho mwezi Kama huu utupe mlejesho
 
Kama unataka kufanya kazi ya hovyo Tanzania basi kuwa mkulima, Lima wewe kwa jembe la mkono , jembe la ng'ombe au punda ama trakta haiwahusu, mbegu ghali si kazi yao, madawa ya kuulia wadudu yako juu shauri yako, utavunaje hangaika tuu SASA unataka kuuza hawa hapa , unapangiwa umuuzie nani na kwa bei gani? Wafanyabiashara wetu kupeleka mazao nje na wafanyabiashara wa nje kuja kununua mazao hapa inaleta uwiano mzuri wa supply and demand, hivyo wakulima kupata fedha na kujiona soko lipo waongeze uzalishaji na kilimo kukua, sasa hii style ya kuzuia wafanyabiashara kupeleka mazao nje inatupeleka wapi?! Watu mlioko mamlakani tunajua mnataka tujaze matumbo tu hata tukishindwa vitu vingine vya msingi ktk maisha ili nyie mseme Taifa halina njaa muendelee kututawala, mtu haishi kwa mkate tu anahitaji pesa mfukoni. Tukilemewa na ulofa ndiyo vile hatutawaelewa kabisa, nyie mnalipana maalawansi , miposho kedekede , mishahara minono , duu mkulima sasa mnadanganya kilimo ni biashara huria siku moja ya pili mnaipiga pini kudadadeki, acheni supply n demand itawale kilimo
 
Ukiuza mazao nje utapata Pesa nyingi utanuanua trekta utalima eneo kubwa
Pili, trekta linasaidia sana kupambana na tatizo la tabia ya dunia kwa maana utaweza kumaliza kulima kwa wakati...
 
Ukiuza mazao nje utapata Pesa nyingi utanuanua trekta utalima eneo kubwa
Pili, trekta linasaidia sana kupambana na tatizo la tabia ya dunia kwa maana utaweza kumaliza kulima kwa wakati...
Tuzidi kushauri ilivyo sahihi zaidi ..
 
Tusiwafanye wakulima wa Tanzania kama misukule wetu........na wenyewe pia wanafamilia na wanatamani kuwa matajiri. Kimfaacho mtu chake.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…