Kwako Waziri mwenye sura nzuri Hussein Bashe;Benk ya Kilimanjaro cooperative Bank ibadili jina itapokelewa vyema mikoa ya kagera Mbeya Mwanza la sivyo

Kwako Waziri mwenye sura nzuri Hussein Bashe;Benk ya Kilimanjaro cooperative Bank ibadili jina itapokelewa vyema mikoa ya kagera Mbeya Mwanza la sivyo

sifi leo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
5,182
Reaction score
8,948
Nikili wazi Mimi ni mdau mkubwa wa masuala ya kiushirika, kwani ni miongoni mwa vijana tulio zaliwa na kuona kabisa jinsi ambavyo bibi zangu walivyopanga foleni kwenye maduka ya ushirika kununua unga wa njano!

Pamoja na hayo, lazima nikili yakuwa Kwa miaka takribani sita Sasa nimekuwa mdau.mkubwa wa masuala haya ya kiushirika.

Wazo langu kkwanza ni kuifufua Benki ya ushirika Kilimanjaro cooperative Benki.

Nina furah ingawa sifurah sana, kwani sijui kama Kuna jipya litafanyika zaidi ya kurudia hayo hayo au Yale yale yaliyoipelekea kudondoka.

Mwaka 2018, niliwai kutana na aliyekuwa meneja wa hii benk tukiwa tunajadiri Kwa Nini taasisi Ile ilikufa ilihali mabosi wake wapo?

Kwa maana yakuwa kama ni taasisi iliyokuwa inaundwa na Saccos pamoja na Amcos Kwa Nini ilikufa ilihali ilikuwa na fedha kutoka huko na hata haikuwa imerejesha hizo fedha Kwa vyama?
Baada ya mjadara mzito tulibaini yakuwa fedha nying ziliibiwa na aliye ziiba ni watendaji ambao mpk Leo baadhi Yao wapo.

Sababu nyingine ilikuwa ni mikopo ya ovyo ovyo iliyokuwa imetolewa Kwa watu binafsi na Amcos nyingi kuliko saccos.

Mikopo binafsi haikufata misingi ya kiushirika zaidi ilikuwa na chembembe za rushwa tu.

Mbaya zaidi aliyekuwa meneja wa muda mrefu aliyekuwa kinala wa kusimamia upotevu wa fedha alipo staffu tu akala shavu kubwa zaidi kupelekwa Tume ya maendeleo ya ushirika Dodoma maana yake aliyemteua alikuwa anamlinda hasije guswa sishangai Waziri mkuu kumpendekeza Bibi huyo ateuliwe na Raisi Ili alihali alikuwa na uchafu wa kuiua Benk hiyo.

Waziri mkuu alipiga sana kelele Kila alipotuma kikosi kinakuta anae guswa ni shoga Ake Kidawa.

Nina jua kabisa uteuzi wa mkurugenzi wa CRDB kuwa Kamishena wa Tume ya maendeleo ya ushirika Kuna jambo linaundwa na soon hicho kiti Cha ukurugenzi atakipoteza maana benk anayoongoza ndiyo iliyoua vyama vya Ushirika,Tanzania akitaka adumu basi afufue mafaili ya Kimei yamwoneshe jinsi yalivyoua Vyama vya ushirika Tanzania Kwa kushirikiana ma PASS Tanzania.

Nimeona vyama vyote vya ushirika vinalazimishwa kununua hisa paspo kuzingatia pahala vilipo,yaani saccos kutoka kagera,mwanza mbeya na rukwa na kwingine kote ni lazima kununua hisa Ili ni wazo zuri na Nina hakika vyama vitanunua na benk itatakiwa kufungua matawi mikoa hiyo ni wazo zuri sana

Ushauri wangu badili jina kutoka Kilimanjaro cooperative Bank iwe Tanzania cooperative Bank Makao makuu yake yawe Dodoma Moshi.iwe Branch,ushauri huu utaondoa Notion waliyonayo watu wengi yakuwa wanaingiza pesa za Kwa WACHAGA, watazitafuna maana wale watu na pesa ni balaaa!

Nina kwambia Mh wazir Nina hakika nalo maana Kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 nilipata bahati ya kuzunguka mikao sita ya Tanzania Bara na KUKUTANA na kauli hizo kutoka kwa viongoz wa vyama vya ushirika wengi waliunga mkono hoja ya ununuzinwa hisa ikiwa itabdili jina .

Naomba kuwasilisha kwako Waziri mzuri Hussein Bashe,ila nakuacha na swali moja,hivi.wajua TASSAF ni kitengo Cha watu kujipigia?jiulize Kwa Nini RuZuki ya pembejeo watu wameanza kutoa no za nida Ili wapewe RuZuki ya pembejeo najua uwezi nielewa NPM nikupe mtonyo watu wanao kupiga. Kiboya.
 
Back
Top Bottom