Kwako Waziri Silaa, vituo vilivyopo kwemye makazi ya watu siyo Mikocheni tu

Ukonga Moshi bar Kuna makazi ya watu chungu mzima, Shule (Moshi fountain) na hapohapo Kuna kituo Cha mafuta ya mitambo.

Slaa unatafuta popularity ya 2024/2025 ila kumbuka ubovu uliopindukia wa Barbara ya banana kitunda, njia panda Shule kivule Hadi njia panda ya Msongola unakusubiri.

Jimbo la ukonga ni sawa na halina mbunge Wala diwani. Kuna Diwani anaitwa Nyansika Getama Motena (Ngemo) amekuwa Diwani zaidi ya miaka 20 lakini n hopeless sawa na ww Slaa. Alianzisha msingi wa ujenzi wa kituo Cha polisi kivule miaka zaidi ya 10 iliyopita, juzi nlimkuta amesimama pale akidanganya kuwa anataka ujenzi wa kituo kile uanze!. Hii ni kwa sababu ya siasa za uongo, ulaghai na udanganyifu zilizozoeleka katika Kila tunapoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu.

Nani ana ushahudi kuwa ulikataa milioni 300?
Ulitangaza kwenye chombo kipi Cha habari wakati unakataa hizo milioni 300?

Unatutambia kuwa bado unakula urithi wa marehemu baba Yako ili tufurahi au tuhuzunike Kwa mbwembwe zako za ovyo?

Kulia kwako bungeni kuhusu uchakavu wa Barbara katika Jimbo la ukonga kulileta mabadiliko Gani chanya zaidi ya ubovu wa kupindukia wa Barabara ya banana kitunda had njia panda ya Msongola?

Acheni unafiki na uzandiki wa kutudhihaki sisi wananchi Slaa!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…