Duh!Hakuna mkataba wowote wa uendeshaji bandari uliosainiwa, ndiyo kwanza makampuni yanashindanishwa na TPA, vijana wanajilia mihela tu huko kila wanapochelewesha.
Makampuni gani "yanashindanishwa"?
Wewe huyo huyo umekwishaandika mara kadhaa humu, kwamba DP World, tayari anafunga vifaa bandarini, sasa tuelewe lipi?
Kama "Makubaliano", ambayo hutaki kuyaita jina la "Mkataba", ni mabovu, huo "Mkataba" wenyewe unaotokana na makubaliano mabovu utakuwaje?
Hata fikra tu za kufikiri hili kirahisi hivi hamuwezi?
Inaonekana sasa, kila mnaloleta kuwahadaa watu, mnazidi kuonyesha ubovu wa jambo lote mnalotaka kuwasukumia waTanzania.