Unajuwa sio kila anayepinga au kuunga mkono kalipwa hapana sio kweli ila ziko sababu, na nataka kuongelea hawa wazee maana huku nje tumegawanyika sana. Kuna watu walikuwa kwenye mfumo muda mrefu na wanadhani hawapewi heshima wanayostahili wao au kuna chuki dhidi ya CCM ndani ya mioyo yao mfano tu Warioba muda mrefu amekuwa kitu kinamsumbua kajaribu watoto zake wapenyeze kisiasa kapata ugumu halafu akiona watoto wa wenzake wanapata lazima inamuuma nafsi yake pia inamshusha kwa family yake. Ila huyu huyu siku mtoto wake akibebwa tu utasikia kauli tofauti wote wanajali family zao na matumbo tu sio taifa.Hao wezi waliokuwa wananufaika na Bandari wana nguvu sana; kama wameweza kumwonga na kumshawishi hadi Waziri Mkuu mstaafu Jaji Warioba , Mzee Butiku ambao ni wazee wa CCM nani tena watashindwa kumwonga?
Kwa taarifa zilizotoka hivi karibuni zinaonyesha wanaopinga mkataba huu ni wezi waliokuwa wananufaika na Bandari na kwamba wanatumia nguvu kubwa kuwahonga wananchi kupinga nia nzuri ya serikali.
Nini mtizamo wako kuhusu version mpya ya utetezi iliyoanzishwa na serikali? Hao wanaohonga ni wakina nani? Niwatanzania wenzetu? Kwanini serikali inashindwa kuwashtaki Kisutu? Je, wakishindwa kuwapeleka Kisutu watawezana na huyu bwana mwenye mkataba wakwenda kuishtakiwa Uingereza au South Afrika?
Kila siku tunatiwa hatiani huko ulimwenguni je tunapokwenda kumwabudu binadamu aitwaye DP World tutamdhibiti vipi asihonge?
Hawa hawa wanaokataa bandari wakati JPM anawapiga spana wazungu kwenye migodi walitoka hadharani na hasa Lissu kumponda JPM huyu anakurupuka ataleta shida na wawekezaji alisimama na wazungu 100% mpaka ndege inashikwa SA wakaanza kumkebei JPM, leo wamekuwa watetezi. CCM kosa walilofanya wao wangeanza na kuikataa DP tu wapinzania wangekuja CCM majambazi hawataki uwekezaji wangefanya wamewasikia wangepata wanachotaka na kukubali. Kuna watu kama watoto tu lazima ucheze na akili zao jifanye hutaki tu watapinga kumbe ndio unakotaka.