Kwamba Mzee Warioba, Butiku, Shivji, Bagonza, Pengo, Kitima wamelipwa kukataa Mkataba wa DP World?

Pengo
Kitima
Bagonza ..
Hawahitaji kuhongwa ...wao Wana uadui wa kiimani na waarabu....

Shivji haihitaji kuhongwa,Shivji ni Communist ndo maana wala hasemi mkataba urekebishwe ..anasema serikali ifanye kazi hiyo...haelewi dunia ya sasa hata serikali za Uingereza na Ujerumani zimebinafsisha bandari...
Shivji kabaki Karne ya 20...ya kina Nyerere na Mao Zedong...na Lenin ..

Warioba na Butiku wanahitaji anything wawe relevant....hawa ni wazee wa Karne ya 20... Hardliners conservative...wafuasi wa Nyerere....
Hawa wote wanaongea wanayo yaamini huku Karamagi akiwalainisha na kuwapa nguvu financially

Sorry umesema shivji hasemi mkataba urekebishwe?
Multiple times ame indicate hilo

Unatoa reference ya ujerumani, unajua terms and conditions za unerumani vs terms and conditon za tz?

Unatengeneza hoja nyepesi sana
 
Pengo
Kitima
Bagonza ..
Hawahitaji kuhongwa ...wao Wana uadui wa kiimani na waarabu....

Shivji haihitaji kuhongwa,Shivji ni Communist ndo maana wala hasemi mkataba urekebishwe ..anasema serikali ifanye kazi hiyo...haelewi dunia ya sasa hata serikali za Uingereza na Ujerumani zimebinafsisha bandari...
Shivji kabaki Karne ya 20...ya kina Nyerere na Mao Zedong...na Lenin ..

Warioba na Butiku wanahitaji anything wawe relevant....hawa ni wazee wa Karne ya 20... Hardliners conservative...wafuasi wa Nyerere....
Hawa wote wanaongea wanayo yaamini huku Karamagi akiwalainisha na kuwapa nguvu financially
Sikutegemea kuwashambulia Hao Wafuasi Thabiti wa YESU Ambao Wameyafuata na KUYAISHI MAFUNDISHO YAKE kwamba wana Chuki na uislamu bila kuweka ushahidi!
Mwalimu wao Mkuu Amefundisha!
[emoji116][emoji116]
Matthew 5:44
[44]But I say unto you, Love your enemies, bless them that curse you, do good to them that hate you, and pray for them which despitefully use you, and persecute you;

Sent from my vivo Y67 using JamiiForums mobile app
 
Pengo mnufaika wa kwanza, hao wengine wameshazeeka na wwananukuliwa vibaya na au wanaongozwa wajibu nini na waandidhi walionunuliwa.
Hivi ni wewe ulianzisha uzi mahali fulani ukitaka tujadili hili suala bila kutua matusi, kejeli na maneno ya kufedhehesha wengine ? Unayofanya hapa ni nini?
 
Huu ni mkataba mkubwa na wa kisasa. Mindset ni tatizo kubwa kwa maana ya watu kukosa ufahamu wa kipi kinachokwenda kufanyika na pia kuwepo kundi fulani la watu wanaofaidika na hizo biashara mfano za ICDs pembeni ya Port hawa ni tatizo kubwa kwani wanatumia nguvu kubwa mpaka ya hawa wazee wanasiasa wastaafu ilimradi waendelee kupotosha na kujificha kwenye siasa za uzalendo wa kuidai Tanganyika.

Hata hiyo Bagamoyo Port ilipingwa na hayati JPM tena mbele ya mkutano wa wafanyabiashara. Suala la bandari litapatiwa tu suluhisho japo muda huwa hauna urafiki kwa mipango ya binadamu.
Je marekebisho ya mkataba yanaweza kuathiri shughuli za uwekezaji?. Kwa sababu huo ni muongozo . Lakini mode operandi ndio tunayotaka Inakujaje ni shida. Je kuna ushahidi juu ya watu hawa kuzuia mode operandi? Au wanashaka na skeleton nzima kuwa haina afya. Je kuna ushahidi wa kuwa ni wafaidika kwa yanayoendelea pale na wanachekewa miaka yote are they very special not touchable
 
Hii inaitwa diversion na hakuna hoja. Ungeleta ushihi kuwa tuna icd 10 katibua hizo kadhaa zina uhusiano na mzee abc. Pia ungesema icd zitaathirika vipi na huu uwekezaji? Je zilizopo zinatosha au zitakuwa exclusively handled na mtu mmoja. Je itakuwa afya?.
 
Pengo mnufaika wa kwanza, hao wengine wameshazeeka na wwananukuliwa vibaya na au wanaongozwa wajibu nini na waandidhi walionunuliwa.
comment yako ni ushahidi kwamba umeshakuwa nyanya sasa!
Yaani Ukiandaliwa chakula na wajukuu unalalamika wanakupunja!
Ukiandaliwa chakula peke yako unadai mnaniona mchafu.... [emoji134][emoji12]

Sent from my vivo Y67 using JamiiForums mobile app
 
Hao wezi waliokuwa wananufaika na Bandari wana nguvu sana; kama wameweza kumwonga na kumshawishi hadi Waziri Mkuu mstaafu Jaji Warioba , Mzee Butiku ambao ni wazee wa CCM nani tena watashindwa kumwonga?

Kwa taarifa zilizotoka hivi karibuni zinaonyesha wanaopinga mkataba huu ni wezi waliokuwa wananufaika na Bandari na kwamba wanatumia nguvu kubwa kuwahonga wananchi kupinga nia nzuri ya serikali.

Nini mtizamo wako kuhusu version mpya ya utetezi iliyoanzishwa na serikali? Hao wanaohonga ni wakina nani? Niwatanzania wenzetu? Kwanini serikali inashindwa kuwashtaki Kisutu? Je, wakishindwa kuwapeleka Kisutu watawezana na huyu bwana mwenye mkataba wakwenda kuishtakiwa Uingereza au South Afrika?

Kila siku tunatiwa hatiani huko ulimwenguni je tunapokwenda kumwabudu binadamu aitwaye DP World tutamdhibiti vipi asihonge?
Hao wanaogopa influence ya mwarabu/uislam,na hiyo team uliyoweka ndiyo miongonimwa 'wafia dini' wa Vita vya msalaba Tanzania, uislam Tanzania uliingia kwa kuja mwarabu,miaka lukuki tumekua tukiikwepa misaada na mikopo ya mwarabu kwa kuogopa influence yake,hao siyo rejea ya maana,hawafikiri kwa akili huru
 
Pengo mnufaika wa kwanza, hao wengine wameshazeeka na wwananukuliwa vibaya na au wanaongozwa wajibu nini na waandidhi walionunuliwa.

Dp w si anapesa ameshindwa nini kuwapandia dau wamuunge mkono,mpuuzi ndio atakayeshabikia huo mkataba wa hovyo.
 
Hii inaitwa diversion na hakuna hoja. Ungeleta ushihi kuwa tuna icd 10 katibua hizo kadhaa zina uhusiano na mzee abc. Pia ungesema icd zitaathirika vipi na huu uwekezaji? Je zilizopo zinatosha au zitakuwa exclusively handled na mtu mmoja. Je itakuwa afya?.
Huwezi ukaweka ushahidi unaochukua nguvu nyingi kuupata, tambua tu ukweli kwamba uwepo wa ICDs ni sehemu ya michezo michafu ya kimfumo ni sehemu ya wachache haswa walio karibu na viongozi wa nchi kuendelea kuwafanya wengi wajinga kwa kutajirika kutoka na mifumo mibovu ya bandari katika ushushaji na upakiaji wa makontena.
 
Kwani hao walio karibu na viongozi wamasemaje?. Na dp huwa hana ICD si ndio?.
 
Je marekebisho ya mkataba yanaweza kuathiri shughuli za uwekezaji?. Kwa sababu huo ni muongozo . Lakini mode operandi ndio tunayotaka Inakujaje ni shida. Je kuna ushahidi juu ya watu hawa kuzuia mode operandi? Au wanashaka na skeleton nzima kuwa haina afya. Je kuna ushahidi wa kuwa ni wafaidika kwa yanayoendelea pale na wanachekewa miaka yote are they very special not touchable
Ni kupoteza muda kwenye mijadala mingi inayolenga kuendelea bandari kuwa na uendeshaji unaofuga wezi.

Sisi tunaokazana na hoja za mbwembwe za operandi bandari yetu inaweka foleni ya meli kule nje, mzigo wa meli mmoja mpaka ushuke tayari rushwa na wizi wa kila aina umeshafanyika.

Tunalia mkataba ubadilishwe hata ukifanyiwa mabadiliko kadri ya matakwa yetu bado watakuja wajinga wengine na hoja za kukwamisha biashara nzima. Huu ulimwengu haumsubiri mtu. wakati wabongo tumenasa kwenye akili za mijadala Zambia, Malawi, Congo wanajipanga kuitumia bandari ya Lobito kule Angola.

Tukumbuke kwamba SGR imejengwa kwa mabilioni ya shilingi tena kwa zaidi ya miaka mitano. Sidhani kama marehemu JPM huko alipolala kaburini anaridhika na huu upumbavu tunaofanya wa kuikosesha mzigo wa maana ambao ungeifanya iingize pesa yenye kutosha kabisa kurudisha gharama zote tulizotumia kuijenga.

Nimeelewa kwanini JPM hakutaka kabisa kuendekeza haya mambo ya kipuuzi ya demokrasia na hakutoa uhuru mwingi wa mijadala. Asingeweza hata kuifikisha nusu hiyo reli yenyewe.
 
Kwani hao walio karibu na viongozi wamasemaje?. Na dp huwa hana ICD si ndio?.
DP atake ICD za kazi gani wakati mitambo yake inashusha meli nzima ya kontena elfu tatu kwa siku mbili tu!.

DP ana mitambo ambayo hawa wauza madawa ya kulevya ndio unakuwa mwisho wao, hakuna magumashi ya kupitisha mizigo ya wizi pale TPA.
 
Hao wezi waliokuwa wananufaika na Bandari wana nguvu sana; kama wameweza kumwonga na kumshawishi hadi Waziri Mkuu mstaafu Jaji Warioba , Mzee Butiku ambao ni wazee wa CCM nani tena watashindwa kumwonga?

Kwa taarifa zilizotoka hivi karibuni zinaonyesha wanaopinga mkataba huu ni wezi waliokuwa wananufaika na Bandari na kwamba wanatumia nguvu kubwa kuwahonga wananchi kupinga nia nzuri ya serikali.

Nini mtizamo wako kuhusu version mpya ya utetezi iliyoanzishwa na serikali? Hao wanaohonga ni wakina nani? Niwatanzania wenzetu? Kwanini serikali inashindwa kuwashtaki Kisutu? Je, wakishindwa kuwapeleka Kisutu watawezana na huyu bwana mwenye mkataba wakwenda kuishtakiwa Uingereza au South Afrika?

Kila siku tunatiwa hatiani huko ulimwenguni je tunapokwenda kumwabudu binadamu aitwaye DP World tutamdhibiti vipi asihonge?
Walianza na version ya udini ikabuma, wakaja na version ya uzanzibari wa Rais ikabuma, wamekuwa na version ya kuhongwa nayo itabuma
 
Kama huelewi kuhusu IGA, elewa kuwa ni makubaliano yenye udhamini chini ya Umoja wa Mataifa, hakuna anaeweza kudhulumiwa kwa kuwa ni mjinga
Nionyeshe IGA yoyote ya kipuuzi kama ilivyo hii aliyoingia Samia, popote duniani.
Unadhani ukiweka "Umoja wa Mataifa" ndiyo watu wadanganyike?
Hii IGA imepitishwa Umoja wa Mataifa wakaisome ili ionekane kama inakidhi matakwa?
 
Hivyo viwanda alijenga nani?,walijenga wao au wewe,?!. Nani aliua viwanda vile?, vimekufa wao wakiwa madarakani au walisha ng'atuka?!. Dah, kweli jf imejaa takataka na mizoga.
Jf imejaa watu wenye akili nyingi wenye kila historia huyo butiku na baadhi yao ndio waliouwa viwanda vyote na kuvifilisi ,juhudi zote za Mwalimu zikawa ZERO!,achana na Sera ya kubinafsisha hii ilikuwa majuzi tu basda ya kuwa haviwezekaniki tena/rubbish!
 
Nionyeshe IGA yoyote ya kipuuzi kama ilivyo hii aliyoingia Samia, popote duniani.
Unadhani ukiweka "Umoja wa Mataifa" ndiyo watu wadanganyike?
Hii IGA imepitishwa Umoja wa Mataifa wakaisome ili ionekane kama inakidhi matakwa?
Ukishasema ya "kipuuzi" tayari umeshaonesha kuwa huelewi hata maana ya IGA ni nini.

Wala hauelewi kwanini serkali zinakuwa na makubaliano ya IGA.

Kwa kukupa darsa tu; makubaliano ya IGA yapo ya aina nyingi sana na kwa sura nyingi sana na yote yanahifadhiwa na kulindwa na Umoja wa Mataifa.

Porojo za hao mawakili uchwara ni kucheza na maneno tu. Kwenye mahakama za kisheria hawana mshiko hata kidogo.
 
Kwa kukupa darsa tu; makubaliano ya IGA yapo ya aina nyingi sana na kwa sura nyingi sana na yote yanahifadhiwa na kulindwa na Umoja wa Mataifa.
'Of course' IGA yapo ya aina nyingi, nani kabishia hilo?
Ndiyo maana hata hii ya kipuuzi inaitwa IGA

Kuhusu kuhifadhiwa na Umoja wa Mataifa kila aina ya IGA, hata za kipuuzi namna ya hii, unadhani ni nani anao muda wa kufuatilia huko Umoja wa Mataifa, kama hakuna kiwango maalum kinachotakiwa kuwemo kwenye hizo IGA za aina mbalimbali?

IGA inasema sheria zenu Tanzania ni substandard, hazifai; hii IGA imesema popote kwamba tutakwenda kusuruhishwa Umoja wa Mataifa kukitokea mtafaruku?

Unatumbukiza tu "Umoja wa Mataifa" humo bila kuelewa unachozungumzia ili uonekane unajua jambo, kumbe huna lolote ujualo.

"...makubaliano ya IGA.... yote yanahifadhiwa na "Kulindwa" na Umoja wa Mataifa"?
Huoni ujinga wa maandishi ya aina hii wewe?
Una maana gani na hiyo "kulinda"? Masharti ya hovyo yaliyomo kwenye IGA ile yalindwe vipi na Umoja wa Mataifa? Ni lini Umoja wa Mataifa" ukawa wakala wa ukoloni mpya?

Hovyo kabisa.
 
DP atake ICD za kazi gani wakati mitambo yake inashusha meli nzima ya kontena elfu tatu kwa siku mbili tu!.

DP ana mitambo ambayo hawa wauza madawa ya kulevya ndio unakuwa mwisho wao, hakuna magumashi ya kupitisha mizigo ya wizi pale TPA.
Icd kazi yake nini?
Madawa yanaingiaje kwenye huu mjadala
Vitu vinaibiwa vikiwa kwenye maji?
 
DP atake ICD za kazi gani wakati mitambo yake inashusha meli nzima ya kontena elfu tatu kwa siku mbili tu!.

DP ana mitambo ambayo hawa wauza madawa ya kulevya ndio unakuwa mwisho wao, hakuna magumashi ya kupitisha mizigo ya wizi pale TPA.
Acha kudhalilisha vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama!
Hawajashindwa kuwadhiti wezi na wazee wa ngada...
 
Back
Top Bottom