TICTS wamekuwa wawekezaji pale Bandarini kwa miaka 22, mbona haijawahi kuondoka mikononi mwa wananchi?.
Tatizo la sasa ni kwamba kuna wenye maslahi wanakwenda kupotezwa kabisa iwapo mfumo wa kuiendesha utakuwa mwingine tofauti na huu wa sasa.
Hao wazee na wao wanapitwa na wakati tena kwa kasi kubwa, wanachoshindwa kujiuliza ni kwamba pato la bandari linapoongezeka hata wao pesa za kuwatunza na familia zao zinaongezeka pia. Mipango ya kitaifa tunaiwezesha kwa pesa za ndani za kwetu wenyewe.
Tatizo wanakuja kujipotezea heshima yao uzeeni, japo sijui wamelipwa kiasi gani cha pesa na hao wapigaji wa bandarini.