Hao wezi waliokuwa wananufaika na Bandari wana nguvu sana; kama wameweza kumwonga na kumshawishi hadi Waziri Mkuu mstaafu Jaji Warioba , Mzee Butiku ambao ni wazee wa CCM nani tena watashindwa kumwonga?
Kwa taarifa zilizotoka hivi karibuni zinaonyesha wanaopinga mkataba huu ni wezi waliokuwa wananufaika na Bandari na kwamba wanatumia nguvu kubwa kuwahonga wananchi kupinga nia nzuri ya serikali.
Nini mtizamo wako kuhusu version mpya ya utetezi iliyoanzishwa na serikali? Hao wanaohonga ni wakina nani? Niwatanzania wenzetu? Kwanini serikali inashindwa kuwashtaki Kisutu? Je, wakishindwa kuwapeleka Kisutu watawezana na huyu bwana mwenye mkataba wakwenda kuishtakiwa Uingereza au South Afrika?
Kila siku tunatiwa hatiani huko ulimwenguni je tunapokwenda kumwabudu binadamu aitwaye DP World tutamdhibiti vipi asihonge?