Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Nina uhakika kina Mo na Bakhresa wanaunga mkono uwekezaji kwa asilimia mia moja, wanajua ni kwa namna gani utakavyorahisisha biashara zao kwa kupunguza muda wa bandarini.Watu ma failures eti ndio wakupe Ushauri ni upuuzi.
Tunaweza sikiliza Ushauri Kwa Mo, Bakhress,Rostam na Jumuiya ya wafanyabiashara ambao ndio wanalipa Kodi na ndio waajiri,hao waganga njaa wasubirie mengine.
Wezi na mafisadi wametengeneza aina fulani ya urasimu pale bandarini na unachelewesha utoaji wa mizigo na wao ndio mahali pa kupata pesa za wizi.
Mzigo ukiwa unatoka na kuingia kwa haraka hata hizo ICD zilizopo pembeni ya bandari zitakuwa hazina kazi kwani hakutakuwa na mzigo wa kuhifadhi eti kusubiri foleni bandarini ipungue!.
Hao wazee wanatumiwa na wezi ili kuijengea imani jamii ya wengi wanaosoma magazeti na kupata habari kwenye mitandao.