Kwangu mimi hiyo ndiyo hotuba ya maana kuliko zote zilizopata kuhutubiwa na Hayati mzee Nyerere

Kwangu mimi hiyo ndiyo hotuba ya maana kuliko zote zilizopata kuhutubiwa na Hayati mzee Nyerere

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200

Mzee Nyerere alijaaliwa hekima na busara za pekee mno na mwenyezi Mungu.

Ukiisikiliza hotuba hiyo hapo juu kwa mfano ni wazi unaona u Walimu wake kwenye muktadha wa kuonya,kuelekeza na kutabiri yawayo huko mbele ya safari.

Mengi kama si yote aliyopata kutuasa mzee wetu yule yalitimia ama yanaendelea kushuhudiwa.

Kwangu mimi hiyo hapo juu ndiyo hotuba yenye darasa zuri mno kwa mwanafunzi yeyote awaye atakaye kuja kuwa kiongozi wa Nchi yetu.

RiP mzee wetu.
 
Kwa nini mzee aliyejaa hekima na busara alikomalia sera za ujamaa na zilizoharibu uchumi na kuacha nchi masikini?
Nchi Masikini yenye watu wa kipato cha kati au nchi tajiri yenye asilimia 0.00001% matajiri wa kufa mtu na wengine mafukara wa kutupwa hata wakifa wanashindwa kukomboa maiti zao wakizeeka hakuna cha pension wala sehemu ya kujibanza (take your pick)

Moja pure ubepari upo kwenye makaratasi tu hakuna nchi 100% capitalist Hata huko Marekani na UK huenda kuna welfare kushinda hata sisi huku tunaojiona wajamaa...,

Kwahio bora wenzetu wenye safety net ya wasionacho ambao wanazidi kuongezeka siku baada ya siku kuliko sis bora liende kila mtu kivyake (that state of things is bound to bring havoc na mwisho wa siku ni machafuko na chuki katika jamii)
 
Jiulize Ujamaa ni nini alafu rejea China ni percent ngapi ya rasilimali ni state owned
Ujamaa wa Nyerere aliuandika mwenyewe katika kitabu chake cha UJAMAA - Essays on Socialism. China hawana kitu hicho sasa hivi. Walikuwa nacho wakati ule wa Cultural revolution ya Mao Zedong na alivyokufa wakautupa. Ndiyo baadaye viwanda vingi vya Ulaya na Marekani vikaenda kuwekeza kule China na kupaisha uchumi wao.
 
Nchi Masikini yenye watu wa kipato cha kati au nchi tajiri yenye asilimia 0000.01% matajiri wa kufa mtu na wengine mafukara wa kutupwa hata wakifa wanashindwa kukomboa maiti zao wakizeeka hakuna cha pension wala sehemu ya kujibanza (take your pick)

Moja pure ubepari upo kwenye makaratasi tu hakuna nchi 100% capitalist Hata huko Marekani na UK huenda kuna welfare kushinda hata sisi huku tunaojiona wajamaa...,

Kwahio bora wenzetu wenye safety net ya wasionacho ambao wanazidi kuongezeka siku baada ya siku kuliko sis bora liende kila mtu kivyake (that state of things is bound to bring havoc na mwisho wa siku ni machafuko na chuki katika jamii)
Ngoja kwanza niulize una umri gani? Maana kama ulizaliwa miaka ya 90's na kuendelea, hujui maisha waliyokuwa wanaishi Watanzania enzi za Nyerere. Ndiyo maana naona unataka kulanganisha umasikini wa Marekani na Ulaya na tuliokuwa nao wakati wa Nyerere. Haufanani.
 
Ujamaa wa Nyerere aliuandika mwenyewe katika kitabu chake cha UJAMAA - Essays on Socialism. China hawana kitu hicho sasa hivi. Walikuwa nacho wakati ule wa Cultural revolution ya Mao Zedong na alivyokufa wakautupa. Ndiyo baadaye viwanda vingi vya Ulaya na Marekani vikaenda kuwekeza kule China na kupaisha uchumi wao.
Vitu vinabadilika kutokona na wakati ila in essence hata the waamini wakubwa wa Socialism ni kwamba Commanding Heights za Economy zinakuwa State owned kwahio kilichopo China ni Socialist Market Economy ingawa private sectors zina-exist in parallel bado State inamiliki vitu vingi...
 
Ngoja kwanza niulize una umri gani? Maana kama ulizaliwa miaka ya 90's na kuendelea, hujui maisha waliyokuwa wanaishi Watanzania enzi za Nyerere. Ndiyo maana naona unataka kulanganisha umasikini wa Marekani na Ulaya na tuliokuwa nao wakati wa Nyerere. Haufanani.
Wewe unaanza kuleta ngonjera hapa..., shida zilizopatikana kipindi hicho zilitokea sababu ya nini ?, Kumbuka Nchi imechukuliwa bado changa, Huku vita baridi ya Marekani na Urusi Mabeberu ukicheza wanakuondoa (ulizia kina Patrice Lumumba, Sankara et al), mabaa ya njaa na ukame, vita na Uganda (na hapo pote hayo yalifanyaki bila kuchimba na kumaliza rasilimali zetu ambazo sasa hivi tunazichimba )

Pili hao wote unaoita mafukara na masikini waliweza kusomeshwa kwa pesa ya nchi (bila mkopo) ambapo sasa hivi na utajiri wetu tuliocheleweshwa sasa hivi tunao watu wanakosa hata mkopo wa Elimu.

Tatu vijiji vya ujamaa ambavyo kila anayehadithiwa anaona ndio ilikuwa kupotea nakuulizia hii miji ya sasa yenye huduma karibu (shule, hospitali soko n.k.) ni nini kama sio modern vijiji vya Ujamaa ?

Nimekuelezea hizo nchi Marekani, UK na hata Scandnavian kwamba ni welfare states kuliko hata sisi (yaani kwa maana nyingine wanatoa safety net kwa wananchi wao za kutosha)...
 
20211015_124514.jpg
 
Back
Top Bottom