jitombashisho
JF-Expert Member
- Jun 11, 2020
- 667
- 2,245
View attachment 2056609
Mzee Nyerere alijaaliwa hekima na busara za pekee mno na mwenyezi Mungu.
Ukiisikiliza hotuba hiyo hapo juu kwa mfano ni wazi unaona u Walimu wake kwenye muktadha wa kuonya,kuelekeza na kutabiri yawayo huko mbele ya safari.
Mengi kama si yote aliyopata kutuasa mzee wetu yule yalitimia ama yanaendelea kushuhudiwa.
Kwangu mimi hiyo hapo juu ndiyo hotuba yenye darasa zuri mno kwa mwanafunzi yeyote awaye atakaye kuja kuwa kiongozi wa Nchi yetu.
RiP mzee wetu.
Nyerere ni kweli alisomesha watu bure lakini uchumi ulimshinda kutokana na sera zake za kijamaa. Ukitaka kuleta visingizio vya nchi yetu changa, vita baridi, sijui ukame sivikubali. Kuna nchi za Asia zimepata uhuru baada ya sisi wameendelea. Ukame upo sehemu nyingi tuu lakini serikali zinapanga. Kabla ya vita na Uganda uchumi ulikuwaje? Maana vita na Uganda kila siku inatumika kama kisingizio cha kushindwa Nyerere kushindwa uchumi. Unafikiri ujamaa uliishia tuu vijijini? Kasome kitabu chake utaelewa Ujamaa alioufanya Nyerere hapa maana naona huna experience nao.Wewe unaanza kuleta ngonjera hapa..., shida zilizopatikana kipindi hicho zilitokea sababu ya nini ?, Kumbuka Nchi imechukuliwa bado changa, Huku vita baridi ya Marekani na Urusi Mabeberu ukicheza wanakuondoa (ulizia kina Patrice Lumumba, Sankara et al), mabaa ya njaa na ukame, vita na Uganda (na hapo pote hayo yalifanyaki bila kuchimba na kumaliza rasilimali zetu ambazo sasa hivi tunazichimba )
Pili hao wote unaoita mafukara na masikini waliweza kusomeshwa kwa pesa ya nchi (bila mkopo) ambapo sasa hivi na utajiri wetu tuliocheleweshwa sasa hivi tunao watu wanakosa hata mkopo wa Elimu.
Tatu vijiji vya ujamaa ambavyo kila anayehadithiwa anaona ndio ilikuwa kupotea nakuulizia hii miji ya sasa yenye huduma karibu (shule, hospitali soko n.k.) ni nini kama sio modern vijiji vya Ujamaa ?
Nimekuelezea hizo nchi Marekani, UK na hata Scandnavian kwamba ni welfare states kuliko hata sisi (yaani kwa maana nyingine wanatoa safety net kwa wananchi wao za kutosha)...
Hakika amenena vyema...
Rushwa, Udini, Ukabila ni mambo ya hatari sana...
Kwa nini Nyerere hakubadilika wakati China inabadilika na kufanya economic reforms? Mfano wa sera mbovu za Ujamaa wake alizofanya aliona wakati wa Cultural revolution ya China. Akaukomalia Ujamaa wake mpaka mwisho. Kama angetaka welfare state unayoifagilia wewe angewaiga hata Sweden kuliko kung'ang'ania Ujamaa wake.Vitu vinabadilika kutokona na wakati ila in essence hata the waamini wakubwa wa Socialism ni kwamba Commanding Heights za Economy zinakuwa State owned kwahio kilichopo China ni Socialist Market Economy ingawa private sectors zina-exist in parallel bado State inamiliki vitu vingi...
Aa!!..wapi, hotuba za kuongelea Wanawake weupe na kupiga Mashangazi wa Kimakonde.
We fisi kweli Bado unapambana na Magufuli tu inaonekana aliwashika pabaya
Hakuna ujamaa wa Nyerere kuna socialism inayobadilika kulingana na wakati, mahitaji na nyenzo ulizonazo, Kubadilika kwa China kumekwenda hatua kwa hatua..., Ujamaa na Kujitegemea ungefanyika sasa hivi kungekuwa hakuna mashamba ya kijiji ya watu kulima na Jembe la Mkono bali multi industrial automated farms ambazo zina tija (wakati ule zilikuwa hazipo sasa hizi technology ipo) Kwahio multi industries (commanding heights of the economy) kama ilivyo China bado zitakuwa mali za UMMA ingawa na private sectors zinafanya kazi sambamba...Kwa nini Nyerere hakubadilika wakati China inabadilika na kufanya economic reforms? Mfano wa sera mbovu za Ujamaa wake alizofanya aliona wakati wa Cultural revolution ya China. Akaukomalia Ujamaa wake mpaka mwisho. Kama angetaka welfare state unayoifagilia wewe angewaiga hata Sweden kuliko kung'ang'ania Ujamaa wake.
Sasa hivi Uchumi tulioweza upo wapi na maendeleo gani ? Ukizingatia sasa hivi tuna idadi kubwa ya rasilimali watu na madini tunayachimba kila leo, na kufungua milango ya kuuza kila kinachouzwa.., Uchumi umefikia wapi kwenye household level ? Watu hawana disposable income pamoja na vitu kuwepo buying power hakunaNyerere ni kweli alisomesha watu bure lakini uchumi ulimshinda kutokana na sera zake za kijamaa.
Alivyochukua nchi alikuwa na wataalamu wangapi na specialists wangapi ? Vita baridi sio story ilikuwepo na ulikuwa ukienda ndivyo sivyo unamalizwa uliza kuhusu kina SankaraUkitaka kuleta visingizio vya nchi yetu changa, vita baridi, sijui ukame sivikubali.
wameendelea baada ya muda gani, na katika scenarios zipi ? wameendelea sababu ya kutokuwa Wajamaa au kuna some extra issue in playKuna nchi za Asia zimepata uhuru baada ya sisi wameendelea.
Hivi wewe unajua ukame uliotokea miaka ya 70 na 80 kupelekea njaa na watu kula ugali wa yanga ? Hard times zipo dunia nzima kwa nyakati tofauti iwe America, Germany au UK zote zimepitia hard times nyakati tofauti na ilichukua muda kuondoka pale walipo Hata Marekani katika their Economic Boom in 60's baada ya stock market Crash watu walikuwa katika ufukara wa kutupwa (the unstability of capitalism boom and bust) au inflation and hyper inflation ya UK, leo mpo vizuri kesho uchumi unachokua a Nose Dive.... (Cycles of Boom and Bust)Ukame upo sehemu nyingi tuu lakini serikali zinapanga. Kabla ya vita na Uganda uchumi ulikuwaje? Maana vita na Uganda kila siku inatumika kama kisingizio cha kushindwa Nyerere kushindwa uchumi. Unafikiri ujamaa uliishia tuu vijijini? Kasome kitabu chake utaelewa Ujamaa alioufanya Nyerere hapa maana naona huna experience nao.
Sera ilikuwa nzuri, hii Sera lengo kuu ni nchi iwe ndo mmiliki kamili wa raslimali na mzalishaji ,kwa [emoji817]. nchi inazalisha bidhaa tosherezi ndani ya nchi,na ziada zinauzwa nje, kwa maana hiyo hii Sera hulifanya taifa kuwa na nguvu kiuchumi ,kwa sbb ya kuteka soko la ndani ,na nje,like China,they produce products for themselves & they sell surplus product to foreigner country!! Sera ilikuwa nzuri Sana lkn wahuni wakaivuruga!! Kama ingeenda vyema tusingekuwa hapa tulipo,kwani China wanaishi malaika!? Waliwezaje !!??Kwa nini mzee aliyejaa hekima na busara alikomalia sera za ujamaa na zilizoharibu uchumi na kuacha nchi masikini?
Kwanini Tanzania haijawa ya tatu kiuchumi duniani kama ilikuwa sera nzuri?Hata u China ni Nchi ya kijamaa na ambayo ndilo Taifa la pili baada ya USA kiuchumi Duniani.
Na hao Mabepari huko nchi zao zipo katika hatari ya watu kuandamana siku yoyote na kupinga kwamba tunanyonywa au kodi ya matajiri iongezwe ili sisi masikini tupewe...., au Kampuni yako kubwa sana ina monopoly tuivunje (Google, Microsoft, Amazon, Rockoffeller n.k.) Au Corporations kubwa kuhonga Policy Makers au mpaka hata Rais ili kupitisha sera zao thus kuibia wananchi (ENRON) Bila kusahau Profit at all Costs zinazoharibu Mazingira kila kukicha (In short mwananchi hata nafasi ni howmuch money to be made)Sera ilikuwa nzuri, hii Sera lengo kuu ni nchi iwe ndo mmiliki kamili wa raslimali na mzalishaji ,kwa [emoji817]. nchi inazalisha bidhaa tosherezi ndani ya nchi,na ziada zinauzwa nje, kwa maana hiyo hii Sera hulifanya taifa kuwa na nguvu kiuchumi ,kwa sbb ya kuteka soko la ndani ,na nje,like China,they produce products for themselves & they sell surplus product to foreigner country!! Sera ilikuwa nzuri Sana lkn wahuni wakaivuruga!! Kama ingeenda vyema tusingekuwa hapa tulipo,kwani China wanaishi malaika!? Waliwezaje !!??
Tumeachana na hizo Sera tumefungulia milango ambayo ilikuwa imefungwa na kuuza nchi left right and centre (Je hali ya Mwananchi imebadilika to the better )?Kwanini Tanzania haijawa ya tatu kiuchumi duniani kama ilikuwa sera nzuri?
Nyerere aliacha madaraka lini na tokea aondoke kwanini tumeshindwa kufikia hapo unapopataka?Ukitaka kujua kwa nini Nyerere na Ujamaa wake uliharibu uchumi na kuacha watu masikini msikilize huyu mchumi
Una uhakika?Hata u China ni Nchi ya kijamaa na ambayo ndilo Taifa la pili baada ya USA kiuchumi Duniani.
State inamiliki vitu gani?Vitu vinabadilika kutokona na wakati ila in essence hata the waamini wakubwa wa Socialism ni kwamba Commanding Heights za Economy zinakuwa State owned kwahio kilichopo China ni Socialist Market Economy ingawa private sectors zina-exist in parallel bado State inamiliki vitu vingi...
Uchumi wa Pakistan kwa siku za hivi karibuni umekua ukikua kwa Kasi lakini unfortunately ukuaji wake umekua ni kwa corporations,campanies na few Richie's,So the govt ilijikuta inatafuta ku punguza hiyo growth ambayo sio inclusive..Hakuna ujamaa wa Nyerere kuna socialism inayobadilika kulingana na wakati, mahitaji na nyenzo ulizonazo, Kubadilika kwa China kumekwenda hatua kwa hatua..., Ujamaa na Kujitegemea ungefanyika sasa hivi kungekuwa hakuna mashamba ya kijiji ya watu kulima na Jembe la Mkono bali multi industrial automated farms ambazo zina tija (wakati ule zilikuwa hazipo sasa hizi technology ipo) Kwahio multi industries (commanding heights of the economy) kama ilivyo China bado zitakuwa mali za UMMA ingawa na private sectors zinafanya kazi sambamba...
Sweden pamoja na welfare state (ambayo mimi siifagilii) inafanya nchi kama sweden kuwa na kodi kubwa sana sababu hizo pesa lazima zitoke sehemu ambayo ndio hio kuwaminya baadhi ili kuwapatia wengine..., ninachofagilia mimi sio kugawana mkate wa wengine wakishatafuta bali kupeana fursa ya kutafuta mkate huo....
To Each According to his Need..., From each According to his Ability (Though I believe Each should be given opportunity to earn his keep)