Kwangu mimi huyu ndio mzamiaji mwenye roho ngumu kinoma, wengine wanangoja

Kwangu mimi huyu ndio mzamiaji mwenye roho ngumu kinoma, wengine wanangoja

Zamani masela Toka kuja dar walikuwa wanapishana na wakaguzi wa tiketi wanapanda juu ya roof ya tren wanakaa juu wanapisha behewa wanadondokea dirisha la chooni au wanajichomeka chini ya viti wanalala kwa nyomi ile hakuna mkaguzi anakagua chini ya viti
Hii naijua mkuu, hata wale wezi wa mizigo mara nyingi walikuwa wakijificha huko juu ya roof ya treni bila kuonekana.
 
Halafu mtu kama huyo akijipata mnasema anaringa, muwe mnauliza kwanza viatu vyao.
Ya jamaa akitusua lawama zinakuwa kibao kwa ndugu jamaa na marafiki, bila kujua njia aliyotumia hadi mwamba akufanikiwa kutusua.
 
Pana dogo alitembea kwa mguu toka Mwanza Hadi south Africa means kwa kuunga unga lift but sehemu kubwa amekanyaga kwa mguu
 
Duh aisee, kweli watu wana mioyo ya paka katika kufikia malengo yao.
Inaitwa moto wa ndani attitude iwe mvua jua lzm ndoto itimie.
Pana jamaa ni tajiri ana maghorofa town alikuja toka bush mtoto wa miaka 14 akiwa masikini kabisa Tena kwa roli aliapata atarudi kijijini akiwa maiti au tajiri alianza kwa kuuza mifuko ya Rambo kwa mali kauli mdogo mdogo akaingia kwenye nguo za mitumba zikamlipa akaanza kwenda china kisha spea za magari akatoboa
 
sasa hivi kutoka dar mpaka lusaka kama huna 120,000 huendi.....

ila dar to harare ni 200,000 ...

gari zipo nyingi, classic, mashaallah n.k
Mkuu, saivi sasa Ukifika south for the first time, unapiga kazi gani sasa kihalali kabisa ili uanze kujitafuta..?
 
Mkuu, south saivi mtu anayekuja kujitafuta mpe ushauri, akifika ni shughuli gani anaweza kufanya..?
Za haram ni nyingi japo siwezi kukushauri kuja kuzifanya maana utaweka maisha yako hatarini na pengine kurudishwa maiti nyumbani.

Za halali ni chache kwa sasa kutokana na watu wengi kutoka nchi mbali mbali kuingia kwa wingi kuja kutafuta kazi hapa.

Kazi ambazo wengi hawana ujanja wa kuzifanya ni zile za mikono kama vile saluni au gereji. Hizi ni kazi zinazofanywa wa waburundi, wakongo, wabongo wachache na kiasi wamsumbiji na zimbabwe kwa upande wa gereji.
 
Back
Top Bottom