Kwangu mimi "Kikwete is the wisest Tanzanian president ever, he's intelligent"

Inategemeana na uwezo wako wa akili na hekima...
Mf. Darasa la kwanza huwaona walio la saba wanaakili nahekima mmmno...
Hata majambazi sugu mauaji huona matapeli kuwa "waizesti" saana
 
Nyerere Je?
 
Ndie mtu ninaemuiga sana maishani mwangu natamani sana siku moja nikutane nae nipige goti nimshike miguu nae anishike kichwa anibariki. (Hiyo ndio ndoto yangu)
Eh

Ova
 
Nimeusoma.. utawala wa nyerere unaonekana kwa macho hata kwa kuusoma tu. Kitendo cha kutuunganisha wa Tanzania kutokuwa na ukabila ni ushahidi tosha wa kuonesha alikuwa kiongozi bora..
Ok, Kabla ya uhuru katika kusoma kwako, kulikuwa na ukabila?
Viwanda alivyojenga na mali kibao za uma zilizopatikana awamu ya nyerere nimeziona wakati nikiwa mdogo.
Wakati tunapata uhuru aliachiwa nini na mwinyi alirithi nchi ikiwa katika hali gani kabla ya mkapa?
Kabla Mkapa hajaja kuviuza kifisadi na vingine kujiuzia yeye na familia yake
Mkapa alibinafsisha viwanda vikiwa vinafanya kazi vizuri? Sera ya ubinafsishaji ilikuwa na objective gani?

MKUU, HII NCHI ILIVYO, MIAKA 30 MBELE UNAWEZA SOMA HISTORIA YA JPM, JK UKASHANGAA NA MTOTO ALIYEZALIWA 2015 ASIKUELEWE UKIMWAMBIA TOFAUTI NA ANACHOKISOMA.
 
Chawa wa Kikwete
 
Kakisome tena. Hajaomba msamaha kwaufisadi aliofanya bali alikukiri maamuzi aliyochukua ya ubinafsishaji kuwa na makosa. Mkapa hajakiri kuwa yeye alikuwa fisadi.


View: https://youtu.be/whymEOI52WQ?si=gR_ghBWKXMj7POdw

Alijiuzia mgodi wa kiwira

Alijiuzia nyumba za serikali upanga, lushoto etc

Yeye mwenyewe mkapa amekiri ela za Epa alishiriki zipigwe.

Yeye mwenyewe mkapa amekiri alibinafsisha mali mpaka kwa shemeji zake

Mkapa ndie rais fisadi kuliko wote ndie pekee aliyefanya biashara akiwa ikulu.
 
Ok
 
Kwenye maembe mabovu unaweza pata yenye uozo nafuu, i.e kutokana na macho na ladha yako
 
Hii nchi ya ajabu sana....
Nikiwaangalia CHADEMA najichekea tu..
 
Bora usaliti urafiki usio na maslahi ya Taifa kuliko usaliti nchi YAko Kwa kumpa tu nafasi nyeti kwa sababu ni rafiki yako

Kwa hili Kikwete alionyesha uzalendo wa Hali ya juu
Na atakumbukwa daima na watu wenye akili na wazalendoo wa Taifa hili

Na Wakati huo naona unafiki mkubwa wa baadhi ya viongozi wasio na misimamo NDANI ya vyama vya siasa
 
Unahangaika ukiwa wapi? Kwa hiyo Kikwete alikuwa na maslahi gani kwa taifa?
 
Wakiondoka madarakani huwa na title mbili, wewe umekuja na mojawapo na wengine wanayo second title.
 
Unahangaika ukiwa wapi? Kwa hiyo Kikwete alikuwa na maslahi gani kwa taifa?
Kusome historia yake kati ya Marais waliongoza nchi kwa utawala Bora uone ni Nani
Waulize upinzani ulichanua awamu ipi ?
Ukimaliza nikuongezee mengine
Urais hawagawi kwa uswahiba Kama wapambavu wengine wanavyofikiri
 
this mwamba he's intelligent & wise hasukumwi na mihemko
Lakin yote kwa yote naamini anawapenda Watanzania that's why he ignores
Kuna mengi mazuri ya huyu mtu mtu
Mkuu Fene , naunga mkono hoja, tena mimi ni supporter wa mtu asifiwe akingali hai!.
Kikwete apewe maua yake!.
P
 
The guy is not wisest if he could be a wiser man asingemkata lowassa MTU aliyekuwa anapendwa na Watz wote nchi nzima that was hell
Sipo hapa kumsafisha Kikwete au kumsifia ila hata yeye Kikwete aliekuwa anapendwa sana na Watz tena kipindi kile hakuwa na kashfa zozote lakini jina lake lilikatwa kitaalamu

Kwenye siasa zetu za Tanzania Kuna nyuma ya pazia nyingi zinazotuacha vinywa wazi bila majibu inapokuja suala la wajumbe
 
Lakini kwani ni lazima Kanda fulani itoe Rais, amini ukweli nawaambia Kilichomnyima Lowassa Urais sio mgogoro na Mstaafu Kikwete Wala Nini , sio Mkatoliki full stop tukiwaambia Rais akiwa Mkristo lazima awe Mrumi, akiwa mwislamu lazima awe Bakwata uwa hamuelewi, sio vyote tunaweza kuandika hapa. Utashangaa litoto lisilojua chochote kwenye inner circle za nchi linabusha. Mnadhani kule Vatican Mama Samia kaenda kupiga picha? Rumi bado inacontrol mifumo mingi Sana, na ukienda kinyume na Maslahi yao utaundiwazengwe na wanaokuzunguka na hautajua Kama Rumi inahusika.

"Roma Locuta Causa Finito"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…