Omnilabeltech
JF-Expert Member
- Jul 26, 2026
- 533
- 845
- Thread starter
- #61
Mkuu,
Inawezekana kuna mara nyingi tu mtu mwenye hela ana akili. Kuipata hela ni vigumu, kukaa nayo ni vigumu zaidi, kuiwekeza izidi ni vigumu zaidi.
Kwa hiyo, hoja yako ina msingi fulani hivi wa ukweli.
Lakini, ni muhimu kuwa na kitu Waingereza wanakiita nuance.
Bila ya kuathiri uzuri na umuhimu wa hoja yako ya msingi, kwamba mara nyingi mtu kuwa na pesa inaonesha kuwa na akili, kuna namna nyingi ambazo pesa inaweza kuwapo hata bila ya mtu kuwa na akili , au, mtu mwenye akiki akakosa pesa.
1. Mtu A ambaye hana akili sana anaweza kupata bahati ya kuzaliwa katika nchi tajiri, na wazazi tajiri, wakati wa utajiri, akapata mifumo yote ya kumsaidia kuwa na pesa, bila ya kuwa na akili kubwa sana, akawa na pesa kuliko mtu B ambaye ana akili kumshinda mtu A, lakini hakuwa na bahati ya kuzaliwa nchi tajiri, au kuzaliwa na wazazi matajiri. Mwishowe ikawa mtu B ambaye ana akili sana kumshinda mtu A akawa masikini na mtu A ambaye hana akili kama mtu B, akawa tajiri.
Wewe unafikiri wale mabikionea wote wa Kinarekani wana akiki kuliko Waafrika wote ambao si mabilionea?
Kuna watu hawana pesa kwa sababu wamezaliwa katika famikia masikini, kwenye nchi masikini zisizo na mifumo mizuri tu.
2. Utajiri wa pesa pia unaendana na mambo mengi. Kuna watu hawana nia ya kuwa matajiri wa pesa. Kuna ma engineer wamegundua vitu muhimu sana kuanzia the original web browser na vingine vingi. Wakaamua kuvigawa bure watu wafaidike, badala ya kuviuza.
Kwao hawa, utajiri wa kazi zao kuibadilisha dunia ni muhimu zaidi kulijo utajiri wa wao kupata pesa.
3. Kuna watu wanapata pesa kwa uhalifu, wizi, udanganyifu, kuuza madawa ya kulevya, kuuza watu, kuuza silaha zinazoangamiza watu. Hawa unaweza kuwaona wana akili kwa sababu wana pesa, lakini pesa zao zinatokana na kuvunja maadili, na kuna watu wengine wengi ambao wangeweza kupata pesa kwa njia hizo, kuwazidi wao, lakini wamekataa kupata pesa kwa njia zisizofuata maadili.
Asante sana kwa maelezo haya Kiranga hapa mm hoja yangu n asilimia wengi wenye pesa ni watu ambao uwezo wao sio mdogo hasa linapo kuja suala la pesa wapo wanao zaliwa humo na wakaziendeleza baada ya kupewa misingi ya kuendeleza tena nadhani hii ita clarify zaid hoja yangu na watu kuielewa