Kwangu mimi, mtu mwenye hela ndo ana akili!


Asante sana kwa maelezo haya Kiranga hapa mm hoja yangu n asilimia wengi wenye pesa ni watu ambao uwezo wao sio mdogo hasa linapo kuja suala la pesa wapo wanao zaliwa humo na wakaziendeleza baada ya kupewa misingi ya kuendeleza tena nadhani hii ita clarify zaid hoja yangu na watu kuielewa
 

Sasa ndugu yangu hao wanao fanya hizo biashaea hawatumii akiki nying kufanikisha mambo yao?
 
Kuna kumiliki na pesa kukupitia tu
Kumiliki hahitaji kutumia akili zake mwenyewe, anaweza kuajiri meneja wa kizisimamia ziendelee kuzaliana.

Mfano kuna lottery millionaires walibahatika kuzipata hela lakini walikuwa hawana akili ya kuzimiliki, wakaajiri meneja wa kizisimamia.
 
Kumiliki hahitaji kutumia akili zake mwenyewe, anaweza kuajiri meneja wa kizisimamia ziendelee kuzaliana.

Mfano kuna lottery millionaires walibahatika kuzipata hela, wakaajiri meneja wa kizisimamia.

Sawa kufanya maamuz hayo tu tayari akili imetumika
 
Sasa ndugu yangu hao wanao fanya hizo biashaea hawatumii akiki nying kufanikisha mambo yao?
tofautisha akili na mbinu za kupata pesa, leo hii kuna wazee wengi wako vijijini huko wana maisha ya kawaida (hawana maisha) wanazidiwa na changudoa aliyepo mjini, kapanga apatiment in kila kitu ndani na ana uhakika wa kula, ila kaz yake ni kubadrisia madanga, tuseme nae ana akil kuzid hao wazee!

Kuna mtu kuwa na mbinu za kupata pesa, hii ni tofaut na akili
 

Mm sipo kwenye mbinu za kupata kumiliki hela sio kaz ndogo inahitaji akili
 
Kuwa na pesa si kipimo cha mtu kuwa na akili, kuna wenye pesa wanafanya mambo ya kijinga ambayo hata mtoto ukimueleza atakataa kufanya
 
Kwanza tujue akili ni kitu gani. Sababu kuna jamaa m1 yupo pale Lumo yombo ni kichaa lakini katika hali ya ukichaa huwezi kumfunga kwenye draft.
Hili jambo linanishangazaga sana.
 
Kwanza tujue akili ni kitu gani. Sababu kuna jamaa m1 yupo pale Lumo yombo ni kichaa lakini katika hali ya ukichaa huwezi kumfunga kwenye draft.
Hili jambo linanishangazaga sana.

Draft mchezo mrahisi tu huo ukipractice sana unaujua
 
Asante sana kwa maelezo haya Kiranga hapa mm hoja yangu n asilimia wengi wenye pesa ni watu ambao uwezo wao sio mdogo hasa linapo kuja suala la pesa wapo wanao zaliwa humo na wakaziendeleza baada ya kupewa misingi ya kuendeleza
Yani hata hao unaowaona uwezo wao si mdogo, inawezekana uwezo wao si mdogo kwa sababu walizaliwa na advantage ya kuzaliwa kwenye pesa.

Na hata unayemuona uwezo wake si mkubwa leo, inawezekana uwezo wake si mkubwa kwa sababu hakuzaliwa kwenye pesa kuuendeleza uwezo wake.

Pesa inawezesha mtu mwenye uwezo mdogo kuishi kwa kufikia full potential yake.

Pia, hivyo hivyo, kukisa oesa kunamzuia mtu mwenye uwezo mkubwa asiishi kufikia full potential yake.

Mfano kipimo cha full potential ni akili 100. Mtoto anayezaliwa kwenye pesa hana akili sana, anafikisha akili 60 tu kati ya hizo 100. Pesa inamuwezesha kufikisha hizo 60 zote anazoziweza. Atapelekwa shule nzuri, atapewa connections nzuri, atapewa mitaji mizuri, atafikisha hizo 60 na hizo 40 nyingine ataajiri watu wamfanyie kazi, atafikisha 100. Anatumia full potential zmyake na nyingine kaongeza za watu wanamsaidia mpaka kafika 100.

Mtu asiye na advantage ya pesa, hata kama anaweza kufikisha potential ya akili 100 zote, haendi shule nzuri, hana mtaji, hana connection, hawezi kuajiri mtu, akioata kidogo tu ukoo mzima unamtazama yeye, matojeo yake ana potential ya akili 100 lakini anatumia 40 tu.

Kwa hivyo hapo utaona mtu mwenye akili kubwa kazidiwa na mtu mwenye akili ndogo mwenye bahati ya kuzaliwa familia nzuri tu.

Muandishi wa Kifaransa, Honore de Balzac hakukosea sana aliposema "Behind every great fortune there is a great crime"

Na ukifuatilia pesa ndefu historia yake huko nyuma, utaona nyingi zimetokana na biashara haramu za utumwa, ukoloni, ujangili, wizi.

Soma historia ya utumwa, ukoloni mpaka Robber Barons wa Marekani, utaona hili jambo.

Kwa hiyo, kwa upande mmoja, pengine tofauti kubwa ya wenye pesa na wasio na pesa inaweza kuwa historia ya kukubali kutafuta pesa kwa namna yoyote huko nyuma, familia, nchi na jamii zilizokubali kutafuta pesa kwa njia yoyote, hata zisizo halali, nyingi zimerithisha vizazi mitaji na kuweza kuuendeleza utajiri.

Jamii ambazo zimekataa kufanya ujangili, kufanya biashara za utumwa, biashara za madawa ya kulevya, nyingi zimeshindwa kupata mitaji.

Kwa hiyo hapo unaweza kuona kuwa na oesa kunaweza kuwa alama ya kukubali kitafuta oesa kwa njia yoyote, hata isiyo halali, zaidi ya kuwa na akiki zaidi.

Kama kuna Chifu A wa kiafrika alikataa kuuza Waafrika wenzake utumwani, kwa kanuni kwamba hataki kuuza watu, na sababu hii ikapelekea Chifu huyu akose mali, na ukoo wake ukaenda kuwa masikini wa mali, na kuna Chifu mwingine B ambaye alikubali kuuza watu wake utumwani, na akapata mali, zikizofanya famikia yake ikawa matajiri wakubwa mpaka leo, utasema kwamba huyu Chifu B ana akili kuliko huyo Chifu A?
 
Mnacomplicate sana maisha, Kutafuta pesa haimanishi lazima uzipate.

Uwe na akili, usiwe na akili, Kuna wakati zinaweza kukipiga chenga tu.

Ndo maana, Matajiri sehemu yeyote ni wachache sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…