Kwangu mimi, mtu mwenye hela ndo ana akili!

Mnacomplicate sana maisha, Kutafuta pesa haimanishi lazima uzipate.

Uwe na akili, usiwe na akili, Kuna wakati zinaweza kukipiga chenga tu.

Ndo maana, Matajiri sehemu yeyote ni wachache sana.

Ndo ujue akili inahitajika mm nimeona watu weng wenye hela akili ipo wanauwezo wa kuona hatari
 

Kuna kitu kimoja kumiliki hela na hii Hela kuipata na kupotea hapa ndo panahitaj akili haijalish umerith au umezitafta mwenyewe
 
Unarud pale pale ukosefu wa akili na umaskini
Hili suala hujalifikiria kwa mapana na marefu yake......

Ungetakiwa ubainishe kati ya pesa na utajiri kipi kinahitaji uwe na akili kama ulivyoandika....

Pesa mtu yoyote anaweza kuwa nayo kwa namna ambayo yeye imempatia.....kuna watu wanashinda bahati nasibu na kupata pesa....kuna watu wanapata madini ya thamani na kupata pesa.......

Kumiliki pesa sio kipimo cha akili na wala sio maana ya utajiri
 
Kuna kitu kimoja kumiliki hela na hii Hela kuipata na kupotea hapa ndo panahitaj akili haijalish umerith au umezitafta mwenyewe
Mkuu,

Ikiwa mkondo wa kupata hela tu unaweza kwenda kwa bahati, usiende kwa akili, huoni kuwa mwenye akili kubwa sana anaweza asipate bahati hata ya kuanzia kumiliki hela (mfano kazaliwa familia masikini, nchi masikini), na hivyo uwezo wake hata wa kuiendeleza hela usijulikane.

Yani hatujui watu wengi Tanzania wakipata dola milioni moja wana uwezo gani wa kuizungusha, kwa sababu watu wengi Tanzania hawapati hiyo hela.

Wakati mtu mwenye bahati kubwa na akili ndogo anaweza kupata pesa kubwa sana kwa bahati ya kuzaliwa nchi tajiri, kwa wazazi matajiri, akapata dola milioni moja, akaitumia vibaya, jamii yake ikamwambia tunakuamini, hukupata ushauri mzuri, tutakupa a professional adviser akushauri mpaka ufanikiwe, hiyo ilikuwa bahati mbaya tu, akapewa tena mtaji na washauri, mpaka akafanikiwa?

Sasa ukiangalia mafanikio ya huyu Mmarekani aliyepewa tena na tena kwa sababu jamii yake ni tajiri, ina weza kum support sana, haina umasikini wa ku operate with a low margin, utasemaje huyu ana akili ya kuendeleza dola milioni moja kuliko yule ambaye hata hajapata nafasi kabisa ya kuanza, kwa sababu jamii yake masikini sana, haimpi support yoyote, tena inamtegemea yeye vibaya sana, ina operate under a very low margin hata kupata mkopo wa shilingi 50,000 tu ni tabu?

Unawezaje kusema yule Mmarekani kafanikiwa kuwa na hela kwa sababu ana akili na huyu Myanzania hajafanikiwa kwa sababu hana akili wakati hapo tatizo si akili, tatizo ni bahati ya kuzaliwa?
 
If you’re so smart,why aren’t You rich??
 
Tatizo linakuja pale pale miuu akili baba wacha niitumie vilivyo
Japo wengi hawakubaliani nawewe ila ukweli upo hivyo,kipimo kikubwa cha intelligence ni unataka nini katika maisha yako na umefanikisha vipi jambo lako..

Kusema kwamba unaweza kua na akili but ukakosa system ya kuku support kufanikiwa hiyo ni victim mentality tu..
 
Ukishakua na akili mojakwamoja huwezi kuValue material things. Usiniambie Mwijaku ana akili kuliko Plato
Materialism Vs Idealism 🤣🤣🤣💺💺💺
 
Akili (Intelligence) sio kitu kimoja tu, na mtu kuwa na akili nyingi darasani au kwenye biashara haimaanishi ana akili ya maisha au ya hisia.
Mwanasayansi wa saikolojia, Howard Gardner, aligundua nadharia inayoitwa "Multiple Intelligences" (Akili Mseto), ambayo inathibitisha kabisa mchanganuo wako: mtu anaweza kuwa gwiji katika eneo fulani, lakini akawa 'kilaza' kabisa katika eneo lingine.
Hapa kuna mtazamo mfupi wa maeneo uliyoyagusa, ambayo yanaonyesha jinsi binadamu anavyoweza kuwa imara au dhaifu:

1. Akili ya Hisia (Emotional Intelligence - EQ)

Hii ndiyo akili ya muhimu zaidi katika kulinda uhai na heshima ya mwanadamu. Kama ulivyosema, ukosefu wa EQ husababisha:
• Hasira isiyozuilika: Inayopelekea mauaji ya kifamilia (mume, mke, au mwalimu kuua mwanafunzi) na kuishia jela.
• Tamaa isiyozuilika: Inayomfanya mtu "azini zini ovyo" na kupata magonjwa kama UKIMWI au kuharibu familia yake.

2. Akili ya Kazi & Uchumi (Financial & Operational Intelligence)

• Akili ya Kazi: Uwezo wa kufanya jambo kwa ufanisi, kuwa mbunifu, na kutekeleza majukumu.
• Akili ya Uchumi: Hii siyo tu kutengeneza pesa, bali ni uwezo wa kuzitunza na kuzizalisha. Wengi wana akili ya kupata pesa, lakini wana 'ujinga' wa kuzitumia.

3. Akili ya Jamii (Social Intelligence / Social Capital)

Huu ndio uwezo wa kuishi na watu. Kama ulivyoiita "Mtaji wa Watu." Unaweza ukawa na pesa, lakini kama huna akili hii, unakuwa mpweke na huna mtu wa kukushika mkono wakati wa shida.

4. Akili ya Mapenzi (Romantic Intelligence)

Hapa ndipo palipo na "Anguko la Wakuu." Historia imejaa wafalme, marais, na matajiri wakubwa walioangushwa na mapenzi. Mtu anakuwa simba wa vita huko nje, lakini akifika kwa mwenzi wake anakuwa "mshamba wa mapenzi" na anasalitiwa au anafilisika kabisa kwa sababu hawezi kufikiri sawa sawa anapokuwa amependa.

5. Akili ya Kiroho (Spiritual Intelligence)

Uwezo wa kuelewa kuwa maisha yana upande usioonekana. Bila kuwa na utambuzi na nguvu za kiroho, mwanadamu anakuwa hana ngao dhidi ya mambo ya giza au anakuwa mtupu ndani ya nafsi yake (hata akiwa tajiri).

6. Shule (Darasani) dhidi ya Mtaa (Formal vs. Informal)

• Akili ya Darasani: Inasaidia kufaulu mitihani na kukariri mifumo.
• Akili ya Mtaani (Street Smarts): Inamsaidia mtu kusoma nyakati, kugundua matapeli, na kutoboa kimaisha hata kama hakusoma.
Hitimisho Lako ni Shule Tosha:
"Mtu anaweza akawa vizuri eneo moja akawa dhaifu eneo lingine." Lengo la mwanadamu timamu ni kujitathmini na kutafuta uwiano (balance) ili udhaifu wa eneo moja usije ukaharibu mafanikio ya maeneo mengine yote.
 
Kasusula alikua na pesa ila hakua na akili, Mr.Nice alikua na pesa ila hakua na akili... and so on...


Cc: Mahondaw
 
Mara nyingi, tatizo si kwamba akili zao hazisaidii, bali wana sifa zinazowakwamisha.

1. Ugonjwa wa Kuchambua Mambo Kupitiliza (Analysis Paralysis)

Watu wenye IQ kubwa hufikiria sana hatari (risks) kuliko fursa. Wanaogopa kufeli, hivyo wanachelewa kuchukua hatua wakati mtu mwenye akili ya kawaida (lakini ana uthubutu) anaanza biashara na kufanikiwa.

2. Kudharau Akili ya Mtaani (Street Smarts)

Shule inatufundisha kufuata sheria. Lakini kutengeneza pesa kunahitaji ujuzi wa kuhimili kukataliwa, kujadiliana (negotiation), na kujenga mahusiano (networking) vitu ambavyo havina mtihani wa darasani.

3.Ego (Kibri cha Elimu)

Wengi huamini kuwa kwa sababu wana vyeti, mfumo wa maisha unapaswa "uwalipe" tu. Wanashindwa kushuka chini na kujifunza biashara kuanzia sifuri.



Mwisho wa siku, dunia haikulipi kwa kile unachokijua inakulipa kwa kile unachofanya kwa kutumia kile unachokijua.
 
Nakubaliana nawe 💯
 

Lakin baada ya kushinda maamuzi ya pale ndo akili inahitajika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…