Kwani Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) haiwezi kuwa na accounts za malengo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza?

Itakuwa ni idea nzuri sana ila changamoto tuliyo nayo Tz ni usjmamizi uoneshao uaminifu na uwazi.

Mzee aliyeajiriwa miaka 30 iliyopita Leo hii anastaafu hadi anakufwa kama sio kufariki KIINUA MGONGO CHAKE KUKIPATA NI SHIDA he vipi au itakuwaje kwa mtoto ambaye amewekezewa fedha hizo toka kwa wazazi wake?

Once uzalendo,uwazi na uaminifu ukiwa dhahiri naamini hakuna litakalokuwa gumu.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Hii sio biashara mkuu, hapa unaweka pesa kwa ajili ya mtoto wako. Kama mwanafunzi atasoma mpaka kidato cha sita inakuwa hivi;

8,000 x 12 x 13 = 1,248,000

Mtoto wako anapewa mkopo huku tayari akiwa na collateral ya 1,248,000 kwenye account ya HESLB
Idea yako Ni nzuri, lakini unajua gharama za chuo za mwaka mmoja kwa mwanachuo mmoja?

Pili vipi concept ya "Time Value of Money"?? Yaan uweke 8,000/- leo Kisha baada ya miaka 13 uje upewe 8,000/- hiyo hiyo ni haki kweli?
 
Tatizo la waafrika tunapenda sana wizi na mambo yetu hayapo wazi kabisa
 
Nafikiri taasisi za kibenki zina jukumu la moja kwa moja na zinashughulika na hili, pia mifuko ya hifadhi ya jamii yaweza chukua hii hao ndio watu sahihi wenye uzoefu ktk masuala ya akiba ya kifedha...

Bodi ya mikopo yenyewe ibaki kama regulatory authority tu kwa vyombo vyote na taasisi zinazoshughulika na mikopo/akiba kwaajili ya elimu ya juu sio eti yenyewe nayo ifungue account.

Ili kuleta ufanisi, ni kutanua wigo wa huduma za mikopo na akiba kwaajili ya elimu ya juu zifanywe na taasisi nyingi na si kuiongezea taasisi moja majukumu...
 
Nafikiri taasisi za kibenki zina jukumu la moja kwa moja na zinashughulika na hili
Mkuu, siwezi kuingia JF kuishauri taasisi binafsi kwa maana hazina shukrani hata kidogo. Bora kushauriana na serikali yangu ambayo ninajua mwisho wa siku faida inakuwa kwa watanzania wote...
 
mifuko ya hifadhi ya jamii yaweza chukua hii hao ndio watu sahihi wenye uzoefu ktk masuala ya akiba ya kifedha...
Mkuu, hiyo mifuko ya hifadhi ya jamii watu wanawapigia kelel kila siku kwamba wanaonewa juu za pesa zao.

Sasa sijui ni kweli au wanawasingizia tu.
 
Bodi ya mikopo yenyewe ibaki kama regulatory authority tu kwa vyombo vyote na taasisi zinazoshughulika na mikopo/akiba kwaajili ya elimu ya juu sio eti yenyewe nayo ifungue account.
Kama NSSF na PSSSF wameweza kuwa mifuko ya kijamii kwanini HESLB isiweze kuwa mfuko wa kijamii ilhali inaihudumia jamii ya wanafunzi na sio wafanyakazi?...
 
Mkuu, siwezi kuingia JF kuishauri taasisi binafsi kwa maana hazina shukrani hata kidogo. Bora kushauriana na serikali yangu ambayo ninajua mwisho wa siku faida inakuwa kwa watanzania wote...
Nafikiri wapaswa fahamu mchango wa sekta binafsi ktk maendeleo ni mkubwa mnoo na hiyo serikali inatambua ushirikiano wa PPP ( Public and Private Partnership).

Taasisi binafsi zina shukrani kwa jamii, labda kama ni taasisi uchwara, ktk utendaji wake mathalani kampuni kitaalamu na kisheria zinapaswa kujitoa kwa jamii (corporate social Responsibility) sehemu ya faida yao wanairudisha kwa jamii achilia mbali kodi yao wanayochangia kwa serikali ambayo huleta maendeleo uyatakayo.

Uzoefu unaonyesha, huduma inayotolewa na serkali peke yake bila ushirikiano na sekta binafsi ina changamoto kubwaaa mifano ipo lukuki.
 
Mkuu, hiyo mifuko ya hifadhi ya jamii watu wanawapigia kelel kila siku kwamba wanaonewa juu za pesa zao.

Sasa sijui ni kweli au wanawasingizia tu.
Malalamiko yapo kila sehemu kwenye hizi taasisi haswa za serikali hata bodi ya mikopo inalalamikiwa mnooo.

Sasa je tunafanyaje?
 
Kama NSSF na PSSSF wameweza kuwa mifuko ya kijamii kwanini HESLB isiweze kuwa mfuko wa kijamii ilhali inaihudumia jamii ya wanafunzi na sio wafanyakazi?...
Kila chombo kinaundwa na sheria na kina majukumu yake mahususi. NSSF na PSSF wao wameweza sababu ni majukumu yao ya kimsingi ndani ya wigo wao, tena kuna mafao kwa wanufaika yanayogusa elimu.

HESLB wao sio jukumu lao, ni bodi ya mikopo yaani wao wanatoa tu funds kwaajili ya wanufaika kwa vigezo vyao, labda utaratibu ubadilishwe kuwezesha wazo lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…