Mimi namuelewa ila naelewa kwa nini Watanzania wengi wanakuwa wagumu kumuelewa.
Tumesema tuna nchi secular, kwenye mambo ya kitaifa, lakini hatuwezi kwenda na kile tulichokisema.
Mkitaka kufuata hizo dini, mtatakiwa muwafuate viongozi wa serikali, dini zingine zimesema watu wawatii viongizi, kwa sababu viongozi wamewekwa na Mungu, sasa hapo utasemaje unapinga uongozi kwa kutumia dini?
Naelewa wengi hamuwezi ku operate nje ya hii mental model ya dini, na ndiyo maana mnashindwa hata kuwatoa hao viongozi.
Kwa sababu badala ya kukataa udhalimu wao unaotumia dini kukandamiza watu, na nyie mnatumia dini kujenga all sorts of arguments from authority and time wasting abracadabras.