Kwani DCI Kingai na wenzie waliiitwa kumtetea Mh.Lissu , au kuja kuthibitisha uhaini wake?

Kwani DCI Kingai na wenzie waliiitwa kumtetea Mh.Lissu , au kuja kuthibitisha uhaini wake?

Walikuwa huru pia kutomtetea Lissu na kuwa upande wa Jamuhuri
Ndo walichokifanya, wamweleza hawawezi kumtetea kwa sababu wao ni sehemu ya Jamhuri. Sasa nyie msiolewa ndo mnaleta upotoshaji. Kweli hiki chama na wafuasi wao ni wapotoshaji sana. Kile kingine ni waongo ila hawa upande wa mtetezi ni wapotoshaji wa kutupwa
 
Hapo ndipo naelewa kwanini huwa mnabishana hovyo, leo ndiyo nimegundua kuwa kumbe huwa mnabishana bila hata kujua mnabishania kitu gani hasa.

Lisu alihitaji waje kuwa watetezi wake waje kumsaidia kumchomoa kutoka kwenye kitanzi, jamaa wakamwambia mwa kulifind mwana kuliget, sisi sio tuliokutuma wala hatuna ushirika na wewe kwenye mambo uliyoyafanya kwa utashi wako. Kwahiyo pambana na hali yako mwenyewe
Ulichelewa kulitambua ili ndugu,wabishi na watukanaji ila kumbe weupe tu. TUMUOBEE LISSSU ARUDI URAIANI NA MAISHA YAENDELEE
 
Walikuwa huru pia kutomtetea Lissu na kuwa upande wa Jamuhuri wangeitwa hostile witnesses

Hapo ndipo naelewa kwanini huwa mnabishana hovyo, leo ndiyo nimegundua kuwa kumbe huwa mnabishana bila hata kujua mnabishania kitu gani hasa.

Lisu alihitaji waje kuwa watetezi wake waje kumsaidia kumchomoa kutoka kwenye kitanzi, jamaa wakamwambia mwa kulifind mwana kuliget, sisi sio tuliokutuma wala hatuna ushirika na wewe kwenye mambo uliyoyafanya kwa utashi wako. Kwahiyo pambana na hali yako mwenyewe
Sikia ,ule uliikuwa ni mtego,Lissu anajua hakuna uhaini na kesi ishaisha Sema Mwamba alitaka waende kule ili akawabane na umma ujue maovu Yao.Kwenye dodoso akina Katuga wangejikuta ama hawana maswali au waulize maswali ya kuitia aibu serikali.Majamaa yamestuliwa yakalala mbele.Lissu ndo angewahoji kwanza kwa maana ya examination in chief Katuga angekuja kwenye cross examination.Serikali ilikuwa inaenda kuvuliwa hadi chupi nakwambia.
 
Hawa watu kupewa vyeo vikubwa inaamunika wana akili kubwa sana. Wao ndio viongozi wa vyombo.

Kupitia Kingai wametoa kauli kuwa hawako tayari kumtetea Mh. Lissu. Sasa najiuliza kwani waliitwa pale mahakamani kumtetea Lissu? Ama kueleza wanachojua kuhusiana na maswala ambayo Lissu atataka mahakama ijue? Kuwa shahidi haimaanishi kumtetea mtu bali kusema ukweli wa unachokifahamu.

DCI ni kiungo muhimu katika yale mashtaka, maana yake yupo kwenye nafasi ya kuthibitisha uhaini wa Lissu. Sasa inakuwaje anakataa kutoa huo ushahidi?

Na kwa nini hawa watu wamegoma kuja mbele ya mahakama? Kwa nini hawako tayari kuja kujibwa maswali ya dodoso hata kwa kusema NDIYO...HAPANA ..SIJUI?

Najiuliza maswali mengi sana. Fikiria hawa ni wakuu wa vyombo wakiongoza taasisi za ulinzi na usalama, iweje wamkimbie au kumuogopa mtu mmoja?
Mtu hanyongwi kwa kuwa wewe unatamani anyongwe.Mtu atanyongwa ikiwa ushahidi utathibiti jinai yake kwa mujibu wa Sheria.
 
Sikia ,ule ilikuwa ni myego,Lissu anajua hakuna uhaini na kesi ishaisha Sema Mwamba alitaka waende kule ili akawabane na umma ujue maovu Yao.Kwenye dodoso akina Katuga wangejikuta ama hawana maswali au waulize maswali ya kujitia aibu serikali.Majamaa yamestuliwa yakalala mbele.Lissu ndo angewahojinkwanza kwa maana ya examination in chief Katuga angekuja kwenye cross examination.Serikali ilikuwa inaenda kuvuliwa hadi chupi nakwambia.
Sasa ndiyo umeandika nini? Mahakama sio vijiwe vya kubishania mambo ya Simba na Yanga. Yaani haifanyi kazi zake kwa ushabiki bali utaratibu. One mistake, inakula kwako.
 
This is crap

Unatetea au unashitaki but means ndio ushuhuda

Huwezi kwenda mahakamani ukasema mimi Siko upande wowote lakini natoa ushahidi
Shahidi anaenda mahakamani akiwa anajulikana anaenda upande wa mshtaki au mshtakiwa
 
Sasa ndiyo umeandika nini? Mahakama sio vijiwe vya kubishania mambo ya Simba na Yanga. Yaani haifanyi kazi zake kwa ushabiki bali utaratibu. One mistake, inakula kwako.
Hujaelewa au huna uwezo wa kauelewa.Hujui kwamba Lissu alitakiwa kuwauliza maswali mashahidi wake! Hujui kwamba yeye asingekuwa na mpaka kwamba angewapiga maswali ya Kila aina? Hujui kwamba Lissu ana uwezo wa hali ya juu katika kuuliza maswali.Kama Katuga aliuliza mpaka mali binafsi za Heche ,nini kingemkataza Lissu kuwaperembesha akina Kingai?
 
Hujaelewa au huna uwezo wa kauelewa.Hijui kwamba Lissu alitakiwa kuwailiza maswali mashahidi wake! Hujui kwamba yeye asingekuwa na mpaka kwamba angewapiga maswali ya Kila aina? Hujui kwamba Lissu ana uwezo wa hali ya juu katika kuuliza maswali.Kama Katuga aliuliza mpaka mali binafsi za Heche ,nini kingemkataza Lissu kuwaperembesha akina Kingai?
Mahakamani ni kama mchezo wa draft, wakati wewe unasukuma kete ili mpinzani wako aingie kwenye mfumo tambua unayecheza naye pia ana haki ya kusukuma kete zake ili wewe ujae kwenye mfumo pia.

Kwahiyo yeye alitumia haki ya kusukuma kete zake ambazo aliamini zingempa ushindi, na serikali nayo ikatumie haki ya kuchagua kete ya kucheza dhidi ya mitego na hila za mpinzani wake.

Wengi mnachokosea ni kulazimisha upande pinzani ucheze kete ileile ambayo Lisu alitaka wacheze, mkahasau kuhifadhi haki ya Serikali nayo kuchagua kucheza kete inayoona inafaa.

Ndiyo maana kwenye draft ukizingiua utaona mpinzani anakula kete zako hata tatu at once, na ukikaa vibaya unapigwa super kabisa.

Kwahiyo ukimpeleka mpinzani kwenye mtego, yeye kuuruka mtego wako sio kosa, ni kanuni za kawaida za mchezo.

All warfare based ona Deception~Sun Tzu
 
Nashangaa asilimia 75 waliochangia huu uzi wameandika utumbo mtupu . Serikali inataka maridhiano na inaonekana maridhiano bila CHADEMA hayawezi kuwa maridhiano.

Kipi kinachowafanya mfurahie Lissu akinyongwa ? Je maridhiano yatakuwepo ? Au tutaendelea kuishi hivi hivi ? Wakati mwingine itikadi za kipuuzi huwa ni sumu mbaya ambayo madhara yake huenda yasionekane sasa lakini miaka ya mbele watakaopata shida na mateso ni vizazi vyenu.

Ifikie hatua tuwe tunajiuliza, kweli kuna uhaini ulipangwa kufanyika ? Na kama kuna uhaini ulipangwa ni nani anayeumia ?

Mitanzania baadhi ni Mipumbavu kupindukia. Lissu akinyongwa kwa uhaini ambao hata haupo kipi kitakachowafurahisha?
 
This is crap

Unatetea au unashitaki but means ndio ushuhuda

Huwezi kwenda mahakamani ukasema mimi Siko upande wowote lakini natoa ushahidi
kwani "kuwa na upande" ndio kutetea? Shaihidi anakisema anachokijua kuhusu jambo bishaniwa. (fact in issue) Mambo hayo atakayoyasema yanaweza yakawa na faida kwa upande wowote aidha wa mashtaka ama mshtakiwa.
 
Shahidi anatakiwa kueleza kile anachokifahamu na sio kukutetea
 
Hawa viongozi wa Ulinzi na Usalama walikua Mashahidi Muhim kwa Upande wa Mashtaka..

Kwakua hawakuitwa, Upande wa Utetezi ukawahitaji ili wathibitishe Uhaini wa Lissu kama ambavyo wangeuthibitisha kama wangeitwa upande wa Mashtaka.

Sababu za kutoitwa upande wa Mashtaka ndio sababu zilizotumika kuwaita upande wa utetezi na ndio maana na huku wamegoma kama kule kwakua lrngo lao ni kumkomoa Lissu kama alivyosema Kingai.

Nawaza tuu, Lissu akiachiliwa huru ina maana Kina kingai watachukia na ndio viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Tutegemee kesi nyingi nyingine za Lissu mpaka siku watakapofurahi.
 
Hawa watu kupewa vyeo vikubwa inaamunika wana akili kubwa sana. Wao ndio viongozi wa vyombo.

Kupitia Kingai wametoa kauli kuwa hawako tayari kumtetea Mh. Lissu. Sasa najiuliza kwani waliitwa pale mahakamani kumtetea Lissu? Ama kueleza wanachojua kuhusiana na maswala ambayo Lissu atataka mahakama ijue? Kuwa shahidi haimaanishi kumtetea mtu bali kusema ukweli wa unachokifahamu.

DCI ni kiungo muhimu katika yale mashtaka, maana yake yupo kwenye nafasi ya kuthibitisha uhaini wa Lissu. Sasa inakuwaje anakataa kutoa huo ushahidi?

Na kwa nini hawa watu wamegoma kuja mbele ya mahakama? Kwa nini hawako tayari kuja kujibwa maswali ya dodoso hata kwa kusema NDIYO...HAPANA ..SIJUI?

Najiuliza maswali mengi sana. Fikiria hawa ni wakuu wa vyombo wakiongoza taasisi za ulinzi na usalama, iweje wamkimbie au kumuogopa mtu mmoja?
Lissu mwenyewe aliwaorodhesha hao kama mashahidi wake kwa upande wa utetezi, wewe unaleta story ambayo Lissu wala Mahakama hawakusema hivyo
 
Kayakanyaga huyo Rasta. Hata asiponyongwa atakuwa kajifunza mengi. Roho za watz zinamlilia milele kwa kuhamasisha kwake uasi uchwara.
 
Back
Top Bottom