Kwani field wanachuo huwa tunaenda kufanya nini?

Kwani field wanachuo huwa tunaenda kufanya nini?

Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo kimoja hapa Tanzania.

Chuo kilitupa nafasi ya kuchagua sehemu ya kufanya field kwenye account ya SIMS, nikachagua kufanya field VETA mojawapo hapa Tanzania

Cha ajabu huku wametupokea lakini hakuna tunachofanya, hakuna mwenye habari na sisi.

Mi nilidhani tunaenda field kufanya kazi zinazohusiana na fani zetu na kujifunza kiundani lakini huku niliko hakuna kinachofanyika.

Silaumu mtu lakini nawaza kama hii VETA haikuandaa program zozote kwa watu wa field kwa nini sasa walikiambia chuo kuwa nafasi zipo. Wametualika tuje kufanya nini exactly, au ili tu ionekane tumekuja field?

Leo ni siku ya pili kuwa hapa na tayari nimeanza kujuta ukizingatia niko mkoa wa watu nimetafuta hadi chumba just to sit all day kila siku

Nakumbuka chuo walikuwa wanatuambia mkienda field msipoteze muda kuchezea simu. Sasa kwa hali hii utafanya nini zaidi ya kutumia simu.

Kama taasisi yenu haina kitu cha kuoffer wanafunzi wa field msiwe mnakuja kutoa nafasi kwa wanafunzi, mnadai mnahitaji watu na wanaapply wanakuja kumbe hakuna cha kufanya, ni kupotezeana muda

Hivi ni sehemu zipi nzuri kuapply field ambapo unaweza kufanya real tasks au real practicals badala ya kukaa tu siku nzima?

(Kozi ni Mechanical Engineering). Naombeni ushauri ili safari ijayo nisichague tena sehemu ambazo tunaenda kukaa tu na kupoteza muda without learning anything.

Natamani nijue kwa uzoefu wenu kama kuna sehemu mliwahi kwenda mkafanya field effectively
ujue VETA zina specialization
isije kuwa umeenda VETA specialized kwa Hospitality na wewe ni Mechanical Engineering
wewe ulitakiwa uchague VETA zinazo tengeneza vifaa vya kilimo/ujenzi nk nk
 
Swali lako ni swali la Aibu sana Mkuu.

Umefundishwa mwaka mzima au miaka miwili. Unapelekwa field ku- practice ulichojifunza. Bado hujui umeenda kufanya nini?

Field ni mafunzo kwa vitendo. Unaenda kufanya ulichofundishwa kwenye nadharia.
Kama ni msaada utaupata mdogo sana kutoka kwa wafanyakazi wenzako au boss utakayemkuta huko.
 
ujue VETA zina specialization
isije kuwa umeenda VETA specialized kwa Hospitality na wewe ni Mechanical Engineering
wewe ulitakiwa uchague VETA zinazo tengeneza vifaa vya kilimo/ujenzi nk nk
No, zipo workshop zote za Mechanical huku
 
Swali lako ni swali la Aibu sana Mkuu.

Umefundishwa mwaka mzima au miaka miwili. Unapelekwa field ku- practice ulichojifunza. Bado hujui umeenda kufanya nini?

Field ni mafunzo kwa vitendo. Unaenda kufanya ulichofundishwa kwenye nadharia.
Kama ni msaada utaupata mdogo sana kutoka kwa wafanyakazi wenzako au boss utakayemkuta huko.
Labda kama hujui kila sehemu ina utaratibu. Umewahi kwenda VETA yoyote?
Kwamba unaingia unaanza kujifanyia kazi unazojisikia au unamaanisha nini?
 
Endelea Kuchezea Simu...
Tutakuja Kukubeba Na Kukupeleka Unapohitajika Kufanya Fildi Yako..
​
 
Aina ya wasomi wa namna hii ni tabu ,so una siku ya pili ukipewa kazi utaweza , kufanya kazi ni pamoja na kuzoea mazingira ..Nyie madogo hizo kazi mkipewa mtaanza kuomba excuses , mnakuja sehemu hata kujaza excel hamuwezi , yaani hata kushika mouse hamjui ila mntaka kwenda site sio hivyo mzee ...Field , ni pana sana unatakiwa kujua mazingira ya kazi . Tulia dogo , usome mazingira , jifunze tu kuwahi kazini ...Baadhi ya mambo hauwezi kufanyia kazi kama novice , utaweza kuharibu kazi .

Jifunze hta kutumia excel usiwe na mbwembwe nyingi .
Hawa ni sawa na wale wanaajiriwa Leo kesho anataka hujui wa idara au kitengo , gari nk
Kisa kasoma udsm
 
Mwaka Kesho karibu EACOP utajenga ujuzi na kazi utafanya haswa na malipo juu sema ndio ujiandae kabisa na interview.
Ikiwezekana uombe na Gasco/Tpdc
 
Yaani uko mazingira ya kazi na huoni cha kufanya…Mimi mwenyewe nasoma nje ndo kwanza niko mwaka wa kwanza ila ukitaka content zangu njoo pm nikupe instagram yangu uone nachokifanya..fake it until you make it
 
Field ni pamoja na kujifunza kuishi na watu, kuchangamana nao, kujua mazingira na taratibu za ofisi nk. Hayo malalamiko yako mwambie immediate supervisor wako. Kama ndio huna mpango nae maana wewe msomi basi utaendelea na simu yako
 
Nimekuelewa
 
Yaani uko mazingira ya kazi na huoni cha kufanya…Mimi mwenyewe nasoma nje ndo kwanza niko mwaka wa kwanza ila ukitaka content zangu njoo pm nikupe instagram yangu uone nachokifanya..fake it until you make it
Yaani aanze tuu kufanya vitu bila mapokezi wala muongozo
 
Yaani aanze tuu kufanya vitu bila mapokezi wala muongozo

IPO hivi field ni mambo mengi hata kujifunza vifaa vya kazi namna ya ku vitunza na kuvi maintain pia ni activities hizo anazoweza kuzijaza kwenye report yake..kujua idara mbali mbali za hapo veta pia ni kazi hio sasa kama yeye amekaa tu hata kugusa vifaa hagusi labda kama wanakatazwa kwenda store wakae tu ofisini
 
Mambo yote hayo mtu ana fanya baada ya kupokelewa na kupewa muongozo wa nn cha kufanya
 
Yaani aanze tuu kufanya vitu bila mapokezi wala muongozo

Kwa mfano mimi nasoma environment engineering japo ndo kwanza hata sijafikia kufanya field ila mwenyewe tu nishatembelea kituo cha maji japo niliishia kupiga picha mitambo yao,nikaenda kwenye bwawa limehifadhiwa nikaona wanavyo operate nikapiga picha nikaenda sehemu wanajenga daraja nikaona wanavyozingatia safety nikapiga picha nikatembelea bustani za miti sehemu nikaongea na mtunzaji hayo yote nayafanya mwenyewe peke yangu….labda kwa kuwa mimi tayari ni mtumishi nayejiendeleza hivyo nina experience na fields work lakini maana yangu ni kwamba mwanafunzi asikae tu kusubiri activities zipangwe apelekwe mambo ya serikali si unayajua wanaweza hata week wakamaliza hakuna schedule yoyote ya field work so ni yeye kujiongeza tu kwa sababu lengo la field kuu ni report kwenye logbook yake
 
Back
Top Bottom