Kwani field wanachuo huwa tunaenda kufanya nini?

Kwani field wanachuo huwa tunaenda kufanya nini?

Hiyo veta haina workshop?...nimeenda veta kadhaa zina workshop ambazo zipo busy balaa sasa wewe sijui upo veta ya mkoa gani?...
 
Ukienda field sio kama watu walikuwa wanakisubiria wewe uende ili ukafanye kazi zao
Ni jukumu lako kuulizia sehemu inayohusika na field yako wewe unawafata watu wanapoenda
Mtu hawezi from nowhere akupangie kabla wewe wenyewe hujajiongeza.
 
hongera na pole!!
kwanza kunakuandaa ratiba ya field kutokana na uhitaji idadi ya walio ripoti inawezekana kuna wenzako wa chuo kimoja au tofauti wantaka kuwaunga pamoja,pili usilaumu kuwa wanataka watu sema wewe ndo unataka field kwa kua bila wewe kazi zao zinaenda.
tatu kabla ya kuomba field chunguza aina ya field na aina ya ofisi unayotaka kwenda kuna kitu kinaitwa organisation culture kina athiri mambo mengi .
nne tafuta mentor ,jishushe ishi km mtendaji sio km bosi utashirikishwa mengi na pia unaweza ukapata mchongo wa ajira hapo hapo
 
Aina ya wasomi wa namna hii ni tabu ,so una siku ya pili ukipewa kazi utaweza , kufanya kazi ni pamoja na kuzoea mazingira ..Nyie madogo hizo kazi mkipewa mtaanza kuomba excuses , mnakuja sehemu hata kujaza excel hamuwezi , yaani hata kushika mouse hamjui ila mntaka kwenda site sio hivyo mzee ...Field , ni pana sana unatakiwa kujua mazingira ya kazi . Tulia dogo , usome mazingira , jifunze tu kuwahi kazini ...Baadhi ya mambo hauwezi kufanyia kazi kama novice , utaweza kuharibu kazi .

Jifunze hta kutumia excel usiwe na mbwembwe nyingi .
pia kwenye taasissi za umma wanaogopeka wanaweza toa SIRI za serikali kuna vitengo uwa wanakuwa makini nao sana aswa uhasibu na fedha,unaweza kuta dogo akitoka ofisini anaanza simulia kijiweni matumizi au mapato ya ofisi na ndio maana kuna taasisi hazitaki issue za field kutokana na nature ya ofisi au majukumu wanapewa yasiyo na SIRI nyingi ndo wengine uangukia kutumwa chai na kahawa na maboss,all in all field ni usenge mtupu nimeshawahi tumwa chai na demu nikiwa field tanesco sema watumishi masela wakanikataza nisiende kumchukulia
 
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo kimoja hapa Tanzania.

Chuo kilitupa nafasi ya kuchagua sehemu ya kufanya field kwenye account ya SIMS, nikachagua kufanya field VETA mojawapo hapa Tanzania

Cha ajabu huku wametupokea lakini hakuna tunachofanya, hakuna mwenye habari na sisi.

Mi nilidhani tunaenda field kufanya kazi zinazohusiana na fani zetu na kujifunza kiundani lakini huku niliko hakuna kinachofanyika.

Silaumu mtu lakini nawaza kama hii VETA haikuandaa program zozote kwa watu wa field kwa nini sasa walikiambia chuo kuwa nafasi zipo. Wametualika tuje kufanya nini exactly, au ili tu ionekane tumekuja field?

Leo ni siku ya pili kuwa hapa na tayari nimeanza kujuta ukizingatia niko mkoa wa watu nimetafuta hadi chumba just to sit all day kila siku

Nakumbuka chuo walikuwa wanatuambia mkienda field msipoteze muda kuchezea simu. Sasa kwa hali hii utafanya nini zaidi ya kutumia simu.

Kama taasisi yenu haina kitu cha kuoffer wanafunzi wa field msiwe mnakuja kutoa nafasi kwa wanafunzi, mnadai mnahitaji watu na wanaapply wanakuja kumbe hakuna cha kufanya, ni kupotezeana muda

Hivi ni sehemu zipi nzuri kuapply field ambapo unaweza kufanya real tasks au real practicals badala ya kukaa tu siku nzima?

(Kozi ni Mechanical Engineering). Naombeni ushauri ili safari ijayo nisichague tena sehemu ambazo tunaenda kukaa tu na kupoteza muda without learning anything.

Natamani nijue kwa uzoefu wenu kama kuna sehemu mliwahi kwenda mkafanya field effectively
jiongeze....
 
Nitafuata huu ushauri
Ila field kumbe inahitaji uzoefu? Sasa uzoefu tunapatia wapi, nilidhani uzoefu unapatikana kwa kufanya kazi mara kwa mara, na kazi unaanza kwa kuelekezwa. So kama hakuna kazi ya kuwapa watu wasio na uzoefu maana yake walikuwa hawahitaji wanafunzi wa field, halafu wenyewe ndio walisema wanataka wanafunzi wa field. It doesn't make sense
Mzee wa kazi kwa unavyotaka utachelewa sana field sisi tulikuwa tunajiongeza siyo kila kitu hadi uambiwe tukajikuta tunajua welding, kusuka hadi mota kitu ambacho ilikuwa ni taaluma ya electricians na kufanya soldering kabisaa.
 
pia kwenye taasissi za umma wanaogopeka wanaweza toa SIRI za serikali kuna vitengo uwa wanakuwa makini nao sana aswa uhasibu na fedha,unaweza kuta dogo akitoka ofisini anaanza simulia kijiweni matumizi au mapato ya ofisi na ndio maana kuna taasisi hazitaki issue za field kutokana na nature ya ofisi au majukumu wanapewa yasiyo na SIRI nyingi ndo wengine uangukia kutumwa chai na kahawa na maboss,all in all field ni usenge mtupu nimeshawahi tumwa chai na demu nikiwa field tanesco sema watumishi masela wakanikataza nisiende kumchukulia
Tufanye ungemchukulia Ile chai. Ungepungukiwa nn haswa? Nyie vijana mna safar ndefu sana. Wewe una kabachelor tu hutaki kutumwa
 
Field maana yake ni upungufu wa vifaa hayo mambo mlipaswa kujifunza hukohuko Chuoni ili ikifika likizo ni kwenda kupumzika sio tena kwenda kujifunza ati mafunzo kwa vitendo.
 
Next time jaribu breweries yoyote!

Kuna mwana alikuwa anaipa credits sana way back akiwa anachukua Electrical Engineering.
 
Back
Top Bottom