Kwani kesi ya Lissu haiwezi kurushwa na vyombo vya habari?

Kwani kesi ya Lissu haiwezi kurushwa na vyombo vya habari?

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
34,954
Reaction score
80,256
Sheria inasemaje? Kesi kurushwa live...

Mahakama haiwezi kuingiza mamia ya watu ila wakii-stream kesi hata tulioko vijijini tunaangalia.

Sijui sheria inasemaje?

Au vyombo vya habari havijawahi kuona umuhimu wa kurusha kesi!

Au sheria inaruhusu wanahabari wanahofia kuwa blackmailed na dola.

Binafsi naona kushawishi watanzania waje mahakamani ni kutafuta umaarufu tu na kuleta congestion isiyo na maana. Tafuteni vyombo vya habari virushe kesi...mtakuwa mmefikia watu wengi saana.

Maoni binafsi.
 
Sijajua wakili wa lissu atakuwa nani ila kama ni kibatala basi huitakii mema serikali maana sio kwa kuaibika huko.
 
Mleta mada uliisoma ile charge sheet? Sasa ule utumbo unaweza kuanikwa hadharani dunia uusikie.
 
..Jaji Mkuu kasema sheria inataka wananchi wapate taarifa za mashauri, na haisemi kesi zirushwe mubashara.


..lakini kwa uelewa wangu kama sheria iko kimya kuhusu jambo fulani basi maana yake haijakataza.

..Na kama Jaji Mkuu anasema wananchi wanatakiwa kupata taarifa, basi matangazo mubashara ni njia nzuri ya kuwapatia wananchi taarifa toka mahakama kuu.

..Na kama waandishi kutoka makampuni ya magazeti wanaruhusiwa mahakamani, basi ni busara, na haki, kuwaruhusu wenye vyombo vya televisheni kurusha, au kurekodi mashauri yanayoendelea mahakamani.
 
Back
Top Bottom