..Jaji Mkuu kasema sheria inataka wananchi wapate taarifa za mashauri, na haisemi kesi zirushwe mubashara.
..lakini kwa uelewa wangu kama sheria iko kimya kuhusu jambo fulani basi maana yake haijakataza.
..Na kama Jaji Mkuu anasema wananchi wanatakiwa kupata taarifa, basi matangazo mubashara ni njia nzuri ya kuwapatia wananchi taarifa toka mahakama kuu.
..Na kama waandishi kutoka makampuni ya magazeti wanaruhusiwa mahakamani, basi ni busara, na haki, kuwaruhusu wenye vyombo vya televisheni kurusha, au kurekodi mashauri yanayoendelea mahakamani.