Kwani Kikwete alikuwa anatumia mbinu gani kuiongoza nchi? Ajira zilikuwa kila mahala

Population growth, na huko mbele ndo noma zaidi wahitimu watakua wengi kuliko ajira
Sema mipango mibovu iliyoanziq kwa jpm. Jpm asingekuwa rais tungefika mbali sana na unemployment rate ingekuwa kidogo sana
 
watu wanazaliana ovyo ovyo kama nzi, unategemea nini, population inakimbilia 70m sasa
 
kiukweli magufuri alimuachia samia mzigo wenye lawama kubwa sana.lakini mama wawatu hakujigamba..amepambana/anapambana kimyakimya kusawazisha mashimo makubwa. makubwa.
nafikili mzigo alioachiwa samia,ingekua samia ndio kamuachia magufuri sijui ingekuwaje.
 
Wastani wa kipato cha mtu wakati Kikwete akiwa madarakani iikuwa ni $1000 leo miaka karibia kumi tuko $1,200, hiki ni kiwango kidogo sana cha ukuaji kwa takribani miaka 10, hii inaamanisha population yetu kubwa iliyoongezeka iko katika kutumia zaidi(tegemezi) badala ya kuzalisha na saving zaidi jambo ambalo sio rafiki kwa uchumi.
 
Jpm aliplay role gani kukuza private sector zaidi ya kuiua
 
Walimu na madaktari wanahitajika sana ku accomodate hiyo number. Tungetegemea ile system ya jk ingeendelea
Nchi ina mambo mengi ya kushugulikia zaidi ya walimu na madaktari, kuna ulinzi, barabara, bandari, kilimo. Bajeti kubwa zaidi ya nchi huwa inaenda kwenye ulinzi na miundombinu. Hapo bado hatujazungumzia matumizi makubwa ya matrilioni ya serikali yasiyo na tija katika kuongeza uchumi kama vile manunuzi ya ndege, magari ya kifahari na korosho.

Uchumi wa Tanzania unavyokuwa unatakiwa ukuze sekta ya Hospitali na shule nyingi zaidi za binafsi ili watu waajiriwe na kampuni binafsi. Ilitakiwa kuwe na hospitali nyingi za hadhi ya Muhimbili za binafsi. Uchumi unaondelea kwa kutegemea zaidi ajira za serikali huwa una changamoto nyingi na ukomo pia.
 
Unafikiri jpm angeendelea kuajiri angejenga bwawa la nyerere na SGR?,maendeleo yana gharama zake
Hapa ndipo tatizo linapoanzia, kwenye uchumi imara serikali haitakiwi kuwa mwajiri mkuu wa kutegemewa.
 
Sio kuajiri tu ata annual salary increment ilikuwa wakika pamoja na kupandishwa madaraja.
 
Jpm aliplay role gani kukuza private sector zaidi ya kuiua
Hakuiua, aliitelekeza. Private sector ya Tanzania ni tegemezi sana kwa serikali( na hii ni by design), pale serikali inapoamua kutoa mkono ndipo inayumba kama mlevi. Serikali ikisitisha semina na mikutano yake kwa mahoteli binafsi yanayumba, tenda kubwa za ujenzi zinategemewa za serikali, kuna benki zinategemea zaidi watumishi wa serikali na serikali kuhifadhi na kukopa pesa huko, hata vyombo vya habari vinategemea zaidi matangazo ya serikali na bahasha za viongozi!. Poor us.
 
Aliiua kwa kuwathreaten yaani alikuwa unpredicatable hujui leo ataamka na lipi. Ki ufupi nchi haikuwa inaongozwa kwa sheria bali matakwa ya mtu. Wawekezaji wako sensitive sana hii risk
 
Kikwete aliongoza nchi kisela sana , Ana fanana na Baba anaehudumia familia na Mtaji wa biashara huku watoto wakiamini baba mpambanaji ndio maana maisha mazuri .Staili yake ilikuwa sio stahimilivu ilikuwa inadidimiza uchumi in long run....Huwezi kuajili kwa wingi huku una Portfolio mbaya ya uimara wa uchumi..Ndio maana kipindi za uongozi wake hela yetu ilishuka thamani sana kutokana na kuitengenezea serikali mzigo
 
Tukiwaambia rais awe mchumi mnakataa hv population inavyo ongezeka sindio na ajira inabidi ziongezeke?
Huo ni uchumi uchwara, population inavyoongezeka sio lazima ajira ziongezeke, ajira zitaongezeka kama teknolojia nayo inaongezeka inapelekea ukuaji wa biashara. Pia ukuaji wa idadi ya watu lazima uendane na ukuaji uchumi na kuna kiwango "optimum" cha idadi ya watu katika nchi kwa nyakati tofauti.
 
Kwamba haya unayosema yalitokea gafla jiwe alipoingia madarakani?
Approach ya Magu ilikuwa tofauti.
Unakumbuka alivyoingia tu akaanza kuhakikisha kama hizi ajira ni sahihi, watu Wana sifa au la!
Maana watu walikuwa wanaajiri majina hewa tu ili wapige hela.
 
Unasemaje? Ni kipindi gani uchumi ulikuwa stable kama kipindi cha jk? Stability ya uchumi ni imports na exports ziwe balanced. Kipindi cha jk mpaka akina obama na jiping walikuja kuangalia fursa tanzani. Jpm alivuta madictator wenzake tu akina kagame na museni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…