Una point hapa, na hili ni tatizo la waandishi wengi Tanzania. Kuna wakati unasikiliza interview, hadi unashangaa huyu ni mwandishi au hustler tu? Utakuta mtu anamhoji Lissu wa Chadema, halafu anauliza unafikiri CCM watafanyaje baada ya Chadema kuamua hivyo?
Kwa mfano, mwandishi professional hawezi kuuliza swali linalotokana na tetesi, lakini asilimia 95% ya waandishi wa habari Tanzania utakuta wanauliza swali kama "kuna tetesi kwamba unatembea na mke wa bosi wako, je ni kweli?".
Nakumbuka kulikuwa na hadithi, sijui kama kweli, kwamba kuna mwandishi mmoja Kenya sijui, alimuuliza Nyerere, baada ya Vita Vya Kagera kwisha, "kuna tetesi kwamba Tanzania mnataka kuikalia Uganda, je ni kweli?" Ilisemekana Nyerere alimjibu "wewe ukisikia tetesi unaziamini bila kuzifanyia utafiti kupata ukweli? Kwa hiyo kukiwa na tetesi kwamba mimi ni baba yako, nilitembea na mama yako, utaamini kwa sababu tu kuna mtu kasema hivyo?"
Na wakati fulani, akihojiwa na waandishi wa habari, Nyerere alikasirika akataka kukatisha mahojiano kwa sababu walikuwa wanamuuliza maswali ya tetesi.