Kwani kuotea ndevu nyumbani ndio kigezo cha kufukuzwa? Naambiwa nikajitegemee wanataka (wazazi) nife kwa njaa!

Komaa kabisa usiondoke hapo ni nyumbani kwa wazazi wako. Waambie kama wanaona vipi wao ndio waondoke hapo waende kwa wazazi wao!

Vipi dada wa dar ameolewa?
 
Pole sana Brother, kimsingi umeshakuwa mtu mzima kwa umri kama wako wapo ambao wameshaoa na wameanzisha familia. Sidhani kama kuna mzazi anapenda kuona kijana wake anateseka, hilo sitaki kuamini. Ila ipo hivi wazazi wanapokuona hapo nyumbani kila siku na wewe umetulia tuu hauonyeshi jitihada yoyote ya matokeo chanua wanaingiwa na uchungu sana, wanawaza mengi walikusomesha kwa gharama ili ukimaliza shule ukajitegemee sasa kwa nn umebaki nyumbani? Kingine kibaya zaidi wewe ni mtoto wa kiume wanaamini ni mjanja mjanja mbona haonyeshi kupambana kama wengine? Afadhali ungekuwa wa kike wangesema ni salama zaidi kubakia nyumbani usije ukabebeshwa mimba ikawa balaa jingine! Kwa hiyo ushauri wangu anza kufikiria nje ya box, jaribu tuu kuonyesha nia ya kufanya jambo hata kama ni nje ya taaluma yako, utaona wana muitikio wao.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Osha vyombo kwanguvu zako zote ili kuonesha ushirikiano katika utafutaji hapo nyumbani

Hautosikia tena kelele

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Tafuta kazi yeyote Halali unayoweza kuifanya dogo! Jichanganye na vijana wenzako wapambanaji huku ukisikilizia ajira

Wazazi sio wanakufukuza wanakuboost ujitegemee

Mi niliondoka home mwenyewe nikiwa around 19s
 
Huwa nashangaa sana jitu linakaa kwao linafuga ndevu nyingi kuliko Baba yake anaelilisha, tena linaweka na kuza na super black ili ziwe kama za Rick Ross, Ndevu zina heshima yake kwa mazingira yake vinginevyo utaonekama muhuni usiwjielewa.
 
Ndevu nitazipunguza ila kuhusu kuhama kiukweli itakuwa ngumu
Vizuri, Na hakufukuzi hujaelewa tu anajaribu kukwambia umekua fikiria kujitafuta na kuhama hapo kwa faida yako siku si nyingi mwenyewe utawashwa kutaka kua na kwako.
 
Mimi nilitimuliwa home nikiwa na miaka 22 tu mzee kaniambia nioe au nikavue dagaa,niliondoka kweli na form four yangu ya 26 nikaingia mtaani nilianza kuchoma mawe na kupasua nauza nikawa nasukuma na mkokoteni kama mwaka mmoja hivi huku naishi kwa mama mdogo mwaka uliofuata nikaenda veta nikagonga miaka mitatu fani bomba nikakomaa mwenyewe kila kitu ndani ya miaka mitatu pale musoma na ule wa kupiga kazi ya mkokoteni ukawa mwaka wa 4,2016 nikamaliza mafunzo yangu nikakaa miaka 4 2020 ndo nikapata ajira leo hii mzee anapiga simu sana anaomba pesa nampa na mpaka sasa nasomesha mdogo wangu anachukua diploma ya civil engineering
Pengine wanataka ukajitegemee akili ifanye kazi
 
Hii thread imebid niscreensot itanisaidia kufundishia vijana wangu hapo badae,
hakika kila andiko lafaa kwa mafundisho bado wewe ni wa muhim tunakuhitaji kama mfano mbaya usiepaswa kuigwa.
 
Hii thread imebid niscreensot itanisaidia kufundishia vijana wangu hapo badae,
hakika kila andiko lafaa kwa mafundisho bado wewe ni wa muhim tunakuhitaji kama mfano mbaya usiepaswa kuigwa.
Unamuuliza upo mkoa gani anasema yap
 
Sasa wewe unatrade forex au unapeleka pesa zako kwa big boys maana kama unatrade forex alafu huna kazi nyingine kuna mawili aidha ufilisike au uwe unapata mkwanja wa kutosha.
sasa wewe unatrade hupati faida that's means huwa unapata hasara, aya ukipata hasara huo mtaji mwingine unatoa wapi? acha kutudhalilisha watu ambao hii game inatupa maisha!
Au ni kamba moja safi ya mkonge kutoka tanga korogwe
 
Sikujua utaishia kunitusi badala ya kunisaidia mawazo yakung'ang'ania haki yangu yakubaki nyumbani
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…Daah mwanangu we hovyo sana, haki yako? Sasa itakusaidia nini hiyo haki? Mwisho utawaua wazee wako urithi wewe ndo unakoelekea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…