Kwani lazima kuoana?

kwakweli I like the attitude...
 
ndoa tamu sana jamani!...........
acha kabisa...........


Nilijua Geoff naona wewe unakula raha ya ndoa sasa..
Ni tamu ukiipatia
Ni chungu kama shubiri pale inapokosewa
heheheheh weekend yako ikawaje kwani ..mie nilikuwa mitaa ile..........
 
Page layout inanikwaza hata kuchangia naona uvivu. I hope the mods are busy doing something about this.

Masaki kweli kabisa hii layout ni issue lakini taratibu mabadiliko yatafanikiwa .
 
wanawake wa kuwaoa wako wengi sana.....tatizo wanaume huwa hawajiamini mpaka wasikie fulani kaolewa wanajuta!

dada 32 mbona ni kidogo sana kuanza kuseme utaolewa na yoyote?! .......idea ya kumuonyesha mwanamme kuwa desperate tu tayari itamfanya akutese atakavyo kisha asikuoe
 


Hiyo (kwenye red) ni miscalculation. Yaani wanajaribu kutangazia umma kwamba wako tayari kufanya lolote ili waolewe? Inaonesha kwamba they are daying for marriage. Na kwa wanaume wakware basi hizo ni sketi rahisi za kuvua hata ikiwabidi kuokoka.


FL1, mwambie huyo rafiki yako aelewe logic rahisi. Kuolewa ni muhimu lakini siyo lazima. Huwezi kufa kwa sababu hujaolewa. Na katika suala la kuoa/kuoelewa, mtu akikosa kitu alichotaka au kutamani, inabidi apokee alichojaliwa na Muumba. Na hapo kuna uwezekano wa kupata mwenza au kukosa kabisa. Akubali kuwa anaweza kupata mume akiwa na uweza wa kusubiri lakini pia ajue kuwa anaweza kukosa kabisa. Nina ndugu yangu (miaka >50) ambaye alikosa mume kabisa. Ila yeye aliamua kuzaa na mtoto wake ni mkubwa tu.
 
thanks Gaijin lakini je kama mme haonekani unaweza kuamua kujipatia katoto kako kisha una-close chapter ama wewe unaonaje ?

Mimi naamini inauma zaidi kukosa katoto japo kamoja kuliko kukosa kuolewa. Avute SUBIRA na kuendelea KUMUOMBA MUNGU apate Mume, ikiwa pamoja na KUONYESHA MAADILI MAZURI kwa jamii inayomzunguka. Lakini atakapofika 36 bado hajafanikiwa kupata mume, Namshauri atafute mbinu za KUJIPATIA KATOTO japo kamoja ka kumfaa maishani. Cha muhimu hapo ni kushukuru Mungu tu hata asipopata Mume, ndicho alichoandikiwa/alichoamua Mungu huenda kuolewa kungemtesa.
 
Ngoja Nirudi kwenye maandiko nijue yanasemaje kuhusu suala hili...
 
Waliomo Ndani wanataka kutoka walio nje wanatamani kuingia kwenye Boti hii

tulioko ndani tunatamani tufie huko...au Bwana aje atuchukue kama yanenavyo maandiko...
umri sio issue kabisa hapa, awe mvumilivu atapata mzuri tuu, nimeshaona harusi/ndoa za wengi ambao bi harusi ni 40yrs au zaidi na kuhusu watoto unaweza kuingia kwa mkwara wakupata watoto ukakukuruka hadi ukakoma, watoto ni zawadi kuoka kwa Mungu...au ukikosa watoto ataolewa tena na mwingine.
32 mbona bado hot sana, awe na subira...vitu vitamu na vizuri kama ndoa haviitaji haraka kama kununua RA4 short chasis ambayo ikikukera unauza unanunua nyingine.
mlete kwangu nimshauri zaidi
 
mie huwaga najiulizaga pia,kuolewa na kuzaa watoto ni kitu must??? as a young woman...i dont want any of this...nikisemaga hivi kila mtu ananishangaa???labda nikifika huko nitajutia.ila kwa sasa am 26 and yes I DONT WANT TO GET MARRIED..AND I DONT WANT CHILDREN!!........huyo dada nadhani anahitaji moral support....!!
 

Mpendwa First Lady wa kwanza;
Kwanza Signature yako nimeipenda. Ubarikiwe na Bwana.
Pili kuhusu huyu dada mie "Mchungaji" nashauri hivi: - Mungu aliyemuumba anamjua, hivyo amemtayarishia mwenzi wake wa Maisha. ASUBIRI. AINGOJE AHADI YA BWANA MUNGU KWAKE.
 

Desperation ni kitu kibaya sana kinachoweza kumsababisha mtu kufanya mambo ya ajabu ajabu. Huyo dada kwa kudai kuwa mwanamume yeyote atakayetokea mbele yake ataolewa naye basi ni ishara tosha kuwa yuko desperate. Mademu wa aina hii nimeshakutana nao wengi sana. Ni rahisi sana kuwamega mademu walio ktk hali hii. Sasa huyu wa FL1 naye asipoangalia (kama bado hajaanza) atamegwa kama kuku halafu atakuwa anaachwa kwenye mataa. Kwa uzoefu wangu mimi na mtazamo wangu, wanaume wengi kwa kawaida hawapendi wanawake walio desperate.

Ila huwa sielewi kwa nini mtu uwe desperate na kuolewa au kuoa. Ndoa kwangu mimi si wajibu wala lazima bali ni hiari. Mimi nimeamua sitaki mambo ya ndoa. Siyawezi masha ya ndoa na huo ni uamuzi nilioufikia kwa hiari yangu. Sasa sielewi kwa nini wengine watape tape hadi kufikia kutoa kauli kama hizo. Nilishagawahi kukutana na mdada mmoja miaka kadhaa iliyopita na akaniambia kuwa akifikisha miaka 30 na bado hajaolewa basi atazaa mtoto na mwanamme yeyote yule bila kujali kama huyo mwanamme atashirikiana naye ktk kumlea mtoto. Nilitikisa kichwa changu tu na wala sikusema kitu.

Ndio maana kila siku ipitayo nashukuru niliumbwa mwanamme maana wanawake wana kazi sana aisee. It's hard out there for women.
 


hapo kwenye kuolewa sawa, lakini mtoto/watoto pia...ni ngumu kidogo.
 

Bora leo hujaandika kiblurei,nimekuelewa kweli.
 
Kutokuolewa ni tatizo ndiyo hasa ukizingatia malengo aliyo nayo katka maisha: kutaka kupata familia yake (kuwa mke wa mtu) na kupata watoto kutoka kiunoni mwake. Kwa hali hiyo kuolewa ndiyo jibu. Kwani naamini hataki kuishi kihuni, bali kuishi akiwa na heshima yake katika jamii.
 
Reactions: Cyb
Kwani naamini hataki kuishi kihuni, bali kuishi akiwa na heshima yake katika jamii.

Hii ni dhana potofu! Ni nani anayetoa mamlaka ya kuamua kuwa wale ambao hawajaoa au kuolewa ni wahuni? Uhuni ni nini?
 
Very well said.Yani watu tunapenda kuhukumu sana.Yani mtu asipoolewa/oa basi ni mhuni?

Sasa sijui na wale waliooa na kuolewa na wanatoka nje ya ndoa zao sijui tuwaiteje? I guess wao wanaheshimika zaidi na "jamii" kwa vile wako kwenye ndoa....
 


heshima ya mtu inakamilika kwa kuoa/kuolewa?....cku hizi mbona kwenye ndoa uhuni ndio kiboko?.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…