Matola, suala la kuoa, si jambo baya, bali ni jambo jema linalopendeza mbele za Mungu na wanadamu pia! Lakini si jambo linalohitaji kukurupuka au kushinikizwa, ni jambo ambalo huitaji utayari wa mhusika kiakili na pengine hata kiuchumi. Zaidi ya hapo suala hili pia hutegemea kama mhusika amepata mwenza kwa maana ya wife material ambaye atakuwa tayari kuchukuliana nawe kwa namna zote za raha na shida. Choice ya partner si jambo la kukurupuka na hivyo huwezi kulifanya kwa kushinikizwa.
Under ideal situation, tunategemea ndoa ilete amani, furaha, baraka, ijenge familia na kumfanya mume na mke kujua wajibu wao iwapasavyo ndani ya familia yao kwa kuzaa na kuwalea watoto wao ipasavyo. Na pia tungetegemea ipunguze uzinzi (Ingawa baadhi ya wanandoa bado ni wazinzi!), na kuongeza heshima ya mtu nyumbani na kwingineko.
Nina wasiwasi kuwa inawezekana wanakushinikiza kwa kuona kuwa labda ka umri kako kamesogea sana, au age mate wako wote wameoa au una uwezo wa kujimudu wewe na familia tarajiwa au pengine unakutwa ukibadili vibinti kila mara kiasi cha kuwatia ukakasi mashuhuda wa hizo tabia!
Mkuu nakubaliana na wewe, kwamba si jambo la busara kuoa kwa kushinikizwa hasa ukizingatia unyeti wa taasisi yenyewe na complications zake. Ila pia si vibaya kama ka umri kamesogea sana, na kama umempata yule ambaye umempima ukaona anafaa, kujitumbukiza kwenye taasisi hii. Lakini kama hivyo vigezo hujavifikia, basi kaka endelea kuwepo kuwepo tu!
Best of luck,
HP.