nyamayao unajua hapa kuna mambo mengi yanachangia ila nadhani lawama zinafaa ziende pande zote mbili. Ingawa kiini cha yote hayo ni mwanamke kwa sababu yeye ndiye mwenye uwezo na kauli ya mwisho ya kusema YES au NO ili uovu huo utendeke. Kuna vitu vingi vinachangia but mimi ninaona hivi (na ninakubali kukosolewa!)
Mpaka hapo uko uko sahihi kabisa. Lawama nyingi zimwendee mwanamke.
-1.Mwanamke unapokuwa na mwenzi wako hasa mbele ya marafikize tupunguze manjonjo jamani
Hapa ndipo unapoanza kukosea. Unapotumia neno "hasa" una maana gani? Una maana huyo mwanamke apunguze manjonjo tu awapo mbele ya marafiki wa mwanamme wake na akiwa mbele ya wanaume wengine it's okay? Wrong! Inatakiwa
aache,
sio apunguze, aache hayo manjonjo mbele wa mwanamme yeyote zaidi ya mumewe. Vivyo hivyo, mwanamme naye anatakiwa aache "manjonjo" yake mbele ya wanawake wengine wawe marafiki si marafiki wa mkewe. Anatakiwa aache hayo unayoyaita "manjonjo". Kama wote hamuwezi kuacha basi hamkuwa tayari kuishi maisha ya ndo in the first place na ndoa yenu tayari iko doomed kabla hata hamjaifunga.
utamkuta mtu yuko na hawa shemejize na mpenziwe basi mara kaingiza ulimi sikioni mara kamtafuna ulimi yaani ili mradi atoe picha kuwa mpenzi wake anafaidi sana. Sasa hivi vinaweza kuwatia marafiki shetani wa wao pia kutamani kuenziwa kama vile japo mara moja (ingawa wanatakiwa kujizuia) ndiposa mtu anaanza kumtongoza mke/ demu wa rafikiye ili tu aonje pepo apowayo mwenzie.
Kama couple wako comfortable na PDA sioni kwa nini wajizuie kufanya hivyo. Heck...si uhusiano wao bana? Sasa mwanamke kwa ujumla huwezi kabisa kumzuia mtu kukutongoza. Ila kama uko
mwanamke mwenye maadili mazuri na unamheshimu mumeo, kwanza, utaji-carry kwa heshima na utakuwa na aura flani kwamba
you don't play that na watu wakikuangalia tu mara nyingi wata sense kitu kama hicho. Pili, ikitokea umetongozwa na mtu wakati uko mke wa mtu unatakiwa umwambie huyo akutongozae kwamba umeolewa. Mwambie kwa heshima tu na wala sio kwa hamaki. Sio unam entertain huyo akutongozaye. Kwa nini um-entertain mwanamme mwingine wakati uko mke wa mtu? Huko ni kumdharau na kumdhalilisha mwenzi wako.
-Pia tunapoonyesha sana manjonjo mbele ya hao mashemeji wengine hutafsiri kuwa unamkaribisha kiaina so anapata nguvu ya kukutokea.
Wewe huwezi kuzuia jinsi matendo yako kwa mumeo yanavyopokelewa na watu wengine. Usijali jinsi watu wengine watakavyoyapokea au kuyatafsiri. Inapotokea unatokewa na jamaa kataa. Mwambie umeolewa na unampenda mumeo na kamwe hata siku moja hutafanya kitu kama hicho. Kataa katakata. Kwa nini uanze kuichekea chekea hiyo njemba ingine. Why? Si uko mke wa mtu? Basi kama ni hivyo mpende na mheshimu mumeo na yeye anatakiwa afanye vivyo hivyo kwako.
2. Tujaribu kuweka distance kati yetu na mashemeji (na userious flani) hivi kwani shemeji akiona unamchekea chekea hata kama ni kwa nia njema basi yeye ashakuteremsha kivazi. Ukiwa na distance na userious flani ni wazi kuwa hata ile wazo la kufikiria kujaribu kukutongoza halitakuwepo.
Sio tujaribu. Ni kwamba ni lazima uweke umbali kati yako na mashemeji zako na wanaume wengine zaidi ya mumeo. Lazima mheshimiane na shemeji yako/zako. Kama shemeji yako anakutongoza na wewe unakubali basi wewe ndio mjinga na mdhaifu zaidi kuliko hata alivyo huyo shemeji yako kwa sababu you should know better.
Where are our manners? je wazazi wetu nao zama hizo walikuwa wakifanya haya? kama hapana ni kwa nini?
Haya mambo yalikuwepo tokea enzi na enzi na yatakuwepo kadri uhai wa mwanadamu utavyoendelea kuwepo. Hakuna cha ajabu hapo.